Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Mag3

Hakuna mtu yoyote anayemshambulia Pasco watu wanahoji hayo Mapinduzi anayoyaita matakatifu, wewe huu upupuu ulioleta ndiyo historia ya mapinduzi?
 
Last edited by a moderator:
Hivi wale watumwa wengi waliochukuliwa uarabuni waliishia wepi.ningefurahi kuona ndugu wetu hao kama ilivyo kwa waliotoka afrika magharibi wanavyoonekana marekani

Aidia,
Hivi unafikiri watu weusi walioko huko USA na Arabuni are proud to be Africanised, kama unataka kugombana nao muulize wewe asili yako wapi Africa, utajuta kuwauliza!!
 
Ha ha ha watetezi wa waarabu wakishindwa wanakimbilia malumbano ya dini
 
Pasco,

Kumbe hivi ndivyo unavyofanya research au ndio umepanga na kina Salim Kikeke muyatkufushe hayo Mauwaji thru BBC na. wewe ndie field corespondent mpaka 13/1/2014. Teh teh. Poor Pasco
Mkuu rizimu ya kahawa, Kahawarizimu, yalipotokea Mapinduzi ya Zanzibar, mimi sikuwepo, nilipopata akili kuhusu haya Mapinduzi, nimekuta yakiitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na slogan ni "Mapinduzi Daima!", hiyo aliyeyatukufusha sio mimi wala Kikeke, bali wale waliofaidika na mapindizu hayo!.

Niliuliza toka mwanzo Mwarabu alipotokazake Omani na kuitwaa Zanzibar, aliwakuta wenyewe?, wenye Zanzibar yao?!, alivipataje hivyo visiwa hadi kuvifanya vyake?, aliviokota tuu kama sadakalawe?, kwa taarifa tuu haswa kwenu msiojua, Mapinguzi ya Zanzibar yalifanywa na wenye Zanzibar yao!, wakampindua mvamizi Mwarabu!, na wengi walidhani Waarabu walitimuliwa!, la hasha, hawakutimuliwa, bali walijitimkia wenyewe, ama kurudi kwao ama kukimbilia uhamishoni!.

Wanaoyaita Mapinduzi yale Matukufu kuwa ni mauaji ya kimbari, ni waliopinduliwa na vizalia vyao!, kama vipi, bora kila mtu arejee kwao kwenye asili yake, muwaachie Zanzibar, wenyewe halisi wenye Zanzibar yao!.

Mtu aje atoke anakokujua, avamie visiwa, avitwae na kuvifanya vyake, atimuliwe, kisha alalamike!.
Mapinduzi Daima!.
Pasco
 
Wa arabuni ni pamoja sultan qaboos mwenyewe.mama ake mswahili

1. Mamako akiwa mswahili babako Muarabu unakuwa muafrika au?
2. swali lilikuwa wawapi waafrika waliopelekwa arabuni, mwenzio akatuonyesha wazanzibari wakristo! Bado nauliza vile vile Augustino ramadhani katokea arabuni ipi?
 
Hao wazanzibari mnao waongelea mbona hata Tanganyika wanaikana? Muungano hawautaki na wakijitenga wanarudi kwa warabu. Wanamtukana Nyerere waziwazi kwa kusema mchonga meno ndio amewarudisha nyuma.
 
Huu mjadala niligombana nao sana humu mkuu, fikiria jina tu lenyewe zanzibar origin yake ni zenj-bar yaani nchi ya watu weusi, ndivyo waarabu walivyoiita zanzibar walivyokuja. Leo mtu anatoka mapovu kuwa muarabu ni native wa zanzibar!
 
Mkuu Pasco nimekupa ushauri tumia lugha ya stara kwenye huu mnakasha watu wapate kujifunza kitu lugha za kejeli dhiaka wote tunazifahamu usilazimishe tufike huko, siyo mbaya kama utataka hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Huu mjadala niligombana nao sana humu mkuu, fikiria jina tu lenyewe zanzibar origin yake ni zenj-bar yaani nchi ya watu weusi, ndivyo waarabu walivyoiita zanzibar walivyokuja. Leo mtu anatoka mapovu kuwa muarabu ni native wa zanzibar!
Kwani hao native ni kina nani?
 
Huu mjadala niligombana nao sana humu mkuu, fikiria jina tu lenyewe zanzibar origin yake ni zenj-bar yaani nchi ya watu weusi, ndivyo waarabu walivyoiita zanzibar walivyokuja. Leo mtu anatoka mapovu kuwa muarabu ni native wa zanzibar!
Mkuu, umeipata wapi hiyo Zenj-bar?
 
1. Mamako akiwa mswahili babako Muarabu unakuwa muafrika au?
2. swali lilikuwa wawapi waafrika waliopelekwa arabuni, mwenzio akatuonyesha wazanzibari wakristo! Bado nauliza vile vile Augustino ramadhani katokea arabuni ipi?
Nipe darsa kidogo sifa za kuwa mwafrika ni zipi?
 
John okelo huyu jamaa ni mkenya aliyetumwa na serikali tatu za afrika mashariki ili zanzibar isije kuwa nchi ndio ukaona muda mchache tu baada ya mapinduzi muungano ukafanyika hii ni hali ya kuifanya zanzibbar iwe koloni la tanganyika hakuna mapinduzi ya halali bali ni ktk hali ya unyanyasaji wa kiitikadi
 
Mkuu, umeipata wapi hiyo Zenj-bar?

Hiyo ni common knowlege (labda useme spelling za kiarabu nimekosea), lakini mantiki ipo pale pale. Au labda wewe una maana tofauti au historia tofauti ya neno zanzibar lilipotokea?
 
Mkuu almansoor mussa

Nadhani John Gideon Okello, alikuwa ni Mganda wa Lango.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…