Mapigo 10 ya Mungu kwenye siasa za Tanzania. Mungu akamwambia Farao bado pigo moja

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku.

BWANA akasema, usiku wa manane nitapita katikati ya nchi ya Misri; na wazaliwa wa kwanza wote watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi wake.

Mapigo anayopata mfululizo ni mpango wa Mungu kumkumbusha kuwa Lipo pigo moja Bado litakalofanya Farao awaachie wana wa Israeli (Watanganyika/Katiba) waende zao.

Sawa ana nguvu kama za Farao, ana majeshi kama ya Farao, ana magereza, ana kila kitu, lakini Bwana wa majeshi atasimama na walio wanyonge.

Mwachieni Lissu aende zake.
 
... kwa muktadha wa andiko hilo, wana Israel kwa kizazi hiki ni akina nani?

Ikumbukwe adhabu ya kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa kwa nyumba zote za wamisri. Je, similar adhabu itakuwa ni kwa watanzania wote? Tumemkosea nini Mungu hata tusioshiriki karamu za "Farao" tuadhibiwe?
 
Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi BWANA anavyowatenga Wamisri na Waisraeli.
 
Ndio hapo sasa ufafanue wamisri ni akina nani na waisrael ni nani ili kila mmoja ajue yuko kundi gani ili (waisrael) wanyamaze kimya maana Bwana ndiye mtetezi wao.
 
... kwa muktadha wa andiko hilo, wana Israel kwa kizazi hiki ni akina nani?

Ikumbukwe adhabu ya kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa kwa nyumba zote za wamisri. Je, similar adhabu itakuwa ni kwa watanzania wote? Tumemkosea nini Mungu hata tusioshiriki karamu za "Farao" tuadhibiwe?
Jikumbishe zaidi.Waisraeli,mbali ya Wamisri,waliambiwa wafanye nini ili malaika mtwaa roho akifika aione tofauti!
 
BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku.

BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

BWANA akasema, usiku wa manane nitapita katikati ya nchi ya Misri; na wazaliwa wa kwanza wote watakufa, tangu yule
Maiti haifai kuaga
 
Huyo kwa picha ni nani?🤔

IMG_20261001_090933.jpg
 
Back
Top Bottom