Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Kule Zanzibar karume akifanya hiyo,na huku Tanganyika Nyerere,aliwafuta kabisa wapigania wa uhuru halisia wa Tanganyika,na yeye akajipa ubaba wa taifa,hii nayo Ni dhambi kubwa,
 
Nimeona mtu anaitwa Mohamed Shamte Hamad ambaye alikuwa waziri mkuu je na yule anayeitwa AbdulJamshid alikuwa ni nani? Pia ni nani alikimbilia uingereza baada ya mapinduzi? Msaada tafazali.
Alikimbilia uingereza Kwa Masada wa Nyerere.
 
Alikimbilia uingereza Kwa Masada wa Nyerere.

Ndugu zangu,
Anaetaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar asome kitabu alichoandika
Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Humo ndimo atawajua viongozi wa kweli wa Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964.

Haiyumkiniki kuwa John Okello awe na uwezo wa kupanga mapinduzi na kisha
kuyatekeleza.

Kupanga mapinduzi kunahitaji fikra na uwezo wa mali na uwanja wa kutekeleza
azma hiyo.

Okello hakuwa na lolote katika hayo.
Nani basi walikuwa vinara wa mapinduzi?

Ingia hapo chini kukisoma kitabu hicho katika mtindo wa, ''Elimu Bila Khiyana,''
kama apendavyo kusema Maalim Faiza:

https://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf
 
Ahsante sana Bwana Mohammed said,kitabu tumekipata,nawashauri wasiokisoma,ni bora wakakipitia,sababu ndani yake kuna kweli wa mambo,yalivyokuwa haswa,ningeomba vile vile kama utakuwa na kitabu cha historia ya waasisi Haswa wa uhuru na ukombozi wa Tanganyika,natanguliza shukurani.
 
Abuha kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika soma kitabu cha Abdul Sykes .
 
Baada ya kumsikiliza Okello hebu sikiliza hapo chini:
Dropbox - KIPINDI MAALUM RADIO KHERI 104.10 FM MIAKA 50 MAPINDUZI YA ZANZIBAR.m4a
Mohamed Said: SIKIZA KIPINDI MAALUM: MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA 1964
 
Heri ya mapinduzi!

Sote tunajua kuwa kamanda John okello ndiye aliorganize vijana zaidi ya 600 na kuwaongoza katika mapambano ya kuipindua serikali ya wachache ya kisultani ya sultan jamshid bin abdulah.

Usiku ule wa 12 January 1964, bw. Okelo alifanya kazi nzito iliyogharimu maisha ya watu (ingawa wapo wanaosema kuwa hakukuwa na umwagaji damu lakini kiuhalisia syo kweli).

Kupitia mapinduzi yaliyotekelezwa kikamilifu na bw. Okelo, kwa mara ya kwanza, watu weusi wakafanikiwa kushka madaraka ya juu huku marehemu abeid aman karume akiwa rais wa kwanza wa SMZ.

Sasa wakuu tuelezane, hv kwanini John okelo hatajwi ktk haya maadhimisho ya mapinduzi badala yake anaenziwa karume pekee?

Inasemekana jamaa alikimbilia Uganda, kwanini?

Karibuni.
 
Historia inaandikwa na washindi. Okello alipigwa chini kijanja. Nai amkumbuke mtu kama huyo
 
Nasikia alikuwa mbeba mizigo bandarini ila alikuwa na kikundi chake cha mapambano ambacho kilikuwa tayari kupambana kwa yeyote atakaewalipa pesa ya maana
So huyu alikodishwa na kina karume kama mpiganaji tu
Siku zote historia huwakumbuka wapanga mikakati ya mapinduzi
 
Kwasababu ni Mgalatia.

Hakuna sababu nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…