Iyo nilishaifanya zaman sana kabla ata sijaoa,
ILIKUA HIVI,[emoji116]
Nilikua bachela afu mpnz wang yuko mbali na tunakoishi, mimi KIMARA mwisho, yeye MBAGALA.
Nikimwambia awe anakuja kwangu kila wikend tuna DO basi chenga chenga znakua nyingi Yaani ni mpaka ajiskie yeye.
Sometimes kwa mwez anakuja mara moja.
Yaani kwa kifupi SHE WAS NOT SERIOUS WITH THAT RELATIONSHIP.
Nikaona isiwe tabu,
ANANICHUKULIA POA HUYU binti afu na mimi ndo nishampenda, anajihisi yuko peke ake.
Inabidi nimpe changamoto kidogo apate wivi nione itakuaje.
PLAN ILKUA HIVI,
Ule ule mtaa nnakoishi, nyumba jiran kuna shoga ake wa kufa na kuzikana (WALISOMA WOTE primary mpaka Advance shule moja)
Basi kuna COUPLE MOJA mtu na dem wae huwa wanakuja pamoja na kuondoka pamoj kazin kwangu kwa gar ya Rav 4 2006.
Nikawashirikisha plan yangu na wakakubali kutoa ushirikiano 100%.
Nikamwomba mshkaj wang kwa wiki 1 nzima tu awe ananipa lift kwny gari yake nnapoenda na nnapotoka kazin.
Ila shemej awe ndie anaendesha, mimi nakaa siti ya mbele na shemeji.
afu yeye awe anakaa siti ya nyuma kwenye tinted asionekane
Akakubal kwa wiki nzima wakawa wananipitia asbh, wakifika shemej anapak.
Anashuka anakuja kunigongea mlangon kwangu nafungua tunaongozana mpk kwny gari tunaondoka kwenda kazin.
Jion wananirudisha, wakifika gari inapak nashuka.
Shemej anafanya kama ananisindikiza kwa mguu mpk mlangon kisha anarud anawasha gar na kuondoka.
Sometimes, tunaplan jamaa abaki ndaninya gari, meji atoke ndani ya gari.
1. Tunashuka tunaegemea bonet ya gari kama vile tunaongea vitu flan flan, mara acheke,mara anishike shavu, mara kaniwekea mkono begani na kufurahi furahi kisha anapanda gar anaondoka.
2. Anaingia ndani kwangu kidogo kunywa maji baridi na stori mbil tatu, dakika 10 au 15 kisha anarud zake anawasha gar anaondoka zake.
Basi yule shoga ake akawa anaona maana mda wa jion alkua anapikia nje ya nyumba, na mimi najifanya sina habari kabisa niko bize na mambo yangu.
Aisee,
Taarifa zilimfikia mpnz wang kua kuna mwanamke huwa ananipitia asbh kisha ananishusha jion kwny RAV 4 ya silver kila nnapotoka kazin.
Siku moja narudishwa kumbe kaja bila kunitaarifu yuko kwa uyo shoga ake.
Nmeshushwa na gari imeondoka namuona uyu apa.
Anauliza
" Uyo aliekushusha ni nani"
Nkamjibu tu shortly,
"Haikuhusu"
Akauliza tena,
"Ndo majibu gani ayo sasa, sio mara ya kwanza wala ya pili najua anakuleta na kukufata hapa kila siku"
"Kama hunipendi bora useme, Yaani uyo ndio anakufanya siku hizi ata hunipigii sim kama zaman"
Nikamjibu,
"Wee Utajua mwenyewe bhana" uku naelekea ndani.
Akajibu,
"Najua tu hunipendi na unanijibu ivyo kwa sababu umepata mwanamke mwenye gari. Wee sawa tu"
Nkamjibu,
"Utajua mwenyewe bhana"
Nikamwambia tena,
"Aisee usniongeleshe sana bhana nmechoka sana nataka nipumzike, Nauli yako hii apa wee nenda tutaongea siku nyingine" akaondoka.
Aisee baada ya hapo, Akaenda zake kwao
Akaanza kunipigia mara kwa mara,
Uko wapi?
uko na nani?
Kesho nakuja.
Ikabid nimstopishe meji wangu, Maana LENGO tayar LISHATIMIA
Gafla nikaona ruti za kuja kuja kwangu na kukaa kwangu zimeongezeka,
MAHUSIANO AKAANZA kuyachukulia serious zaidi.
Akawa anakuja ananifulia, ananipikia mpk sometimes anaacha baadhi ya nguo zake kwangu,
Sometimes anakuja usiku wa manane ananigongea namfungulia, anaangalia uku na kule nisije nikawa niko na mwanamke mwingine.
Nikajisemea kimoyo moyo,
" NAAM , Hapa ndo nlipokua napataka[emoji4]. Amekua serious na mahusiano sasa [emoji106]"