Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Hilo nalo swali? Rais wenu anachaguliwa wapi na nani? Na akiwa mjeuri nini kinampata? Unamkumbuka aboud jumbe? Mi naona unabisha tu kinafiki ilhali wajua kuwa zanzibar inatawaliwa na Bara.ni kakoloni ketu kadogo. Rais tunamweka tunayemtaka sisi.

Nyie wenywe mnashindwa kujitawal mtaweza kutawala watu wengne?
 
Mwaka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.
Ukisema uhuru bandia unakosea ndugu mwanadishi. Muhammed Shamte Hamadi ndie waziri mkuu wa kwanza na ndie alipewa hati ya Uhuru mnammo tarehe 10/12/1963 ikitambulika Zanzibar Kama taifa huru. Huku likiandaliwa na bunge la Uingereza liwe chini ya jamhuri ya Kenya.
Muhammed Shamte Hamadi mnamo tarehe 10/12/1963. Na likawa linataumbulika taifa la Zanzibar lipo huru na umoja wa mataifa Hadi umoja wa dolar ya Uingereza.

Shamte akihutubia UN na Kisha kupewa hati ya Uhuru wa Zanzibar.
 
 
Historia inaandikwa tu kwa yale mambo yanayowapendeza wenye mamlaka
 
inashangaza sana kwa wale wanaokataa uwepo wa mkono wa nje katika hichi kinachoitwa mapinduzi.. John Okello alikua swahiba wa mwalimu kitambo na haishangazi kumuona akiclaim kuwa yeye ndo alikua mastermind wa yaitwayo mapinduzi. bahati mbaya iliyoje
 
KWANINI CHE GUEVARA ASIWE NDO JOHN OKELO WA LATIN AMERIKA.
UKOLONI MAMBO LEO WA MATAIFA YA MASHARIKI BADO UPO KAZINI
 
Sababu zanzibar serikali ndo inaomba omba kwetu kwa niaba ya watu wake milion 2. Kamkoa hako ndo tunakasadia.
Hata Rais mnashindwa kumpata mumekuja Zanzibar kuomba mwanamke awaongoze, mashoga ni shida
 
Hilo nalo swali? Rais wenu anachaguliwa wapi na nani? Na akiwa mjeuri nini kinampata? Unamkumbuka aboud jumbe? Mi naona unabisha tu kinafiki ilhali wajua kuwa zanzibar inatawaliwa na Bara.ni kakoloni ketu kadogo. Rais tunamweka tunayemtaka sisi.
Your browser is not able to display this video.
 
Hata Rais mnashindwa kumpata mumekuja Zanzibar kuomba mwanamke awaongoze, mashoga ni shida
Hilo jina lako uliona sababu Mod hawataruhusu Uondoe V. Uweke J? 😁😁😁😁 Why unajiita kiungo hicho? Ni sababu ndivyo ulivyo...
 
Historia ya kweli Tanganyika haiwezi kuiface. Okello alitumiwa na Nyerere kupindua Zanzibar, sasa tueleze unahitaji tuendelee na historia hii ? Au unapendelea ile ya kubabaisha ? Aliepinduliwa alikuwa kiongozi halali Zanzibar wakaekwa vibaraka vya Tanganyika ambavyo vimeuza mamlaka ya Zanzibar.

Maasalaam
 
Mr F.
Januari 2016 nilifanya kipindi na Azam TV kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar.
Baada ya kumaliza kipindi hicho nilikaa kitako nikaaandika hayo hapo chini:

''Leo asubuhi nilifanyiwa mahojiano na mtangazaji Faraja Sindegea wa Azam TV kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar.

Mtangazaji alifungua kipindi kwa utangulizi kuhusu historia ya mapinduzi na umuhimu wa kuyaenzi mapinduzi.

Nilimtaka radhi kwa kumwambia kuwa itafaa kama tutayazungumza mapinduzi kutoka kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru wa Zanzibar lakini michango yao haitambuliwa na nchi yetu.

Nilikwenda moja kwa moja kwenye kumbukumbu za Aman Thani kueleza yale ambayo si wengi wanayafahamu.

Watazamaji nadhani kwa mara ya kwanza waliona picha ya Aman Thani kwenye televiseheni zao na picha ndiyo hiyo hapo juu.

Nilieleza kuwa nimezisoma kumbukumbu za Aman Thani na niligusia umuhimu wa nyaraka zake kwa mwanafunzi yoyote yule anaejifunza historia ya siasa za Afrika hususan historia ya Zanzibar na mapinduzi yaliyokuja kutokea mwaka wa 1964.

Nimesema kuwa kumbukumbu za Aman Thani zinakuja na picha nyingine kabisa ya mapinduzi ambayo si wengi wanaijua.

Nilieleza kuwa ni Aman Thani peke yake katika wafungwa wa siasa wa Zanzibar aliyeweza kueleza kwa kirefu kuhusu Jela za Mateso zilizoundwa baada ya mapinduzi na jinsi alivokabiliana na Mtesaji Mkuu Hassan Mandera.

Niliwaonyesha watazamaji baadhi ya vitabu muhimu vya historia ya Zanzibar pamoja na kitabu, ''Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha,'' kitabu ambacho nilisema mwandishi Minael- Hosanna O. Mdundo amepotosha mambo mengi.

Mtangazaji Faraja alitaka kujua John Okello ni nani?

Nilimweleza kuwa John Okello hakuwa chochote katika mapinduzi ila alitumiwa kutoa matangazo ya kuwatisha wananchi.

Kwa lugha ya wenye mapinduzi yao ni kuwa, ''Walimvisha blanketi la U-Field Marshall na likamwenea na yeye mwenyewe akaamini khasa kuwa hakika ni ''Field Marshall.''

Hapa kuhusu, ''Blanketi la Okello,'' niliwapeleka watazamaji wangu kwenye rejea ya kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Nilimtaja Abdallah Kassim Hanga kuwa ndiye aliyepanga mapinduzi akishirikiana na serikali ya Tanganyika.

Katika muktadha huu niliwarejesha tena watazamaji kwenya kumbukumbu za Aman Thani aliposema kuwa hayakuwa ''mapinduzi,'' bali mavamizi.

Aman Thani nikaeleza kuwa ametoa changamoto katika picha maarufu ya Okello hapo chini kuwa atokee mtu awaonyeshe Wazanzibari khalis katika picha ile.''

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…