Emmanuel kant
JF-Expert Member
- Mar 15, 2026
- 333
- 857
Tafteni namna ukimblock mwashamba na watu wajamii yake usione chochote kutoka kwake hadi um unblock. Nyuzi zao zinatia kichefuchefu, ignore iko soft sana. Punguzeb na censorship na kuunganisha nyuziAsante sana mkuu wangu.
Kimsingi, nimetaja BAADHI ya kitakachokuwemo ila NI ZAIDI ya hapo.
tunaisubiri....Hahaha, lengo ni kuboresha. Kuna faida kubwa kuliko hasara
mimi sitaki wafadhili.. mkuu wacha kutumia maneno meusi unatuumiza macho au ndo umeanza kutumia akili mnemba..?Watakulipia wafadhili kwa niaba yako maanaK wa sasa ufadhili kwa matumizi ya AI ni mingi.
Hata hivyo, ni vizuri kwa Jf kuendana na dunia inapoendaa ila natumai Mijadala haitopoteza ule mguso wa kibinadamu wa kawaida... Maana teknolojia kikizidi, authenticity hupungua
tunaisubiri kwa shauku kubwa ila isiwe na akili kama za meta Ai bali iwe na busaraJe, umewahi kujiuliza mustakabali wa mijadala yetu hapa JamiiForums utakuwaje? Fikiria ulimwengu ambapo kuandika hoja nzito, kufanya utafiti wa kina, na kujibu mada mbalimbali kunakuwa rahisi, haraka, na kwa ubora wa kiwango cha juu zaidi.
Mimi na wenzangu (timu nzima) tunayo furaha kuwatangazia kuwa kuanzia wikendi hii, tunaleta mapinduzi hayo mikononi mwenu! Tunazindua zana mpya za Teknolojia ya Akili Unde/Mnemba (AI) hapa jukwaani.
Lengo letu si kubadilisha asili ya mijadala yetu inayoongozwa na binadamu, bali ni kuwapa uwezo zaidi ili kufanya mazungumzo yenu kuwa hai na yenye tija zaidi.
Zana hizi mpya zimeundwa kuwa rahisi sana kutumia na zitawapa faida zifuatazo mara moja:
1) Majibu Mahiri na Msaada wa Papo Hapo: Pata mapendekezo ya haraka ya kujenga hoja zako na msaada wa kimawazo unapokwama kuandika. Zitaokoa muda wako sana!
2) Utafiti wa Haraka: Kusanya taarifa na ukweli (facts) kwa haraka zaidi bila kulazimika kuondoka kwenye uzi.
3) Uchambuzi wa Picha: Unaweza kuweka picha na AI yetu ikakusaidia kusoma na kuchambua yaliyomo ndani yake kwa kina.
4) Kutengeneza Picha: Unahitaji picha maalum kusindikiza bandiko lako? Sasa utaweza kuiagiza AI itengeneze picha papo hapo kulingana na maelezo unayoyatoa. Hapa, inabidi uelewe 'prompt engineering' kwa kiasi ili kupata matokeo chanya.
Tungependa wanajamvi wote mpate nafasi ya kufurahia mabadiliko haya.
Tunaomba mzijaribu kwenye mada zenu kisha mtupatie mrejesho wa kweli kabisa—iwe ni sifa, changamoto mlizokutana nazo, au mapendekezo ya nini tuboreshe. Tafadhali, weka maoni yako yote kwenye huu uzi maalum. Mawazo yako yanatusaidia kuboresha zaidi.
Asanteni kwa kuendelea kuifanya JamiiForums kuwa sehemu bora na salama kwa fikra huru. Tukutane kwenye mijadala wikendi hii!
Nawatakia wakati mwema.
Hayo ma AI yenu Huwa yanaongea mambo meeengi tena karibu 60% Huwa uongo.Je, umewahi kujiuliza mustakabali wa mijadala yetu hapa JamiiForums utakuwaje? Fikiria ulimwengu ambapo kuandika hoja nzito, kufanya utafiti wa kina, na kujibu mada mbalimbali kunakuwa rahisi, haraka, na kwa ubora wa kiwango cha juu zaidi.
Mimi na wenzangu (timu nzima) tunayo furaha kuwatangazia kuwa kuanzia wikendi hii, tunaleta mapinduzi hayo mikononi mwenu! Tunazindua zana mpya za Teknolojia ya Akili Unde/Mnemba (AI) hapa jukwaani.
Lengo letu si kubadilisha asili ya mijadala yetu inayoongozwa na binadamu, bali ni kuwapa uwezo zaidi ili kufanya mazungumzo yenu kuwa hai na yenye tija zaidi.
Zana hizi mpya zimeundwa kuwa rahisi sana kutumia na zitawapa faida zifuatazo mara moja:
1) Majibu Mahiri na Msaada wa Papo Hapo: Pata mapendekezo ya haraka ya kujenga hoja zako na msaada wa kimawazo unapokwama kuandika. Zitaokoa muda wako sana!
2) Utafiti wa Haraka: Kusanya taarifa na ukweli (facts) kwa haraka zaidi bila kulazimika kuondoka kwenye uzi.
3) Uchambuzi wa Picha: Unaweza kuweka picha na AI yetu ikakusaidia kusoma na kuchambua yaliyomo ndani yake kwa kina.
4) Kutengeneza Picha: Unahitaji picha maalum kusindikiza bandiko lako? Sasa utaweza kuiagiza AI itengeneze picha papo hapo kulingana na maelezo unayoyatoa. Hapa, inabidi uelewe 'prompt engineering' kwa kiasi ili kupata matokeo chanya.
Tungependa wanajamvi wote mpate nafasi ya kufurahia mabadiliko haya.
Tunaomba mzijaribu kwenye mada zenu kisha mtupatie mrejesho wa kweli kabisa—iwe ni sifa, changamoto mlizokutana nazo, au mapendekezo ya nini tuboreshe. Tafadhali, weka maoni yako yote kwenye huu uzi maalum. Mawazo yako yanatusaidia kuboresha zaidi.
Asanteni kwa kuendelea kuifanya JamiiForums kuwa sehemu bora na salama kwa fikra huru. Tukutane kwenye mijadala wikendi hii!
Nawatakia wakati mwema.
Hata kuitumia AI yataka akili mkuu wangu. Ukiitumia kienyeji, unapata matokeo ya kienyeji.Kwa mtu asiyetumia ubongo wake AI inaweza kukupoteza mbaya sana.
Tutaelekezana, mdogo mdogoJambo zuri sana hili la kimapinduzi, Sasa mkuu Melo kwenye "prompt engineering" mtupige msasa kidogo ili tuweze kupata AI ideas inayokidhi viwango.
Dah, hili swali la TCRA.Maxence Melo kwanini jamiiforums haipatikani Tanzania?
Unamaanisha nini mkuu?Nona sana.
Kama hiyo AI ikinisuta kwa lugha chafu na nikaireport,Naam, kwa wale mnaopenda misuto - itaweza.
Pia, kutakuwa na version ya games
Nashukuru Mkuu, maana hii kitu inasumbua sana, unataka picha ikae hivi inakuja kivingineTutaelekezana, mdogo mdogo
Mkuu,Habar yako kiongoz MELO
kaz nzur n vemà kuendana na nyakat zilozopo kwan AI haikwepek MILLENIUM wenzangu tukubal mabadiliko kwan Dunia inaenda kwa kaz ya 6G sasa
Sasa bwana max tujuze kuhusu matumiz ya VPN kuingia humu kwan inachosha na inaua betr Za simu zetu kwan mchakato huko TCRA umefikia wapi had sasa
Uwe unatupa updates boss
Itakula bonge la ban. Ila, nayo imefunzwa kuwa na adabuKama hiyo AI ikinisuta kwa lugha chafu na nikaireport,
Na yenyewe mtaipiga Ban?
Ni kweli, wengi huishia kupata matokeo wasiyotarajia tokana na kutojua hasa walitakiwa ku-prompt vipi.Nashukuru Mkuu, maana hii kitu inasumbua sana, unataka picha ikae hivi inakuja kivingine