YAITWAYO "MAPINDUZI"
John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.
Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike.
Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!
Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!