Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

kwani bigjii ikiisha utamu si inatemwa? yeye alitumika kwa lengo maalum so baada ya lengo kukamilika si basi na yeye kazi yake imeisha
 
Mbona wewe umeshamkumbuka na hapa umetukumbusha sisi!
 
Aise yule mzee Mohamed Saidi yupo wapi? Maisha yamebana hadi nashindwa malizia kile kitabu Kwaheri Uhuru Kwaheri ukoloni
 
Wakati Mobutu seseseko anapinduliwa Hayati Laurent Kabila alikuwa Mikocheni Dar Es salaam

Wakati RPF wanakinukisha Kigali, Kagame alikuwa Kampala

Wakati wa Iran wanakinukisha Iran Ayatollah Khomein alikuwa Paris

Wakati Zimbabwe wanakinukisha Mnangagwa alikuwa Pritoria

Wakati wanajeshi wetu wanakinukisha Kampala Nyerere alikuwa Msasani Dsm
Wakati ZANU of wanakinukisha Zimbabwe Mugabe alikuwa Zambia

Viongozi wa Mapinduzi/ Mapambano huwa hawawi eneo la tukio ukiona upo eneo la tukio Wewe ni mpiganisha vita sio Kiongozi wa Vita ndio sababu Karume alikuwa Dar anakula bata Okelo akawa Eneo la tukio
Vp Kwa Fidel na Che mbona wote historia imewaandika? wakati Che hata urais hakuwahi kuwa
 
Vp Kwa Fidel na Che mbona wote historia imewaandika? wakati Che hata urais hakuwahi kuwa
Wewe unawajua Fidel na Cheguavara kwa kuwa ndio walioandikwa unawajua wasioandikwa? , Pengine kuna Watu wali play part kubwa kuliko Hao lakin hawakuandikwa na huwezi kuwajua!

Hata kwenye Mapinduzi ya Znz hajatajwa Karume pekee wapo kina Nassoro Moyo ( Baraza la Mapinduzi) hiyo kutajwa kwa Che hakumaanishi hakuna wasiotajwa

Pengine Kizazi cha kina Castro kikiisha madarakani watajitokeza wa Cuba walio play part kubwa lakin hawakutajwa popote
 
Kuna kitabu niliwahi kukisoma kinasema huyo jamaa alikuwa mkenya aliyeishi Uganda pia alichangia kukamilisha mapinduzi ya Zanzibar.

Baada ya hayo alirudi Uganda akawa mtu wa karibu sana na Idd Amin Dada wa Uganda ila alijiharibia baada ya kusema maneno haya 'NOW UGANDA HAS TWO FIELD MARSHALS'

usemi huo wa John Okello ulimuudhi sana dikteta Idd amin dada maana alihisi kama Okelo alikuwa na mpango wa kuja kumpindua basi Idd Amin Dada akamuua mapema tu, huo ndiyo mwisho wa John Okelo.
Okelo hakuuawa na Amin acha story za vijiweni humu
 
[HASHTAG]#naumbu[/HASHTAG] njoo hapa useme Nani alimuua John Okelo ili tupate kufahamu.
 
3607f2719f45cf9a0495656d116f1f55.jpg
Kwa wale wasiomjua Okelo ndiye huyo aliyekaa akiongea na Waandishi wa habari bàada ya Mapinduzi.
 
John Okello alikodishwa Kama Mpiganaji Mamluki.

Kwenye Sherehe za Uhuru wa Kidemokrasia wa Africa Kusini ushawahi kusikia Nyerere anatajwa kule?
Nyerere alipigana Frontline?
 
Pengine hakuwa na cheti cha kuzaliwa au cha darasa la vii.
 
Najaribu kuwaza, isingekua Okello kutokea kwenye picha za awali za mapinduzi pamoja na kutangaza mapinduzi hayo redioni, huenda leo tusingemsikia huyu mwanamapinduzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu kuwaza, isingekua Okello kutokea kwenye picha za awali za mapinduzi pamoja na kutangaza mapinduzi hayo redioni, huenda leo tusingemsikia huyu mwanamapinduzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna kitu utakigundua katika haya Mapinduzi
  1. kuna wanayoyakubali na kuyaenzi mpaka leo wanaona wamepata Uhuru na Ahueni
  2. na kuna wanaoyaona Mapinduzi km ni Haramu Sultani alikuwa na Haki ya kuendelea kutawala kwani alishinda na kupewa Uhuru na Mwingereza Disemba 10, 1963
sasa Okello hawamkubali kabisa, kwani walijua wale wakwezi na wakulima wasingeweza kujitawala na pia wanajua hadi leo wakirudi mabeberu wa Sultani itakuwa km Dubai
pana kazi Mkuu
 
Kazi kweli ipo.
 
Hayo ya kuwa Muasisi wa Tanu tunayapata kwenye maandiko ya Mohamed said kwa kuwa kiserikal kila kitu kafanya Nyerere na 'wenzie'

Kwa hiyo na kwa Zanzibar Mapinduzi alifanya Karume na 'wenzie' na Okelo yumo humo kwenye na 'wenzie'

Hata Africa kusini, Nyerere yupo kwenye Kundi la 'nakadhalika'

Karume Hakufanya Zanzibar. Acha kukariri Pumba za CCM
 
Mkuu katika Concept ya Historiography of African History yaani jinsi historia ya Africa ilivyo andikwa kuna Theory Nyingi zilitumika kuandika historia ya Africa miongoni mwazo ni

"The Great Man Theory "
Kwa mujibu wa theory hii inasema kwamba historia huwekwa na Mashujaa au Viongozi na hao ndio wanaitwa Makers of History

Kwaiyo kwa mujibu wa Nadharia hii ni kwamba atakaye zingatiwa kuwa ndiyo aliyefanikisha mapinduzi ya Zanzibar ( ZNZ Revolution ) ni Rais Karume na wala sio Okello

Kwaiyo kwenye Vitabu vingi vya historia utakuta Karume ndiye anayetambulika kama Mfanikishaji wa Mapinduzi ya Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom