Mapadri na wanatheolojia wakatoliki mbona mnatofautiana kuhusu Utatu Mtakatifu?

Jinsi ulivyoandika, na namna ulivyoandika, wewe siyo mtu uliye na afya njema ya kichwani. Ni mtu wa kuonewa huruma kwa kunyimwa utimilifu wa afya ya akili. Mwenye akili timamu angeweka hoja yake, kukubali au kukataa, bila ya kumtusi mwingine.

Hakuna mwanadamu mwenye kumfahamu Mungu kwa 100%. Mwanadamu amefunuliwa kidogo sana kumhusu Mungu, ndiyo maana Yesu, Kristo alisema kuwa hakuna amjuaye Mungu isipokuwa yeye pekee aliyetoka kwake.
Yesu anasema kuwa Yeye ameketi kuume kwa Baba. Ulishawahi kujiuliza ameketi kuume kwa Baba, ameketi akiwa katika hali gani?

Jambo pekee unalotakiwa kufahamu kuwa kama.Mungu aliweza kuwafanya baadhi ya watumishi wake waonekane zaidi ya sehemu moja kwa wakati mmoja; na tunaamini Mungu ni muweza wa yote, hivyo hawezi kushindwa kujigawanya katika nafsi, au kutokea katika namna tofauti tofauti. Lakini nafsi pekee iliyowahi kuonekana katika umbile la mwanadamu, huku ikiwa na nguvu ya kiMungu, na Yesu Kristo, na ndiyo jina pekee alilopewa mwanadamu kwaajili ya wokovu wake. Na ndiyo nafsi pekee iliyopewa mamlaka ya kuwahukumu wanadamu.
 
Kabla ya maneno ya kashfa(MPUMBAVU, WAPUMBAVU), unge-halalisha unachoamini kuhusu NAFSI kuwa ni maana Universal kwa ushahidi kisha ndo uendele na UPUMBAVU wowote ule uliokusudia kuuweka bayana, ingekaa vizuri sana!
Exactly correct.
 
Kama hoja ni hiyo basi hata wanao abudu sanamu wapo sahihi maana mungu anaweza kujigeuza sanamu...tumia akili hakuna mungu mwenye nafsi zaidi ya moja
 
Kama hoja ni hiyo basi hata wanao abudu sanamu wapo sahihi maana mungu anaweza kujigeuza sanamu...tumia akili hakuna mungu mwenye nafsi zaidi ya mpja
Mmmmmh. Wewe unadhania kwamba Mungu anaweza kutafsirika kwa akili yako ya kibinadamu. au Kwa maneno marahisi kwamba unaweza kumweleza Mungu ni wa namna gani. Kamwe hautakaa uweze. Utajizungusha-zungusha na maelezo lakini maelezo yako hayatakuwa na mashiko yatakuwa na kasoro siku zote. Ndo mana wale wenye Hekima walifikia mahali wakakiri na wakasema Mwacheni Mungu aitwe Mungu yenye chimbuko lake kutoka Zaburi 46:10
 
Mungu kajieleza yeye mwenyewe vizuri tu ...sasa kama una amini mungu aelezeki mbona mnamuelezea kuwa ana nafsi 3...kwa hiyo tuamini hoja zenu na tukanushe hoja zetu .....Mungu kajielezea vizuri kwenye biblia kuwa yeye ni mmoja nafsi moja tena kuna maandiko kabisa mungu anauliza ..je tuwe zaidi ya mmoja ili mimi mungu nifanye amani na miungu mingine ?
 
Mungu kajieleza yeye mwenyewe vizuri tu ...sasa kama una amini mungu aelezeki mbona mnamuelezea kuwa ana nafsi 3...kwa hiyo tuamini hoja zenu na tukanushe hoja zetu .....

Mungu kajielezea vizuri kwenye biblia kuwa yeye ni mmpja nafsi mpja tena kuna maandiko kabisa mungu anauliza ..je tuwe zaidi ya mmoja ili mimi mungu nifanye amani na miungu mingine ?
Ni vifungu gani ? -naomba link mkuu.
 
Unasema nimtumie Roho Mtakatifu kuelewa neno la Baba au la Mwana? Do you see where you contradict yourself???
 
Biblia ndio msingi wa imani yetu ndugu. Weka bidii kusoma biblia.
Faith without reason is STUPIDITY. Tumpende Mungu kwa akili siyo imani pofu. Huo ni ujinga uliojengwa na mamlaka kudhibiti watu.
 
Reactions: Lax
Ninashukuru na nimefurshi sana kwa mchango wako. Je kanisa limekataa hadharani Modalism? Katekisimu katoliki imerekebishwa? Huu uelewa unaweza kuwa nao wewe kama mwanatheolojia makini lakini wanachofundishwa wakatoliki na baadhi ya madhehebu kuhusu Utatatu ni tofauti kabisa. Where is the public declaration of the church that it has abandoned Modalisim??? Waumini bado wanaona kwa mujibu wa mafundisho kwamba baba mwa na roho mtakatifu ARE THREE DISTINCT BEINGS!
 
Bado unarudi palepale kwamba miungu ni watatu. What was your point. Acknowledge that there are three distinct beings or God has three manifestations.
 
Asante sana. Mungu amejieleze mwenyewe ili tumuelewe. Watu wanatunga maneno yao ili kufunika jambo ambalo Mungu ameliweka wazi.
 
Biblia ndio msingi wa imani yetu ndugu. Weka bidii kusoma biblia.
Ukisoma biblia kama gazette
Inashangaza jinsi binadamu anavyoweza kuwekeza nguvu zake kuumiza kichwa chake kwa kujadili fiction!
Nimecheka mpaka mhudumu wa hapa mahali nilipokaa akaniuliza mzee vipi tena au kuna msiba? Maana alidhani nalia. Kweli inashangaza.
 
Madhehebu yote ya kikristo yanadai kuongozwa na Roho Mtakatifu, yet they disagree on basic doctrines. Kwa wengine Mungu ni mmoja tu, wengine ana nafsi tatu (three distinct beings of one nature), wengine Yesu ni Mungu , wengine Yesu aliumbwa na Mungu, wengine Roho Mtakatifu ni Mungu na wengine Roho Mtakatifu ni kani/nguvu ya utendaji wa Mungu. Kila mtu ana Roho Mtakatifu wa kwake kwa hiyo usilete kabisa habari za kuongozwa na Roho Mtakatifu. Au unataka kusema kwamba Roho Mtakatifu wako
ndiye wa kweli kuliko hao wengine????
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…