Mapigano kati ya Israel na Palestina yalianza tangu enzi za vita kati ya Mfalme Daud Muisrael na Goliati Mfilisti (Mpalestina)

Ugomvi ulianzia tumboni mwa mama yao
 
Sasa unaposema Waisrael sio Wakaanani unamaani nini hapo?
 
Sasa unaposema Waisrael sio Wakaanani unamaani nini hapo?
Kuna kabila la Ngoni kutoka S.A walikuja Tanzania wakachanganyika na jamii ya Watanzania je, tutasema Watanzania ni Wasouth?

Au wale watumwa kutoka Afrika magharibi wakauzwa South America (Latin America) kama Brazil n.k wakachanganyika na jamii za kule je, tutahalalisha kuwa wale Afro-Latinos wa Latin America ni Waafrika?
 
Ukitaka kuelezea hii historia anzia kwa baba wa Imani, Ibrahim. Kwamba baada ya Sara kupata mtoto wake wa kiume Isaka ilimlazimu Hajir aliyekuwa kijakazi wa Kimisri (Mwarabu) aliyezaa na Ibrahim afurushwe na Mwanae Ishumael. Wakati huo Ibrahim alikaa maeneo ambayo kwa leo ni Iraqi, na huyu Ishumael ndiye chimbuko la Wapalestina wa leo wakati Isaka ndiye chimbuko la Waisrael wa leo kupitia kwa Mwanae Yakobo (Israeli mwenyewe) aliyewazaa akina Yusufu na nduguze 11.

Hivyo kusimulia hii historia kwa mlengo wa kiimani utaona hivi vita ni vya wanandugu wa baba mmoja yaani Ibrahim, lakini mama tofauti. Vita wakati wa Daud na Goriat ulikuwa ni mwendelezo wa uhasama uliokuwa umehasisiwa toka kuzaliwa kwa hawa wanandugu. Waisrael kukaa Kaanan na baadae kutawanyika na kurudi tena hakukuanzia na kukomea kwa Musa tu, hata hii ya kurudi kwao miaka ya 1948 baada ya kufurushwa na Hitler ilikuwa ni muendelezo wa kile kilichoanza enzi za Musa kuwatoa utumwani Misri.
 
Ni kweli Ishamaeli mtoto wa mjakazi wa kimisri ambaye alikuwa mchepuko wa Ibrahim ndiye aliyezaa na Ibrahimu ndio uzao wa Waarabu na Waisrael ni uzao wa Mtoto wa ndoa wa Ibrahim toka kwa Sarah mkewe wa ndoa

Sasa Wapalestina wamatokana na ukoo wa nabii Nuhu ambaye alikuwa na watoto wawilili mmoja shem ambaye ndio climb uko la Wayahudi na mwingine akiitwa Hamu ndio chimbuko la Wapalestina na Waswahilii

Kula chuma hicho
 
Sawa kabisa Boi Manda, lakini huyo kijakazi hakuwa mchepuko bali Ibrahim alishauriwa na mkewe wa ndoa yaani Sarah, ajishindie huyo kijakazi ili apate walau mtoto atakae kuja kuwa mrithi wa mali za Ibrahim. Basi bwana, baada ya huyo kijakazi kumzalia Ibrahim huyo mtoto wa kiume, kijakazi akakunjua makucha na kuanza kumdharau Sarah ambae kwa muda mrefu wa ndoa alikuwa ajabahatika kupata mtoto.

Mara tu baada ya Sarah kumpata mtoto Isaka ktk umri wa uzee nae kalianzisha huku akimsii mzee Ibrahim amshughulikie huyo kijakazi na kitoto chake. Ndiyo ukawa mwanzo wa kuwafukuza kijakazi na mtoto wake waende wasikokujuwa.

Ni uzao huu huu wa Ishimael mtoto wa kijakazi, mtume Mohamed alikuja kuzaliwa baada ya vizazi vingi, na vilevile ni uzao ule ule wa Isaka mtoto wa Sarah ambao baadae Yesu alikuja kuzaliwa baada ya vizazi vingi.

Hivyo utaona kwa msingi wa historia ya kiimani, uhasama wa hawa watu ni wa vizazi na vizazi kuanzia kwa mama zao.

Lakini je, kwa ulimwengu tulio nao sasa hivi, mauwaji yanayoendelea huko Gaza ni ya kuacha yaendelee bila kukemewa na jumuyia ya kimataifa? Hapana, stop war in Gaza, stop killing the innocent.
 
Waisrael na Wapalestine wenyewe wanasemaje kuhusu huo mgogoro wao na sababu zake.

Maana wayahudi wenyewe hawaukubaki ukristo wala uislam lakini humu jukwaani sababu ya uhasama inanasibishwa na ukristo na uislam.

Wao humezesha vitu gani vizazi vyao? Huwapa sababu gani watoto wao za kupigana na kuwachukia wenzao
 
Mgogoro huu inategea unauangalia kwa jicho gani. Ukiuweka kwa kuangalia haki za kibinadamu kinachofanywa na Israeli ni kitu kibaya sana thidi ya ubinadamu, lakini je kilichofanywa na Hamas kwa Waisrael
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Code:
Baadaye WAKANAANI wakaenda kuishi hapo kabla ya ahadi ya Mungu kutimia.
Siyo kweli kwa sababu,

Mwanzo 15,
17 Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
18 Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

Makabila hayo 10 yote yalikuwepo eneo hilo kabla ya Ibrahim kupewa.
 
Hivi huwa mnazingatia kitu gani kusema waisrael siyo waarabu?.

Ebu nisaidie kunielewesha kwa kuzingalia ramani hizi,
 
Waliokuwa wanaugomvi tangu kwenye tumbo la mama yao ni Esau na Yakobo baadaye huko mbele ya safari ndio kinakuja kuzaliwa kizazi cha nabii Rutu ndio kinatokea kizazi cha Waisrael na Palestina
Luti na Ibrahim waliishi pamoja mpaka pale walipoanza kugombania maeneo ya malisho na ndipo Ibrahim alimuacha Luti katika bonde lote la Jordan na yeye Ibrahim akaelekea upande ambao ni kati ya mto Nile na mto Efrat.
Mwanzo 13,


5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.
6 Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.
7 Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.
8 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.
9 Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.
10 Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao.
12 Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma.
 
Kuna uhusiano kati ya Uyaudi, Ukristo na Uislamu, chimbuko la hizi dini ni moja japo kila upande unaamini uko sahihi kuliko upande mwingine. Kabla ya kuzaliwa Yesu kulikuwa hakuna ukristo na kabla ya kuzaliwa Mohamed kulikuwa hakuna Uislamu lakini Uyaudi ulikuwepo.

Uyaudi ulichagizwa na ahadi za Mungu kwa Ibrahim na uliendelea hata pale Waisrael walipokuwa Misri hadi kurudi kwao Kaanan. Yesu alipozaliwa aliukuta Uyaudi, na Wayaudi wenyewe hawakumuamini hivyo walibaki na dini yao, japo hata Yesu mwenyewe alikuwa Myaudi kwa asili. Misingi inayojenga ukristo ni ileile iliyojenga uyaudi tofauti ni kwamba Uyaudi unaamini ktk Torati tu.

Uislamu ulikuja miaka zaidi 500 baada ya ukristo. Sitaki kuongelea sana maana wao ktk mafundisho yao wanadai hata Ibrahim mwenyewe alikuwa Muislam!!! Ninachojuwa ni kwamba Ibrahim baada ya kupata ahadi toka kwa Mungu alikuja kuzaa watoto wawili kwa mama tofauti. Mama wa kwanza Muyaudi Mwenzie alimzaa Isaka na mama wa pili kijakazi wa Kiarabu alimzaa Ishimael. Ni katika uzao huo zilikuja kutokea hizi dini. Yaani ktk uzao wa Isaka kulikuja kutokea Uyaudi na baadae Ukristo, na ktk uzao wa Ishimael kulikuja kutokea Uislamu.

Kisa cha ugomvi kati ya Waisrael na Wapalestina ni hadithi ndefu, ambayo kama ni kwa kufuatilia maandiko ya vitabu vya dini, ina chimbuko kuanzia kwa mama yake Ishimael na mama yake Isaka pamoja na watoto wao. Sababu utofautiana tu kulingana na kizazi lakini uhasama ni wa tangu jadi.
 
Aisee umenitoa tongotongo.

Kwa maana hiyo kila kizazi kina sababu zake as kwanini wanapigana sivyo??

Kwa hivyo sababu za vita ya 1960's, 70's na miaka hiyo kabla ya 2000 inaweza kua sio sababu inayofanya wachapane zaidi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…