Kwa mtazamo wangu, perfomance ya waziri kwa kiasi kikubwa inakuwa influenced na sera/ilani ya chama na zaidi maono/mtazamo wa mtawala aliyepo madarakani.
Mfano, huyo waziri Jamal uliyemsifia enzi za utawala wa Nyerere kwamba ndie aliyewezesha ujenzi wa viwanda akiwa waziri wake, kiuhalisia kulichangiwa na mtazamo wa Nyerere kutaka hili taifa liwe na viwanda vyake, pamoja na nia ya kuliwezesha hilo iliyokuwepo.
Hili halishabihiani na utawala wa Magufuli ambaye nae alitaka kuiona Tanzania ya viwanda, lakini sikumbuki aliweza kujenga vingapi mpaka mauti yalipomkuta, licha ya yeye pia kuwa na waziri wake wa viwanda.
Napingana nawe unapozungumzia suala binafsi la elimu ya waziri husika kama ndio inawezesha hilo, kwasababu tumeona mara nyingi hapa kwetu, wasomi wakishapewa madaraka huweka elimu zao mifukoni na kugeuka chawa wa watawala.
Hili Nyerere hakuliruhusu, alimuacha mtu mwenye elimu yake afanye kazi kwa weledi kwa maendeleo ya taifa, anastahili pongezi. Hivyo kwangu, kufaulu au kufeli kwa mipango ya nchi, kwa kiasi kikubwa kunachangiwa na maono ya mtawala, kama akiwa mjinga ataliangusha taifa.
Hao mawaziri wote uliowataja hapo juu, sioni ni yupi mwenye sifa hitajika za kulishibisha andiko lako, kwa sababu naamini, wote hufuata mawazo ya mtawala kwenye utendaji kazi wao, wanajipendekeza, hawana uthubutu wa kuanzisha wazo lao na kulifanyia kazi.