Mapendekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha: Igeuze Arusha kuwa ndo "Financial Centre" ya Tanzania na iwe mfano wa mikoa ingine na tafuta washauri maalum

Mapendekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha: Igeuze Arusha kuwa ndo "Financial Centre" ya Tanzania na iwe mfano wa mikoa ingine na tafuta washauri maalum

Mada ina assumptions zilizojengwa kwenye taarifa uwongo na kukosa uelewa wa unachotaka (lack of knowledge in the subject matter), haiwezi kujadilika. Ni kupoteza muda tu
Watu wa aina yako hauwezi kukubaliana na mapendekezo haya.

Nimeongelea mambo ya msingi kabisa kuelewa lakini kwa kuwa hutaki hiyo kitu waendekeza personal attacks.

I have knowledge on the sujbect matter na pengine ninakusaidia hata weye ndugu.

Hakuna uongo hapo wala assumptions.
 
Siyo kweli huwezi kunizidi. Mimi ni ex CEO wa one of public parastatal na elimu yangu ni MBA.

Uliposema Financial hub ina maana unaongelea biashara ya fedha na siyo madini, mahoteli au utalii.

Financial markets ina husisha mfumo unaohusisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za fedha (loans and fixed term deposits), dhamana za Serikali (bonds) fedha za kigeni (International currencies and derivatives), mitaji (stock exchange) etc.

Sasa kwenye mada yako hujagusa huku ndiyo maana nakuona luwa wewe siyo expert kwenye suala ĺa financial markets
 
Mkuu, Arusha watu wanaojifanya wao ni watoa ushauri kwa viongozi ni wengi sana ila mostly wanatoaga theories ambazo ni undoable practically, nimekaa Arusha for 5 years, i know them very well na tena hawa washauri wanatafutaga njia ya kukuweka karibu ili wapitishe mambo yao huku wakikuacha kiongozi na theories ambazo ni ngumu mno kutekelezeka. Wao wabaki na ushauri wao, Makonda atafanya yaliyo ndani ya uwezo wake. Tena i am sending him link ya huu uzi ajionee washauri wanavyoibuka kwa kasi, i warned him and i will warn him again.
 
Yaani ile zero kutoka Koromije ndio umeipa huo ushauri?
Pole mleta mada kwa kupoteza muda wako kuandika hayo yote.

Kukusaidia wewe, fahamu tu, Makonda yeye anaamini anajua kila kitu, hahitaji ushauri wa mtu yoyote, ni jeshi la mtu mmoja lenye kuweza kufanya chochote.
 
Siyo kweli huwezi kunizidi. Mimi ni ex CEO wa one of public parastatal na elimu yangu ni MBA.

Uliposema Financial hub ina maana unaongelea biashara ya fedha na siyo madini, mahoteli au utalii.

Financial markets ina husisha mfumo unaohusisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za fedha (loans and fixed term deposits), dhamana za Serikali (bonds) fedha za kigeni (International currencies and derivatives), mitaji (stock exchange) etc.

Sasa kwenye mada yako hujagusa huku ndiyo maana nakuona luwa wewe siyo expert kwenye suala ĺa financial markets
Mkuu, Financial centre yabeba financial hub na financial markets.

Mimi sijasoma sana kama weye ila nina knowledge ya kutosha na siwezi kujisifu.

Lakini nina bahati ya kutembea na nimetembea kwelikweli dunia hii.

Nazungumzia Arusha kuwa Financial Centre kutokana na hadhi yake ya kuwa tourist destination ya nchi.

Kwa mfano mji wa Shanghai ni financial center ya China kwa sasa. Mji huu zamani ulikuwa ni kijiji cha uvuvi na mji wenye masoko yaani market town na hiyo ni kwenye kuanzia miaka ya 1900s.

Nikisema financial centre ya Tanzania namaanisha mji wa Arusha kuwa financial centre yaani mambo yote ya fedha, uchumi na biashara, Utalii, viwanda na madini kama nilivyoyaongelea kwenye mada.

Unanipata ndugu?
 
Mkuu, Arusha watu wanaojifanya wao ni watoa ushauri kwa viongozi ni wengi sana ila mostly wanatoaga theories ambazo ni undoable practically, nimekaa Arusha for 5 years, i know them very well na tena hawa washauri wanatafutaga njia ya kukuweka karibu ili wapitishe mambo yao huku wakikuacha kiongozi na theories ambazo ni ngumu mno kutekelezeka. Wao wabaki na ushauri wao, Makonda atafanya yaliyo ndani ya uwezo wake. Tena i am sending him link ya huu uzi ajionee washauri wanavyoibuka kwa kasi, i warned him and i will warn him again.
Arusha mie si mkazi ila natembekea mkoa huu safari za kitalii mwaka wa 15 huu.

Mada hii nimeandika nikiwa Tarangire.
 
Binafsi nimeona "potential" yako katika uongozi una uthubutu lakini ninahusudu uthubutu wako huo kwamba utachochea harakati za wananchi kujiletea maendeleo.

Mtu akikwambia kuwa, "samahani umefeli katika zoezi la usaili lakini tumeona "potential" ndani yako, fahamu kuwa bado waonekana una uwezo wa aina fulani na huenda huko baadae ukapitishwa kweye usaili mwingine.

Neno hili "potential" lamaanisha kuwa na uwezo na kuendeleza kitu au mtu kwa ajili ya baadae. Hata mtu akiwa ana duka auza bidhaa, akitokea mteja ambae yupo tayari kununua bidhaa lakini hana fedha wakati huo ila akisema atakuomba uweke bidhaa alochagua pembeni, tayari huyo ni "potential customer".

Kwahiyo umeonekana una "potential" kwa ajili ya baadae nafikiri hichi kitendo kilotokea hivi karibuni ni uthibitisho kuwa una "future" huko mbele.

Hivyo kama kiongozi ulie na dhamana ya kuongoza mkoa ukiwa mwakilishi wa raisi wa Jamhuri ya Muungano, una jukumu la kuja na mikakati hii ikiwa imeweka malengo rasmi yaani kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wa Arusha,kutatua migogoro ya ardhi, kuondoa kero za uhalifu, kuinua uchumi wa mkoa, kupunguza tofauti ya kipato, kuhakikisha kodi yakusanywa, kuwashughulikia kisheria wakwepaji kodi na wabadhilifu wa fedha za kodi hiyo na kusimamia na kuimarisha usalama wa mkoa wa Arusha.

Arusha tayari ni mji wa kibiashara kuanzia madini, Utalii mahoteli na biashara zingine nyingi tu.

Mapendekezo yangu kwako nikiwa ni mtu ambae nimeiona Arusha kuwa ina "potential" kiuchumi, basi keti chini na timu yako panga mikakati ya kuifanya Arusha kwa kituo cha biashara Tanzania yaani "Financial Centre of Tanzania".

Kama nilivyosema hapo juu Arusha ina madini, mbuga za wanyama, mahoteli ya kimataifa, kituo cha biashara cha AICC, uwanja mpya wa mpira waja na biashara zingine nyingi tu ambazo zina uwezo wa kuinyanyua Arusha kiuchumi.

Si tu Arusha yavutia wageni watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani pakini pia yaweza kuvutia zaidi uwekezaji wa ndai ambapo watanzania wenye fedhawaweza kuleta biashara zao Arusha na kuibadilisha kimuenekano. Nimeona yupo mfanyabbiashara mmoja ambae amenunua hoteli ya kitalii na kuamua kuivunja yote.

Hii ni ishara tosha kwamba endapo tunapata wafanyabiashara zaidi wa ndani basi mzungunguko wa fedha mkoani Arusha waweza kupongeza pato la mkoa na pia kusaidia kuongeza na kupanua soko la ajira khasa kwa vijana mkoani humo.

Arusha ni mkoa unotoa madini pekee duniani ya Tanzanite ambayo hutumika kutengeneza vito ghali katika nchi nyingi duniani khasa Antwerp, Singapore, India na Sauri Arabia. Hii pekee yanofanya Arusha kuwa "Exporter" pekee wa madini hayo jambo linoweza kufutanya kuwa na uchumi imara unofanana na wenzetu wa Botswana.

Botswana walitengeneza mazingira mazuri ya kuwezesha madni ya Almasi kutengenezwa nchini humo na bandikuu ya Botswana kusimamia biashara hiyo kwa umakini.

Utalii pia bado waifanya Arusha kuendelea kuwa kivutio kwa raia wa kigeni nchini. Jambo hili laweza kuangaliwa zaidi ili kuongeza idadi ya watalii kila mwaka. Hii yaweza kufanikiwa tu endapo mkuu wa koa utafanikisha kuwa na programs maalum kwa ajili ya kuitangaza Arusha kupitia tovuti za kibalozi huko nje, matangazo katika sehemu mbalimbali,nje na ndani ya nchi na pia kuwa na vituo maalum katika balozi zetu ili kuvutia zaidi watalii.

Mapato yanopatikana katika mkoa wa Arusha kuanzia kodi ya maendeleo na Utalii , madini vina uwezo wa kuuboresha uwanja wa ndege wa KIA ili kuwa na hadhi inofanana na mkoa wa kimataifa. Majengo ya uwanja huo kwa sasa yana paa za mabati ambayo si taswira nzuri kwa mkoa. Hivyo litakuwa ni jambo la kimaendeleo kufikiria kujenga upya uwanja huo kwa kuupanua zaidi na kuujenga kisasa.

Ndugu mkuu wa mkoa, kama huelewi Arusha ni mkoa ambao ni mali yaani financial Asset ya nchi kutokana na hadi yake kimataifa. Kuwepo tu kwa kituo cha biashara cha kimataifa chaifanya Arusha kuwa kivutio na kuleta shauku kwa wawekezaji wa kimataifa.

Hivyo situ kuna kituo AICC lakini pia kuwa mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu na kuna mahakama ya AFCHPR na pia kuna mahakama ya umoja wa mataifa ya ICTR inoshughulikia kseiza mauaji ya kimbari yalotokea Rwanda. Mambo haya yaifanya Arusha kuwa ni kioo cha sheria za nchi na za kimataifa na pia kioo cha sheria za haki za binadamu.

Mazingira mazuri yanoandaliwa na serikali katika sehemu yoyote ile, husababisha kukua kwa ari na mori kwa wananchi kujiletea maendeleo wao wenyewe. Watu wengi duniani bado waishangaa China na kuiangalia kwa jicho la uhasidi kwa namna ambavyo imeweza kuwanyanyua wananchi wa kuipato cha chini kwenda kwenye kipato cha kati.

Hivyo mkuu wa mkoa, huu ni wakati wako wa kuonyesha umahiri wako katika kuhakikisha wapata njia sahihi za kuwanyanyua wananchi wa kipato cha chini wa Arusha na kuwa na uwezo kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ni wakati wa kufanya tathmini ya kutambua ni viwanda vipi vyahitaji kuboreshwa au msaada wa fedha ili kujiimarisha. Tusisahau Arusha iliwahi kuwa na kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre ambacho leo hii ni historia,je ni kwanini tulishindwa kukiimarisha kiwanda hichi?, haya ndo masuali ambayo yataleta majibu na namna ya kuweza kuangalia uwezekanio wa kua na viwanda kama hichi.

Viwanda vidogovidogo "Smallscale industries" navyo ni sehemu ya uchumi wa sehemu yoyote na litakuwa ni jambo la kimaendeleo ikiwa kutatengwa eneo maalum au "Industrial Estate" ambalo litasheheni biashara zote ndogondogo ambazo zatambulika na zote kulipa kodi kulingana na mapato yao.

Mafuriko yanotokea sasa na kuathiri maeneo mengi ni dalili ya miundombinu mibovu au ulokosa kufuatiliwa. Hivyo ujenzi wa miundombinu bora itasaidia kupinguza athari za mafuriko na pia kuwezesha mkoa kuwa na njia safi na salama za magari na watembea kwa miguu.

Bado Arusha ni soko linokuwa yaani (emerging market). Soko linokuwa ni lile soko ambalo lina viashiria vyote vya soko liloendelea lakini halijafikia viwango vinotakiwa. Hivyo ni lazima viashiria hivi viwepo na hapo ndipo Arusha yaweza kuongeza uchumi wake na pia kuvutia aina zingine za uchuni kama ule uchumi wa gig enonomy ambao wahusisha biashara za kuagiza vyakula kupitia mtandao wa internet au simu ya mkononi.

Aina hii ya uchumi wa internet waweza kuwasaidia vijana kujiajiri katika maeneo ya usafirishaji abiria na kusambaza vyakula. Ajira za namna hii zitawafaa wale vijana ambao hawana ajira rasmi lakini ambao wanakuwa wamejiandikisha TRA. Hivyo biashara kama ya Uber na Uber Eat zaweza kuwa ni moto au Hot-cake katika mji.

Hivyo mkuu wa mkoa mimi nimekupa mawazo ambayo nina uhakika yaweza kukutoa katika siasa za malumbano na kutafuta kiki kama ambavyo itaweza kutafsiriwa na mahasidi wako. Kazi ya uongozi ni ngumu lakini kwa nchi hizi zetu za Kiafrika imegundulika kuwa bila msukumo (unofuata sheria) nchi yetu/ zetu haiwezi kuendelea.

Mwisho "but last", ndugu mkuu wa mkoa tafita washauri maalum wa kukusaidia kazi yako mkoani Arusha. Katika video ilowekwa hivi majuzi katika mitandao ya kijamii kuna makosa kadhaa ambayo yahitaji ushauri maalum. Washauri hawa maalumau "special advisors" ni watu maalum wenye uwezo na utaalm wa kushauri viongozi namna ya kujiweka kwenye macho ya umma.

Hawa watashauri namna ya kuandaa hotuba yako na pia watashauri na kutathmini hotuba hiyo hata kama haikuandikwa. Ukumbuke kuwa hotuba au maneno yoyote mara tu yatokapo kinywani hayawezi kurudi nyuma na hii ni kutokana na uhuru wa vyombo vyetu vya habari na kukua kwa teknolojia na uwepo wa mitandao wa internet.

Hivyo hawa washauri maalum ni muhimu sana ingawa wanalipwa na malipo ya kazi yao ni kutokana na utaalam wao wa kushauri.

Mwisho , hongera kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na piga kazi,weka siasa za kiki pembeni, na "make Arusha Great" kiuchumi na financial Center ya nchi ili iweze kuwa mfano kwa mikoa ya Tanzania.
Haya mambo yanatakiwa kuratibiwa na Tume ya Mipango badala ya Hawa ambao Leo wapo kesho hawapo.maa a sio mambo ya overnight au mda mfupi.kutoa majibu.

Wazo ni zuri ila waliotakiwa kuratibu sio RC Bali Tume ya mipango.Mbona Dom Wana Master plan Yao ambavyo wanataka Jiji liwe?
 
Lakini RC si aweza kuwa awasiliana na hiyo tume ya mipango na mwisho kupewa "go ahead" na mawazo yake?

Tume ya mipango yatakiwa kuwa ni kama mwangalizi wa utaratibu mzima wa mipango ya maendeleo ya taifa inohusisha mikoa yote.

Huoni kwamba TIC na Tume ya MIpango yaweza kutumia urasimu kuzuia mawazo ya kimaendeleo ya viongozi.
 
Sio kazi yake,yeye ni Kusimamia utekelezwaji wa sera za Nchi za Uchumi na kijamii kutoka Tume ya Mipango,Wizara na Maelekezo ya Viongozi.

Kimsingi huwezi kuwa unaanzisha vya kwako pamoja,Bali weka ubunifu wako wenye Tija.
 
Sidhani kama kuna mahala katika mada nimesema aanzishe vya kwake.

Bali nimesema aubadilishe mkoa, auendeleze na aufanye kuwa ni mkoa wenye tija zaidi kiuchumi.

Zamani alikuwepo mzee marehemu Lawrence Gama, huyu mzee alikuwa na maono sana kama kiongozi na kila mkoa alokwenda alihakikisha unabadilika.

Mkoa wa Kilimanjaro uliwahi kuongozwa na mzee Gama na akaunyanyua kwa kiasi chake pia hata mkoa wa Ruvuma alikwenda pale na kufanya machache tu mkoa ukawa moja ya "The Big Four".

Unafahamu kwamba miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa ni mikoa iloitwa "the big four"? Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa?

Mikoa hii ilikuwa yailisha nchi lakini leo hii twapewa mchele wenye virutubisho kutoka nje ili tule tuvimbiwe.

Wamkumbuka au umewahi kumsikia marehemu mzee Gama?
 
Hawezi fanya hivyo kama hakuna policy statement au policy guidelines ya kufanya hivyo.
 
Waulizwe Serikali ila policy statement iliyopo Kwa Arusha ni kuwa kitovu Cha Utalii na mikutano na sio financial center kama unavyotaka wewe.
Je, hufahamu kuwa hizo policy huweza kupitiwa mara kwa mara na kufanyiwa mabadiliko?

Hujawahi kusikia watu wasema kuna "change of policy" kuhusu jambo fulani?

Usichoshwe na masuali yangu twaelimishana.
 
Labda kwa ujeuri wake aweza kuendelea kiukaa kimya juu ya hilo na sidhani kama kuna alie na interest ya kufungua kesi ya madai.

Yule anetuhumu si ndie yule aneenda polisi kupeleka tuhumua zake au?

Na polisi si wapo? na watapokea tuhuma hizo na kuzifanyia maana hilo ni jukumu lao.

Tukiendelea kutoa tuhuma tu mitandaoni nafikiri haitasaidia kupata hakai ya kusikilizwa madai hayo na pia haki ya mtuhumiwa kupata nafasi ya jibu tuhuma kwa njia sheria ambayo ni polisi na mahakama.

Mimi hayo ni mapendekezo yangu hayamaanishi kuwa namuunga mkono Mr Makonda kwa kutojibu tuhuma.
Upo sahihi mkuu kulalama kwenye social networks hakusaidii,ni kutumia lugha watakaoisikia hawa watawala
 
Mkuu, Financial centre yabeba financial hub na financial markets.

Mimi sijasoma sana kama weye ila nina knowledge ya kutosha na siwezi kujisifu.

Lakini nina bahati ya kutembea na nimetembea kwelikweli dunia hii.

Nazungumzia Arusha kuwa Financial Centre kutokana na hadhi yake ya kuwa tourist destination ya nchi.

Kwa mfano mji wa Shanghai ni financial center ya China kwa sasa. Mji huu zamani ulikuwa ni kijiji cha uvuvi na mji wenye masoko yaani market town na hiyo ni kwenye kuanzia miaka ya 1900s.

Nikisema financial centre ya Tanzania namaanisha mji wa Arusha kuwa financial centre yaani mambo yote ya fedha, uchumi na biashara, Utalii, viwanda na madini kama nilivyoyaongelea kwenye mada.

Unanipata ndugu?
Nabishana na mtu mwenye kichwa kigumu tu.
 
Waulizwe Serikali ila policy statement iliyopo Kwa Arusha ni kuwa kitovu Cha Utalii na mikutano na sio financial center kama unavyotaka wewe.
Nashukuru mkuu ChoiceVariable umekuja labda huyu atakuelewa. Nami hoja yangu ni hiyo kuwa Arusha can be tourist centre but not financial centre. Ila anakichwa kigumu kuelewa.
 
Back
Top Bottom