Mapenzi niue: Yule Jennifer aliyekula nauli ya Emmanuel, ahukumiwa Miaka 7 Jela

Mapenzi niue: Yule Jennifer aliyekula nauli ya Emmanuel, ahukumiwa Miaka 7 Jela

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Mwanamke mmoja wa Nigeria anayeenda kwa jina la Jennifer, amehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au kulipa kiasi cha 420,000 pesa za Nigeria kwa kosa la kula nauli ya mwanaume Emmanuel 30,000 ambayo alitumiwa kisha hakwenda eneoo la tukio kuonana na mwanamume huyo.

Jen haamini macho yake 🤣
IMG-20250827-WA0043.jpg

Mwanamke huyo alishtakiwa na mwanaume ambae alituma nauli hiyo kwa kusema alimtumia nauli mwanamke huyo lakini baada ya kutuma nauli mwanamke huyo hakuweza kwenda. Mbaya zaidi akawa hapokei simu

Mahakama imemkuta na hatia mwanamke huyo na kumfunga miaka 7 jela aidha amlipe Emmanuel N420,000

Kuna Mpemba fulani nataka nimpeleke Kisutu. Dharau zimezidi
 
..kwa kosa la kula nauli ya mwanaume Emmanuel 30,000 ambayo alitumiwa kisha hakwenda eneoo la tukio kuonana na mwanamume huyo.
Dah,
Hiyo ni kama sh 49k za Tanzania ndo zinamtokea puani, miaka 7 au mzigo wa faini.

Angembembeleza mwamba aitandike daily kwa mwezi mzima yaishe
 
Jamani ila huyu dada jasiri sana 🤣🤣🤣🤣 nisingekubali nipelekwe mahakamani tungeyamaliza nje ya mahakama.
Nisiulizwe ningeyamaliza vipi 🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣 Naomba tuyamalize wote muda huu
 
Back
Top Bottom