Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

IFIKE WAKATI WAZANZIBARI NA WAPEMBA WAMTAMBUE RASMI BABA WA TAIFA LA ZANZIBAR NDUGU, JOHN OKELO.
BILA KUFANYA HIVYO, LAANA YA KUTUMIKA NA TANGANYIKA KUBAGUANA NA KUTAFUTA MADARAKA KWA GHARAMA YA KUIANGAAMIZA NCHI YAO ITAENDELEA KUWAANDAMA MILELE
 
Ubaba wake ukuepo kwa misingi ipi?
 
John Okello ambaye aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa mwaka 1937 huko Uganda katika kabila la Langi ambalo pia ni la Rais wa Zamani wa Uganda Milton Obotte. Alizaliwa akiitwa John Gideon Etuku. Wazazi wake walifariki Akiwa bado mdogo na kulazimika kwenda kulelewa na mjomba wake pamoja na wadogo zake wawili lakini kutokana na utukutu wake hakuweza kuishi kwa mjomba sababu alikuwa akipigwa na akakimbia kwenda kuanza vibarua huko Soroti katika Gineri ya kuchambua pamba. Inasemekana alitaka kwenda kujiunga na jeshi lakini hakufanikiwa kutokana na umri mdogo.

Katika harakati za kutafuta maisha alifika hadi Nairobi nchini Kenya na kuendelea hadi Mombasa ambapo alikuwa ukifanya kazi za vibarua. Alichukia kiuitwa boy , mtumishi, au mtumwa . Mwaka 1955 aliwekwa gerezani huko na akiwa humo alikutana na wapiganaji wa maumau waliokuwa wakipinga Ukoloni nchini Kenya kutoka kwao alipata hamasa ya Kupambana na ukoloni na ukandamizaji.

Mwaka 1959 akiwa na rafiki yake Mluo walienda Pemba katika eneo la Vitongoji na akawa anafanya kazi ya kugonga na kuuza mawe. Huko alipendwa na kuwa na ushawishi na ndipo alipoanza kuonesha nia yake ya kuuondoa utawala wa Sultan. Wakati anaondoka Pemba alipatia chama cha ASP nyumba yake ili waifanye ofisi ya chama.

Mwaka 1963 alihamia Unguja na kuanza kufanya kazi za kupaka rangi nyumba pamoja na kufanya kazi katika kiwanda cha kuoka mikate na akaendelea na vuguvugu la kisiasa.

Kumekuwa na Tetesi kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi na askari polisi na askari wa Mau mau lakini pia kuwa aliwahi kupigana wakati wa vita vya pili vya Dunia, dhana zote hizo si za kweli. Ukweli ni kuwa Okello hakuwahi kuwa mwanajeshi au kupata mafunzo ya kijeshi. Majigambo yake kuwa alikuwa na uzoefu wa kijeshi yalikuwa ni mbinu tu ya kumsaidia kuongoza mapinduzi

Alifanikiwa kuanzisha chama cha Mafundi rangi wa Unguja na Pemba na kupitia chama hicho aliweza kupenyeza ushawishi wake wa kufanya mabadiliko ya kumuondoa Sultan

Baada ya kufanikisha Mapinduzi aalimkaribisha Karume kuongoza serikali. Tatizo la Okello hakuwa na back up ya kisiasa na hakuweza kuaminika. Akatupwa na kufukuzwa bila shukrani. Mwanzoni alipelekwa Kenya lakini akafanya jitihada za kutaka kurudi nchini akakamatwa Mwanza na kufungwa. Lakini baadae akarudi Uganda.

Wakati Idd Amini alipompindua Obotte mwaka 1972 alikwenda kumpongeza. Lakini baadae akawa na Mawasiliano na kundi la Obotte lililokuwa Tanzania, katika harakati za kutaka kujiunga na kundi hilo alikamatwa na kuuwawa na Idd Amin.

Kwa hiyo tunaona kuwa Okello alikuwa Mwanamapinduzi. Kuongoza na kushiriki Mapinduzi ya Zanzibar haikuwa kwa ajili ya Mshahara, bali ilitokana na nia yake ya dhati ya kupinga ukoloni na ukandamizaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu karume hakua na role yoyote kwenye mapinduzi yale.
 
Mkuu hiyo hadithi umeipata wapi? alihamia Unguja 1963 na ndani ya mwaka alifanya mapinduzi. Unafikiria mapinduzi ni jambo la masihara ?
 
Mhh...na Wafia dini wale wa itkadi kali utasemaje?
Okelo hakua na ugalatia kindakindaki historia yake amefungwa na kufukuzwa nchi zote EA alikua mkatili ndio maana aliongoza mapinduzi unless uniambie Wagalatia kindakindaki ni wauaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wakiandika ukweli ulivyo, hautakubalika bado. Lakini ukweli madaraka ndivyo yanavyopatikana. Madaraka ni kama kupata dhahabu au almasi kule mgodini. Ukipata madini hayo halafu uzubaa kidogo watu wenye hila wapo pale watakupora tu pengine hata kupoteza maisha yako. Ndivyo ilivyo kuwa kwa field marshal huyo wa enzi hizo. Hata kwao Uganda, kaburi au taarifa za kifo chake hazipo wazi.
 
Kagasheki??? ni nani tena. alifanya nini?
 
Gy
kuna nini hpo sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikubwa ni shinikizo kutoka jumuiya za kiwataifa na mashirika mbalimbali ya haki za kibinadamu, wanadai kuwa ule ulikuwa ni unyama (genocide) dhidi ya wanawake watoto na wazee wa kiarabu hasa wenye asili ya Oman, maana watu wenye asili ya Uajemi wawakuguswa hata kidogo.

Wengi waliuwa cold blooded yani unaambiwa walikuwa wanapanga mstari msururu mrefu na wote wanauwawa kwa upanga maana hata risasi zilikuwa chache yaani kifupi yale yalikuwa mapinduzi ya mapanga

Makaburi ya watu wengi(mass grave's) yalitapakaa maana ilikuwa ni ngumu kuzika watu wote kwa muda huo mfupi, sasa kutokana na pressure za media ndio kina Karume wakamrushia mpira Okelo na wao kwa kukwepa mkono wa jumuiya hizo za kibinadam wakaamua kujificha nyuma ya mgongo wa kaka mkubwa Tanganyika,

Na wao ndio waliomshinikiza mkapitalisti Nyerere aliolesoma Marekani na Ulaya na Missionary schools za haohao makapitalisti kugeukia upande wa wakomunisti chini ya uangalizi wa Abrahaman Babu(huyu jamaa unaambiwa ni hatari kuliko hata huyo Okelo mliemtia umaridadi)

Vitu vingi juu ya historia ya mapinduzi ya Zanziba havipo wazi, yani unaambiwa Okelo alikuja akadai ametumwa na Mungu cjui yesu kwenye nchi ambayo 99% ni waislam na kufanikiwa kupata sapoti ya wazawa bado haiingii akilini hata kidogo,

Kuna kitabu alikuwa nacho mwalimu wangu wa historia zamani hizo sidhani kama nnaweza kukipata nikiweke hapa, ila kuna documentary iliokwenye mfumo wa video ilirekodiwa na muitaliano mmoja akiwa kwenye helicopter inaonesha watu wanapanga mstari kwenda kuuliwa na pia inaonesha makaburi ya watu wengi na kuna mizoga ya watu wengine baharini wakijaribu kutoroka kwa kuogelea

sasa kipindi ambacho nyie mnataka akina John Okello waandikwe kama mashujaa wa mapinduzi wao watu wa haki za kibinadamu wanataka hao mashujaa wenu wajulikane kama wahalifu wa kivita sasa sijui mna compensation ya kuwalipa hao warab wa Oman [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…