Pole, sana mkuu kwa hayo yote, R.I P R hakika jamaa alikuwa na mapenzi ya kweli sana kwako. Wanaume wachache sana Wa Sikh hizi wenye mapenzi ya kweli namna hiyo. Kweli kizuri hakidumu.
Lakin badae ulikuja kujua R alifariki kwa ugonjwa gan, malaria tu? Au. Mungu ambariki mwanao azidi kuwa na akili nzuri
Nimejikuta nalia eti daaa, kwa kua umeniuliza acha tu nikujibu.
Kifupi mpaka leo sijui alifariki kwa ugonjwa gani, baada ya mimi kurudi shule ndugu nasikia walienda kwa mganga, maana ziliibuka imani za kishirikina kwa upande wa wao. (Alinambia rafiki wa marehemu)
Mganga akawambiwa ametolewa kafara na mtu aliekuwa anapendana sana na marehemu. Ambaye alikuwa anashirikian kila kitu na marehemu kifupi marehemu alikuwa anamapenzi makubwa na huyo mtu na alikuwa akimuamini sana.
Ndugu wa marehemu wakafikiria ni nani wakasema mtu aliekuwa akipendwa sana na marehemu ni mama A ambaye ni mimi sasa.
Hivyo wakasena basi nitakua nimemuua ili mimi nichukue akili zake ati nisome. Kumbuka niko shule na sijui kinachoendelea.
Kumbe mganga akawaambia kuwa mganga nilieenda ana nguvu sana na hawezi kurudi hata wafanye nini wakijaribu chochote wataisha ila wanaweza lipa kisasi kwa kuniua na mimi.
Nasikia walifanya mambo yao nife ila Mungu mkubwa sikujua wala kuumwa hata mafua mpaka namaliza masomo.
Rafiki wa R alikuwa akiulizwa baadhi ya vitu maana yeye alikiwa karibu sana na sisi na akalazimika kushirikishwa kila kitu ila yeye hakuafiki hilo hata kidogo maana mimi alikuwa akijua vyema siwezi fanya hivyo hata iweje.
Nilipomaliza masomo nilirudi na kwenda kuwaona wakwe zangu ila hawakunipokea vyema niliwasalimia wakaitika tu kisha wakaingia ndani na kuniacha nje kama masaa 2 nikabeba mwanangu nikaondoka. Ndio kuja kupewa mkanda mzima na rafiki wa marehemu baada ya kukutana nae.
Tangu hapo sijawahi kwenda wala wao kuja na mama alishahama pale so hata hawajui mtoto alipo wala mimi nilipo.
Kifupi ni hivyo sijui ugonjwa uliomuua.