Sultan Seyyid Said amekuja Zanzibar mwaka 1832, naamini unakijua fika alichowafanya watu aliowakuta Zanzibar kwa miaka yote zaidi ya 130, na hakuna yoyote aliyehadithiwa kilichotokea na aliyeandika kilichokuwa kinatokea, hivyo hakuna anayesikitika!, labda nikukumbushe tuu kidogo
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa, -hasiwa, -bakwa, na kuuawa kinyama!
Lakini kwa kilichotokea ile 1964, kwa vile mmehadithiwa, na wengi wengi mmeathirika ndio maana mnasikitika mnaponisoma, kitu pekee ninachoweza kusema ni poleni sana!.
Na ili kuukata mzizi wa fitna kama Mapinduzi yale yalikuwa matukufu au mauaji, ifanywe research kupima pros na cons za mapinduzi yale, pros zikizidi, then ni haki na halali kuyaita Mapinduzi Matukufu, na cons zikizidi, then tuyaite mauaji ya Zanzibar ya mwaka 1964, lakini katika mapinduzi yote ya umagwaji damu yanapotokea popote duniani, siku zote huwa kuna casualities na heroes, ukiandika chochote kwa kuwatumia wahanga wa casualties tegemea machungu, na kuyaita mauaji ya kimbari, mauaji ya halaiki etc, lakini ukiandika kuhusu the heroes, tegemea watasifu utukufu wa mapinduzi hayo na kuyaita Mapinduzi Matukufu na vibwagizo vya Mapinduzi Daima!.
Mimi bado nasisitiza Zanzibar wanahitaji the truth and reconciliation commission kuponya makovu ya Mapinduzi.
Pole tena.
Paskali