Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bado kichwa kinautoto tu kujiapiza kulipa kisasi ndio utoto wenyewe, piga chini maisha mengine yasonge.kama ni Malaya kibaoooo wapo kojoa, kuwa mwepesi sepa. Japo dhambi zipo pia.Nimegundua kwa mara ya pili mapenzi ni upumbavu na upuuzi tu, yalishanikuta mara ya kwanza nikapuuzia na hii mara ya pili nathibitisha ni upuuzi tu!
Baada ya siku kadhaa kuwakejeleli watu hapa JF waliokuwa wakilialia kipuuzi kuhusu mapenzi na mimi yamenikuta aisee!
Unampenda mtu na kumjali na kumfanya mtu muhimu halafu anakuja kukugeuka kipuuzi! Muhimu ni kwamba nilishajiwekea kutomuamini 100% mwanamke na hii imesaidia kidogo. Ila nimeumia sana.
Kuna mwanamke nilipanga kumuoa na tulipanga naye mambo mengi tu, tulipanga mwakani nifanye kweli kumuoa ila kumbe kuna mwenzangu sasa kapeleka posa na mwanamke kakubali kuolewa!
Sasa najiuliza kule kumjali kote na kujifanya kunionesha ananipenda kupitiliza yale yote yalikua maigizo? Mpaka muda huu nashindwa kumtafakari huyu binti maana kanipotezea muda aisee.
Leo nasema kamwe sioi, sioi, sioi kamwe! Naanza kulipa kisasi sasa, nitawadanganya, kuwachezea na kuwapotezea na ninyi muda ili kulipa hiki kisasi. Nasema kataa ndoa, kataa ndoa!