Ni bila ridhaa ya wageni wakaazi, na sio wananchi.
P.
Tuwekee link.Ni lazima wakimbie kwa sababu ,Ilikua ni kutumikia jela,Ama kuolewa kwa lazima(warabu wa kik) ,Adhabu ilio kali hidhran na pili pili juu.Fuatilia youtube mahojiano sheikh muhamad barwan
Kuelekea kumbukumbu ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Wanabodi,
Nafuatia makala maalum kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, zinazorushwa mfululizo na Idhaa ya KIswahili ya BBC kila siku kuanzia 1:00-1:30.
Katika kipindi cha leo, Mmoja wa askari aliyekuwa zamu ikulu ya Sultani, kwa jina maarufu la Mzee Sukari, anasimulia first hand information kuhusu mapinduzi hayo! akihojiwa na Baruan Muhuza wa BBC. Amekiri kuwa Sultani hakufukuzwa Zanzibar, alikuwa akitafutwa hivyo alitoroka mwenyewe!, na baada ya Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, waarabu hawakufukuzwa Zanzibar, bali walijiondokea wenyewe!.
Kesho kutafanyika mjadala maalum kuhusu Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar utakaoanza saa 12:45-1:30.
Baada ya mapinduzi Zanzibar - BBC Swahili - BBC.com
Zanzibar na miaka 51 ya Mapinduzi - BBC Swahili
Siku ya kilele, kutatolewa nishani maalum za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, sijui kama yule shujaa halisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Field Marshal John Okello, atakumbukwa!.
Paskali
Kuelekea kumbukumbu ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
hao hao wachache wange zaana lakini walichofanyiwa Mungu anajua.waliopelekwa arabuni watakua wachache sana maana huko ni jangwa wangepelekwa kufanya nini wakati hakuna mashamba?
Natuma salamu za pongezi ya miaka 54 ya Mapinduzi, matukufu ya Zanzibar kwa Wanzibari wote, Wazanzibara na Wapemba, japo hawakushiriki Mapinduzi.Pasco,
Kumbe hivi ndivyo unavyofanya research au ndio umepanga na kina Salim Kikeke muyatkufushe hayo Mauwaji thru BBC na. wewe ndie field corespondent mpaka 13/1/2014. Teh teh. Poor Pasco
Maadam hili lilisemwa tuu lakini halikutekelezwa, na sasa waarabu wanang'ara sio Zanzibar tuu, bali hadi huku kwetu bara, kwa hili tuu la Mwarabu kung'ara, nalo halistahili shukrani?, tena sio tuu anang'ara, bali hadi kutaka kurejeshewa Zanzibar kwa kipande cha karatasi!, huu ni Wema ulioje?.Moja katika hotuba za karume alisema tutawamaliza waarabu wote mpaka akitokea mwarabu basi awe tunu na watu waseme ...mwaraaaaaaabu yuuuuuuuuuule
Yaan awe tunu kama dawa.
Lakini Mungu mkubwa akaondoka yeye warabu wanangara znz
Tuwekee link.
P
[The 1964 Zanzibar Massacre Arabs mass murdered by blacks by wlidha111 - Dailymotion] is good,have a look at it!
Natuma salamu za pongezi ya miaka 54 ya Mapinduzi, matukufu ya Zanzibar kwa Wanzibari wote, Wazanzibara na Wapemba, japo hawakushiriki Mapinduzi.
Mapinduzi Daima.
P
Sultan Seyyid Said amekuja Zanzibar mwaka 1832, naamini unakijua fika alichowafanya watu aliowakuta Zanzibar kwa miaka yote zaidi ya 130, na hakuna yoyote aliyehadithiwa kilichotokea na aliyeandika kilichokuwa kinatokea, hivyo hakuna anayesikitika!, labda nikukumbushe tuu kidogoUtukufu wa mapinduzi ni kitu gani???
Kuvamiwa Zanzibar na jeshi la Nyerere likisaidiwa na baadhi ya vibaraka wapenda madaraka kutoka ASP na Umma Party ???
Kuuliwa watu bila makosa na kunajisiwa wasichana na wake za watu??
kukamatwa kwa waziri mkuu Muhammed Shamte pamoja na baraza lake la mawaziri na kupelekwa magereza ya Tanganyika na kufungwa kwa zaidi ya miaka 10 bila kufikishwa mahakamani ??
Kuwekwa kwa Muhammed Shamte magereza ya Nyerere hata kabla huo uitwao muungano haujafikiwa ???
Kuendelea kuwanyima watu wa Zanzibar haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka ???
Kuweka vikosi vya jeshi na usalama kila mtaa ???
Kuingiza madawa ya kulevya , malaya na kila aina ya uchafu ???
kuwaweka masheikh ndani ya magereza ya Tanganyika na kuwabqambikizia kesi za ugaidi kwa kutumia haki yao ya katiba kupinga muungano ???
Sultan Seyyid Said amekuja Zanzibar mwaka 1832, naamini unakijua fika alichowafanya watu aliowakuta Zanzibar kwa miaka yote zaidi ya 130, na hakuna yoyote aliyehadithiwa kilichotokea na aliyeandika kilichokuwa kinatokea, hivyo hakuna anayesikitika!, labda nikukumbushe tuu kidogo
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa, -hasiwa, -bakwa, na kuuawa kinyama!
Lakini kwa kilichotokea ile 1964, kwa vile mmehadithiwa, na wengi wengi mmeathirika ndio maana mnasikitika mnaponisoma, kitu pekee ninachoweza kusema ni poleni sana!.
Na ili kuukata mzizi wa fitna kama Mapinduzi yale yalikuwa matukufu au mauaji, ifanywe research kupima pros na cons za mapinduzi yale, pros zikizidi, then ni haki na halali kuyaita Mapinduzi Matukufu, na cons zikizidi, then tuyaite mauaji ya Zanzibar ya mwaka 1964, lakini katika mapinduzi yote ya umagwaji damu yanapotokea popote duniani, siku zote huwa kuna casualities na heroes, ukiandika chochote kwa kuwatumia wahanga wa casualties tegemea machungu, na kuyaita mauaji ya kimbari, mauaji ya halaiki etc, lakini ukiandika kuhusu the heroes, tegemea watasifu utukufu wa mapinduzi hayo na kuyaita Mapinduzi Matukufu na vibwagizo vya Mapinduzi Daima!.
Mimi bado nasisitiza Zanzibar wanahitaji the truth and reconciliation commission kuponya makovu ya Mapinduzi.
Pole tena.
Paskali