Mapenzi ni upuuzi

Mapenzi ni upuuzi

Nimegundua kwa mara ya pili mapenzi ni upumbavu na upuuzi tu, yalishanikuta mara ya kwanza nikapuuzia na hii mara ya pili nathibitisha ni upuuzi tu!

Baada ya siku kadhaa kuwakejeleli watu hapa JF waliokuwa wakilialia kipuuzi kuhusu mapenzi na mimi yamenikuta aisee!

Unampenda mtu na kumjali na kumfanya mtu muhimu halafu anakuja kukugeuka kipuuzi! Muhimu ni kwamba nilishajiwekea kutomuamini 100% mwanamke na hii imesaidia kidogo. Ila nimeumia sana.

Kuna mwanamke nilipanga kumuoa na tulipanga naye mambo mengi tu, tulipanga mwakani nifanye kweli kumuoa ila kumbe kuna mwenzangu sasa kapeleka posa na mwanamke kakubali kuolewa!

Sasa najiuliza kule kumjali kote na kujifanya kunionesha ananipenda kupitiliza yale yote yalikua maigizo? Mpaka muda huu nashindwa kumtafakari huyu binti maana kanipotezea muda aisee.

Leo nasema kamwe sioi, sioi, sioi kamwe! Naanza kulipa kisasi sasa, nitawadanganya, kuwachezea na kuwapotezea na ninyi muda ili kulipa hiki kisasi. Nasema kataa ndoa, kataa ndoa!
Bado kichwa kinautoto tu kujiapiza kulipa kisasi ndio utoto wenyewe, piga chini maisha mengine yasonge.kama ni Malaya kibaoooo wapo kojoa, kuwa mwepesi sepa. Japo dhambi zipo pia.
 
Mapenzi yanaumiza kila mtu, ni asili ya binadamu kuumia kihisia.

Ukitaka yasikuumize njia ni moja tu-usipende.

Ukitaka kuepuka kupenda njia ni moja tu-kufa.

Ukitaka kufa njia ni moja tu-penda.
 
H

Hukuwa makini pengine dalili zote zlikuwa nazo wewe ukang'ang'ania. Sasa angefanyaje.
Hao wa kuwadanganya huwapi ng'oo wameshajanjaruka.
Hakukua na dalili yoyte mkuu
 
Back
Top Bottom