Milio ya risasi imesikika katika kambi ya jeshi iliyo karibu na mji mkuu wa Mali Bamako, na kuzusha hofu ya kwamba Jeshi linataka kufanya uasi kwa Serikali iliyo madarakani katika Nchi hiyo ya ukanda wa Sahel inayoghubikwa na mzozo na maandamano ya Raia wakishinikiza Rais kuachia madaraka.
•
Bado hakuna taarifa za kutosha kubainisha kilichotokea, Mashahidi wa kiraia na wa kijeshi wamesema kuwa milio hiyo ya risasi ilitoka katika kambi ya jeshi ijulikanyo kama Kati, iliyo umbali wa takribani kilomita 15 kutoka Bamako.
•
Taarifa zinasema Wanajeshi wengi hawafurahishwi na hali ya kisiasa inayojiri nchini humo, na wanataka mabadiliko.
( via @dw_kiswahili )