Mapinduzi ya Mijadala JamiiForums: Zana Mpya za Akili Unde (AI) zinakuja Wikendi hii!

Watakulipia wafadhili kwa niaba yako maanaK wa sasa ufadhili kwa matumizi ya AI ni mingi.

Hata hivyo, ni vizuri kwa Jf kuendana na dunia inapoendaa ila natumai Mijadala haitopoteza ule mguso wa kibinadamu wa kawaida... Maana teknolojia kikizidi, authenticity hupungua
mimi sitaki wafadhili.. mkuu wacha kutumia maneno meusi unatuumiza macho au ndo umeanza kutumia akili mnemba..?
 
Habar yako kiongoz MELO

kaz nzur n vemà kuendana na nyakat zilozopo kwan AI haikwepek MILLENIUM wenzangu tukubal mabadiliko kwan Dunia inaenda kwa kaz ya 6G sasa

Sasa bwana max tujuze kuhusu matumiz ya VPN kuingia humu kwan inachosha na inaua betr Za simu zetu kwan mchakato huko TCRA umefikia wapi had sasa

Uwe unatupa updates boss
 
Je, umewahi kujiuliza mustakabali wa mijadala yetu hapa JamiiForums utakuwaje? Fikiria ulimwengu ambapo kuandika hoja nzito, kufanya utafiti wa kina, na kujibu mada mbalimbali kunakuwa rahisi, haraka, na kwa ubora wa kiwango cha juu zaidi.

Mimi na wenzangu (timu nzima) tunayo furaha kuwatangazia kuwa kuanzia wikendi hii, tunaleta mapinduzi hayo mikononi mwenu! Tunazindua zana mpya za Teknolojia ya Akili Unde/Mnemba (AI) hapa jukwaani.

Lengo letu si kubadilisha asili ya mijadala yetu inayoongozwa na binadamu, bali ni kuwapa uwezo zaidi ili kufanya mazungumzo yenu kuwa hai na yenye tija zaidi.

Zana hizi mpya zimeundwa kuwa rahisi sana kutumia na zitawapa faida zifuatazo mara moja:

1) Majibu Mahiri na Msaada wa Papo Hapo: Pata mapendekezo ya haraka ya kujenga hoja zako na msaada wa kimawazo unapokwama kuandika. Zitaokoa muda wako sana!

2) Utafiti wa Haraka: Kusanya taarifa na ukweli (facts) kwa haraka zaidi bila kulazimika kuondoka kwenye uzi.

3) Uchambuzi wa Picha: Unaweza kuweka picha na AI yetu ikakusaidia kusoma na kuchambua yaliyomo ndani yake kwa kina.

4) Kutengeneza Picha: Unahitaji picha maalum kusindikiza bandiko lako? Sasa utaweza kuiagiza AI itengeneze picha papo hapo kulingana na maelezo unayoyatoa. Hapa, inabidi uelewe 'prompt engineering' kwa kiasi ili kupata matokeo chanya.

Tungependa wanajamvi wote mpate nafasi ya kufurahia mabadiliko haya.

Tunaomba mzijaribu kwenye mada zenu kisha mtupatie mrejesho wa kweli kabisa—iwe ni sifa, changamoto mlizokutana nazo, au mapendekezo ya nini tuboreshe. Tafadhali, weka maoni yako yote kwenye huu uzi maalum. Mawazo yako yanatusaidia kuboresha zaidi.

Asanteni kwa kuendelea kuifanya JamiiForums kuwa sehemu bora na salama kwa fikra huru. Tukutane kwenye mijadala wikendi hii!

Nawatakia wakati mwema.
tunaisubiri kwa shauku kubwa ila isiwe na akili kama za meta Ai bali iwe na busara
 
Hayo ma AI yenu Huwa yanaongea mambo meeengi tena karibu 60% Huwa uongo.

Ulisema limekaea linajichekesha linarudi.kusahihisha Sasa Kuna haja gani ya kutumia tool ambayo haiaminiki?

Kwa mtu asiyetumia ubongo wake AI inaweza kukupoteza mbaya sana.
 
Hata kuitumia AI yataka akili mkuu wangu. Ukiitumia kienyeji, unapata matokeo ya kienyeji.

Ni sawa na wakati mtandao unaanza, wengi walisema mtandaoni pamejaa uongo, matusi, kutongozana etc.

Ni vile mtu anaitumia zana flani, anaishia na matokeo sawa na alichoingiza.
 
Habar yako kiongoz MELO

kaz nzur n vemà kuendana na nyakat zilozopo kwan AI haikwepek MILLENIUM wenzangu tukubal mabadiliko kwan Dunia inaenda kwa kaz ya 6G sasa

Sasa bwana max tujuze kuhusu matumiz ya VPN kuingia humu kwan inachosha na inaua betr Za simu zetu kwan mchakato huko TCRA umefikia wapi had sasa

Uwe unatupa updates boss
Mkuu,

Jitihada zipo kubwa tu. Mamlaka zaidi ya TCRA zimekuwa engaged.

Next week naamini kutakuwa na update ya maana sana (if not over this weekend too).

Asante
 
Back
Top Bottom