Pre GE2025 Mapendekezo ya CHADEMA juu ya Miswada ya Sheria za Uchaguzi ambayo Kamati ya Bunge inazuia yasisomwe Bungeni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nataka unijibu je unaona sahihi na unaunga mkono kwa kila jimbo kuwe na wabunge wawili?
Cdm wanataka sera ya majimbo, unajua mfumo wao utafanya vipi kazi? Au unatumia mapendekezo ya cdm kwa mfumo wa kiccm? Je wakipunguza mishahara na muda wa vikao vya bunge? Jitahidi kutokutumia mtazamo wako kwenye mifumo ya wengine. Kwa taarifa yako watapunguza sana matumizi yasiyo na tija ya serekali.
 
Chadema inastahili pongezi
Tangu zoezi la kukusanya maoni lianze, maoni ya Chadema ndio the most exhaustive na bango kitita lake ndilo bango kitita kubwa kuliko michango yoyote!.

P
Hata hicho kipengele cha 5 cha kila jimbo kuwa na wabunge 2 wa kike na kiume? Unajua idadi ya wabunge itafika hata 700 kama hilo litapita? 300 tu hawa asilimia 90 hakuna wanachofanya sasa kumbe wanataka waongezwe wafike hata 700?
Ama kweli hii nchi kukombolewa ni miaka 100 au 300 ijayo
 
Pendekezo moja kati ya arobaini, umelishikia bango. Wao wameleta solution kwa issue ya viti maalumu. Hatuwezi kuendelea kulipa wabunge wa dezo.
Ni la hovyo.........
Huwezi mtu ukakaa ukawaza kuongeza idadi ya wabunge.
Inashtua kidogo.
 
Haki hata mimi hili limenishangaza sana. Yani wabunge ina maana watafika hata 800. Sijui hili linasaidia vipi mwananchi. Yani eti akiwepo wabunge wa kike na kiume so hoja zitakuwa zikiwasilishwa kijinsia au...
Na hapa unaona watu wanasema maoni safi.

Hii nchi watu wanaleta ushabiki kisiasa tu na ndio maana adui mkubwa wa nchi hii ni ujinga si kitu kingine. Ujinga ni mtaji wa wanasiasa na unawafanya wazidi kutajirika
 
Jibu hoja kulingana na hoja iliyopo mezani kwa sasa. Kinachoendelea na kujadiliwa kwa sasa siyo habari za utawala wa majimbo. Hoja ni juu ya kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo.je unakubaliana na huo ujinga?
 
Hapo kwenye wabunge wawili kwa Jimbo kwa maoni yangu ni Big no, mengine safi.
 
Kwenye mapendekezo hayo Unapata picha gani?
CHADEMA ni walafi tu wa madaraka, hawana nia ya kweli kulikomboa taifa hili kutoka kwenye makucha ya CCM.
Ni another monster in making.
 
Jinga kabisa wewe. Soma uelewe. Viti maalum vya wanawake vinafutwa! Badala yaek wanawake wapigiwe kura....
 
Tuondolee ujuha wako hapa
 
Kwamba Chadema wanataka bungeni kuwe na wabunge wanawake na wanaume kwa kila jimbo?

Kama kweli wamependekeza hivi, wamekosea, tena wamekosea sana, sijajua kama kuna sehemu kwenye mapendekezo yao wameweka namna ya kupunguza mishahara na marupurupu ya wabunge.

Lakini kama hawajagusa hapo, halafu wakataka wawepo wabunge wa jinsia mbili kwa kila jimbo, plus viti maalum, Chadema wamefeli, watu tunazungumzia kupunguza gharama, iweje wao waongeze gharama?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Jibu hoja kulingana na hoja iliyopo mezani kwa sasa. Kinachoendelea na kujadiliwa kwa sasa siyo habari za utawala wa majimbo. Hoja ni juu ya kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo.je unakubaliana na huo ujinga?
Don't be naive, tazama kwenye kichwa Cha Uzi wako pale juu, Kuna popote umesema wabunge wawili Kila Jimbo, au umejitia hasira na mapendekezo ya cdm na hoja za kuokoteza?
 
Point.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…