Imekuwa kawaida kwa gazeti la Monitor la Uganda kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar kwa kutoa makala zinazomtambulisha Field Marshall John Okello kama kiongozi pekee wa mapinduzi ya Zanzibar.
Mwaka huu wametoa makala iliyoandaliwa na mwandishi Felix Ocen inayomtambulisha John Okello akiwa na miaka 25 akiongoza kikosi cha watu 600 kwa muda wa masaa tisa tu na kufanikisha kumpindua Sultani.
John Okello aliyeingia Zanzibar miaka minne kabla ya mapinduzi, alikuwa mzaliwa wa familia ya kawaida katika wilaya ya Alebtong kaskazini mwa Uganda.
Okello, baada ya harakati zake za mapinduzi aliandika kitabu alichokipa jina The Revolution in Zanzibar, lakini kilipigwa marufuku kuchapishwa na serikali zote za Afrika Mashariki.
Gazeti linasema kuwa Okello aliongoza D-Day na wafuasi wake bila uwepo wa watu tunaoambiwa waliongoza mapinduzi hayo yaani Abeid Karume na Abdurahman Babu. Hawa wawili walikuwa wamefukuzwa visiwani na utawala wa Sultan, na walishangazwa sana kusikia kuna mapinduzi Zanzibar.
Okello alifanya siri mpango wake wa D-Day mpaka ilipofika usiku wa tarehe 11 January 1964, alipowakusanya wafuasi wake na kuwaamuru kuivamia kambi ya silaha ya Ziwani wakiwa na silaha za jadi.
Baada ya kufanikiwa kuiteka kambi ya silaha huku walinzi wa kambi wakitoroka, Okello na wafuadi wake walielekea mji mkongwe wakiwa wamejiimarisha kwa silaha kali. Kwa masaa machache walifanikiwa kuuteka mji mkongwe huku Sultan akikimbilia Dar es salaam kuomba hifadhi kwa Nyerere, lakini Nyerere alikataa na ikamlazimu Sultani kuelekea Mombasa kisha Uingereza.
Mpaka kufika asubuhi, Okello na wafuasi wake walikuwa wameshikilia vituo vyote vya muhimu huku akiwaamsha wazanzibari kwa tangazo "
This is John Okello, the Field Marshall of Pemba and Zanzibar. Wake up you imperialists, there is no more imperialist government. Wake up you Blacks, pick the weapons and clear out the remnants of the imperialist government.... I am giving the Sultan 20 minutes to kill his children and wives and later himself, or else Okello will do it."
Mpaka kufika jioni watu takribani 13,000 walikuwa wameuliwa, huku zaidi ya 12,000 wakiwa waarabu. Viongozi wote ambao hawakufanikiwa kutoroka zahama ya Okello walitangaza kujisalimisha na kumuunga mkono Okello.
Okello aliunda kikosi cha wapiganaji wa mapinduzi kilichoitwa "Freedom Military Force" au Jeshi la Uhuru. Pia aliunda baraza la kwanza la mapinduzi, lakini walipompendekeza kuwa rais wa baraza alikataa. Badala yake aliwaita akina Karume kutokea Tanganyika, akampendekeza Karume kuwa Rais na Babu kuwa waziri mkuu.
Mengine fungua link usome wenyewe.
How Ugandan led revolution that ended Arabs reign over Zanzibar
Hapa kuna maswali kadhaa.
1. Kwanini CCM wanatudanganya watanzania na kuidanganya dunia?
2. Kuna faida gani tunazopata kwa kukataa kumtambua Okello kama kiongozi na baba wa taifa la Zanzibar?
3. Kwanini viongozi wa Afrika Mashariki walimwogopa Okello?
4. Inaonekana Okello alitekwa na watu wasiojulikana wakati wa utawala wa Iddi Amini na hajulikani alipopotelea mpaka leo. Serikali ya Zanzibar imefanya juhudi zipi ili haki za huyu Field Marshall zipatikane zikiwepo za kupewa heshima anayostahili?
Nawasilisha