Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja waje unataka kujua jinsi alivyo mchuviding..naniliuu nii!Wana jf mimi kama kijana mzalendo mwenye kiu ya kujua historia ya nchi yangu, katika kufuatilia historia ya mapinduzi ya Zanzibar nimekutana na jina la JOHN OKELLO kwamba ni miongoni mwa wapiganaji katika kuitafuta Zanzibar huru. Naomba kwa mwenye historia japo kwa ufupi ya mtu huyu anisaidie ili niweke kumbukumbu zangu sawa.
Okelo ndiye aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar siyo Karume. Historia imechakachuliwa na watawala ili kumpa ujiko Karume kwakuwa Okelo hakuwa mzawa. Baada ya kufanikiwa kupindua wakamtimua na kumpa ujiko Karume kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa mapinduzi hayo. Usisahau kuwa Karume naye asili yake ni MalawiWana jf mimi kama kijana mzalendo mwenye kiu ya kujua historia ya nchi yangu, katika kufuatilia historia ya mapinduzi ya Zanzibar nimekutana na jina la JOHN OKELLO kwamba ni miongoni mwa wapiganaji katika kuitafuta Zanzibar huru. Naomba kwa mwenye historia japo kwa ufupi ya mtu huyu anisaidie ili niweke kumbukumbu zangu sawa.
Okelo ndiye aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar siyo Karume. Historia imechakachuliwa na watawala ili kumpa ujiko Karume kwakuwa Okelo hakuwa mzawa. Baada ya kufanikiwa kupindua wakamtimua na kumpa ujiko Karume kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa mapinduzi hayo. Usisahau kuwa Karume naye asili yake ni Malawi
Okelo ndiye aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar siyo Karume. Historia imechakachuliwa na watawala ili kumpa ujiko Karume kwakuwa Okelo hakuwa mzawa. Baada ya kufanikiwa kupindua wakamtimua na kumpa ujiko Karume kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa mapinduzi hayo. Usisahau kuwa Karume naye asili yake ni Malawi
Hamjui mnaloliongea. tafuteni vitabu msome msitegemee stori za vijiweni.Kweli historia inakawaida ya kujirudia, kumbe hizi ndio tabia za Wazanzibari, wanapenda mtu mwingine awafanyie kazi wao wale tu basi and then waje wajisifu kua wamefanya wao, barabara, umeme, mishahara ya viongozi wao na pesa za kuhudumia Wazenji zote zinatoka bara, mara baada ya mambo kua mazuri sasa wanadai wajitenge, kisa tu eti vipimo vya kijiolojia vinaonesha Zanzibar kuna mafuta! Sijui kwanini hawa watu hua hawana shukurani.
YAITWAYO "MAPINDUZI"
John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.
Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!
Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.
Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.
Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]
Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?
Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?
Mwanamapinduzi John Okello kama ijulikanavyo katika Historia kwamba ndiye aliye ongoza kikundi kidogo cha Makamanda na kuipindua serikali ya Sultan Jemshid huko Zanzibar. Lakini, cha kushangaza huyu Mkombozi aliishia kufukuzwa Zanzibar...
Alipotelea mikononi mwa Field Marshal Idd, DSO, The conquerer of British Empire!