Jana jumamosi nilikuwa nasikiliza kipindi cha Tunu Zetu radio Amani ya jimbo katoliki Arusha. Padri alikuwa na mada ya Utatu Mtakatifu ambayo aliianza na ataendelea nayo. Niliwahi kupeleka hoja kwa Madrid, maaskofu na wanateolojia wakatoliki kwamba Mungu ni mmoja aliyejidhihirisha katika namna/nafsi tatu tofauti. Uumbaji (Baba), ukombozi (Mwana/Yesu), utakatifuzaji/uongozi (Roho Mtakatifu). Huyo ni Mungu yuleyule. Hoja hiyo ikapingwa. Jana padri mkatoliki akasema hayohayo! Akasema ukienda huko "mbinguni" hutakuta hao watatu kama "three distinct beings". Mungu ni mmoja tu. Najua yako madhehebu mengine ya kikristo yanakubaliana kabisa na teolojia hii. Wakatoliki mbona tena mnakinzana?? Huyu padre naye amesoma kwenye seminary na vyuo hivyo hivyo na mtaala huohuo. How comes then the interpretation of the Trinity differs? Hebu wekeni hapa hoja zenu.