Mapadri wakizeeka wanapewa mafao ya kujikimu?

Mafao ya kujikimu wajikimu nini sasa..

Kwanza wao hua hawastaafu Kama watumishi wa uma,wakifikia umri wa uzee huendelea kutunzwa kwenye nyumba za mapadre mpaka mwisho wa maisha yao.
Mafao ,umeona anawajukuu au mitoto ,akipewa mafao ni ulafi huo
 
Tumewaongelea mapadre vyakutosha, hebu na upande wa ubwabwa nako, masheikh wakistaafu wanapewa pensheni au posho yoyote?
 
Kanisa katoliki haliamini katika utimilifu bali linaamini kuwa kuna kuanguka katika dhambi. Ndiyo maana kuna utaratibu wa kuungama dhambi kwa mwanadamu yeyote hata akiwa Askofu wa Roma (Papa). Hata Padre anategemewa kuanguka katika dhambi naye hutubu na upadre wake kuendelea. Dhambi husika inaweza kuzaa matokeo ambayo huwezi kuyafuta kama mimba hadi mtoto.

hivyo ni ukengeukaji kusema mapadre wana watoto. Hivyo waruhusiwe kuoa. Maana yake ni kuwa walitenda dhambi na kanisa liwaruhusu waendelee kutenda dhambi.

nasisitiza hakuna Padre bila useja. Useja ukimshinda Padre, anasepa na hakuna anayemkataza kama Dr Slaa.

jaribu kutofautisha dhambi na ndoa.

Aidha kuna mapadre waliooa kwa taarifa yako. Hao ni wachungaji wa Anglican Church wanaokubali kurudi RC wanakubaliwa kwa utaratibu maalum na Askofu wa Roma. Barikiwa
 
Aidha kuna mapadre waliooa kwa taarifa yako. Hao ni wachungaji wa Anglican Church wanaokubali kurudi RC wanakubaliwa kwa utaratibu maalum na Askofu wa Roma. Barikiwa
Una ushahidi wa Padre yeyote yule wa Anglikana hata mmoja tu aliye kubaliwa kurudi RC kwa huo utaratibu maalum unao usemea na huyo Askofu wa Roma?

Au umeamua tu kuchapia?
 
Mi nijuavyo kwa ufahamu wangu mapadre wa Rc wengi wao huhudumiwa hadi mwisho wa maisha yao,na hakuna watu wanaoishi maisha ufahari kama mapadre,Maisha yao ni raha mustarehe
Mapadre ni VIUMBE WAPWEKE
 
Una ushahidi wa Padre yeyote yule wa Anglikana hata mmoja tu aliye kubaliwa kurudi RC kwa huo utaratibu maalum unao usemea na huyo Askofu wa Roma?

Au umeamua tu kuchapia?
@kolola anafikiri thehebu RC ni sawa na vyama va siasa sawa na CCM au Chadema, uhame huku na ukapewe cheo huko.
Upadre unasomewa na unataratibu na kanuni za kanisa ili uupate.
 
Una ushahidi wa Padre yeyote yule wa Anglikana hata mmoja tu aliye kubaliwa kurudi RC kwa huo utaratibu maalum unao usemea na huyo Askofu wa Roma?

Au umeamua tu kuchapia?
Kumbe huelewi kitu! Bye
 
@kolola anafikiri thehebu RC ni sawa na vyama va siasa sawa na CCM au Chadema, uhame huku na ujapewe cheo huko.
Upadre unasomewa na unataratibu na kanuni za kanisa ili uupate.
Pole sana! Uliza hata Padre yeyote atakueleza ukweli. Mchungaji wa Anglican akiomba kurudi RC atakubaliwa kwa utaratibu maalum kwa vile inaaminika kuwa Anglican walikengeuka tu. Kibali hutolewa na Papa.

 
Padre wa kanisa katoliki ni mali ya kanisa na atatunzwa na kanisa maisha yake yote. Hivyo hakuna mafao yoyote wanayolipwa kwa sababu kanisa linawahudumia kwa kila kitu.Pia upadre si kazi ni wito wa kujitolea ndiyo maana mapadre hawana mishahara.
 
Ni mapokeo tu ya kanisa. Hakuna mafundisho ya moja kwa moja ya Mwenyezi Mungu ya kiwazuia Makuhani wake kuoa. Ingawa Mapadri wa Kikatoliki, mara nyingi hutumia mfano wa Mtume Paulo ambaye kimsingi hakuoa maisha yake yote!
Uko sawa mkuu. Kwa kanisa la Roma maandiko( Bible) is not the final authority! Yaani Imani hizi we acha tu. Anyway, angalau Roma wameamua kupata kimoja, ufalme wa dunia. Kwa walokole feki akina Gwajiboy ,mwamposa, mzee upako nk .huko ndo majanga tupu.
 

Daa muandiko wako ni m baya sana. Unachanganya R L paka unaboa
 
Hello habari Ndugu Nina swali . Hivi mapadre wakikatoliki pale wanapokuwa wazee je wana mafao yeyote ya kuwasaidia kujikimu? Au je pale waumwapo wakati wa uzee wao ni Kanisa linatakiwa kuwahudumia ama inakuwaje! Au wanakuwa wanaishi wapi ?
Wito wa upadri ni utume na anayekuwa padri anajitolea na halipwi mshahara na pia hana mafao yoyote. Isipokuwa tu kwamba kanisa limeweka utaratibu wa matunzo ya wahudumu wao hadi kufa kwao. Kama vile ilivyo kuwa padri aliye kwenye utume anahudumiwa na kanisa, hivyo pia anapougua, zeeka na hata kufariki anahudumiwa kanisa, taifa la Mungu.
 
Maisha ya kutokuwa na watoto,ni maisha ya upweke.
Kama umesoma saikolojia upweke hauletwi na kutooa. Kuna watu wengi sana wameoa na wana watoto na ni wapweke na hawa utasemaje, nao ni mapadri, masista au mabradha?
 

Aise
 
Mkuu unasema "Ipo siku wataruhusiwa kuoa"

Swali langu ni kwamba,

Kwani nani kawakataza kuoa? Je ni sheria ya Mungu au ni binadamu tu ndiye aliyewawekea huo utaratibu?

Nauliza tu kiroho safi ili nijue.
Ni sheria ya kanisa. Ingawa kibiblia siyo dhambi kutokuoa kama unaweza kuishi bila kona kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…