Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

UKWELI WA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho na mauaji kwa miaka 51 sasa. Vizazi vimelishwa uongo wa uhalisia wa mapinduzi na wanamapinduzi wa kweli wa Zanzibar bila sababu za msingi, lakini kwa maslahi ya watawala wa Zanzibar kwa msaada wa watawala wa Tanganyika leo Tanzania. Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963. Na huu ndio uhalisia wa uhuru wa Zanzibar nje ya mapinduzi ya John Okello yaliyotekwa na Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume

Leo taifa la Zanzibar linaadhimisha kile kiitwacho ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, lakini uadhimishwaji huo upo katika msingi ule ule wa kilaghai na ghiriba. Wanamapinduzi halisi wametupwa, hawatajwi wala kukumbukwa popote na zaidi wengi wamefutwa usoni pa dunia. Wamevishwa wengine taji la mapinduzi ilihali hawakujua hata kilichotokea Usiku wa tarehe 12 Januari 1964. Karume huyu Abeid hakujua hata mapinduzi hayo yaliandaliweje na nini kilitoke bali aliyajua mapinduzi yao yaliyokuwa yakiratibiwa Dar es Salaam chini ya Juius Nyerere

Lakini ukweli unaanzia kwenye kundi la watu 300 waliokitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.

Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.

Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbalimbali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhidi ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.

John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello. Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.

Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo). Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.

Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa "Mapinduzi". Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.

Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyingine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye.

John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao." Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa" na "Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito. Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000".

Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha" Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na PembaNafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija", " na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba... Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu"

Huko mjini Dar es Salaam ndani ya kipindi cha mapinduzi kulikuwa kugumu sana, hata Julius aliingiwa na hofu ya utawala wa mkono wa chuma wa Okello, sasa ikaanza kusukwa mikaka ya kumpoka mamlaka Okello, Okello hakuwa na chama cha siasa hivyo Mwalimu akapendekeza liundwe baraza la mapinduzi na Okello awe ndie mkuu wa baraza hilo ambalo ndilo litakuwa na mamlaka yote ya Zanzibar.
Okello alikubali wazo hilo ambalo kikao kilifanyikia Dar es Salaam 1/2/1964, ikakubaliwa urais apewe kiongozi wa chama cha siasa yani Karume lakini asiwe na sauti yoyote katika Zanzibar.

Baada ya mgawanyo huo ilikubaliwa pia Abdulahman Babu awe mkuu wa vyombo vya habari pia akiwa ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Walikubalikubaliana kuwa tare 1/4/1964 warejee tena Dar kwaajili ya kumalizia mipango ya kuitawala Zanzibar. Hapo ndipo siku aliyokwenda kufutwa Okello katika ardhi ya Tanganyika na Zanzibar katika msingi na muundo wa kisiasa, viongozi na wajumbe wote wa baraza la mapinduzi walipanda ndege moja kuja Dar akiwemo Mungu wa Afrika Okello, walipofika uwanja wa ndege, itifaki iligeuzwa na John Okello akaambiwa asubiri kushuka awe wa mwisho. Baada ya kushuka wajumbe wote ndani ya ndege ile, alikwende komandoo mmoja wa Kitanganyika aliyeita Mzena ambaye baadae alikuwa kuwa mkuu wa ujasusi. Alimwamuru Okello asalimishe silaha yake na kisha kumwamuru rubani aipaishe ndege kuelekea Nairobi.

Kenyatta alimuambia Nyerere kuwa mtu huyo (Okello) sio wa Kenya hivyo ndege ikaelekezwa Uganda ambako alibwagwa na historia yake ikaishia hapo. Huku nyuma kazi ya propaganda ya kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli ilisimamiwa na Babu, alipiga propaganda kupitia radio kuwa akiyefanya mapinduzi ni Karume na ASP, hata chama chake cha UMMA Party hakukisemea tena.

Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi. Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.

Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995, 2000, 2010 na mwingine unatarajiwa hapo Oct 2015. Viongozi walaghai na wenye kujali hali za siasa zao wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani kwa jicho la tatu. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe,

Katika uga huu wa kisiasa nikuwa matakwa ya Wazanzibar katika siasa mpya bado yanafinyangwa bila sababu za msingi. Tutumie mda wetu kumuenzi mwanamapinduzi wetu Che Guevara wa Afrika Field Marshal John Okello baba wa Taifa la Zanzibar.

Niwapongeze ndugu zangu Ahamed Bargash, Mohamed Said, Dr Harith Ghasany na wengine wengi wanaopigana na kurejeshwa kwa historia ya kweli ya Zanzibar

We tapeli umemplipa Oluoch
 
Last edited by a moderator:
So notorious. Unatukebehi. Tungejuaje historia ya mapinduzi kama wale walioshiriki wasingetukalisha chini na kutusomesha. Tungeliyakuaje ya Kipumbwi na Sakura kama Victor Mkello na Mzee Mkwawa wasingetufungulia milango ya.siri ile nzito? Dr. Ghassany alifanya utafiti. Kapita maktaba nyingi America na Uingereza hadi nyumbani kwa Mzee Mkwawa Makorola Tanga na Nguvumali. Huko hakuonyeshwa nyaraka. Kule alielezwa kuhusu kambi ya askari mamluki wa Kimakonde wakata mkonge kutoka shamba la.Sakura waliokuwa wakifanya mazoezi porini. Regional Commissioner Jumanne Abdallah na Area Commissioner Ali Mwinyi Tambwe wote wakisimamia mpango ule. Dr. Ghassany hakuyakuta haya katika utafiti wake Library of Congress Washington wala Rhodes House Oxford. Haya kaja elezwa Tanga Makorola na Nguvumali na watu ambao hakuna aliyekuwa anajua mchango wao. Hakika kwa kiasi chetu tunaijua historia ya mapinduzi.
 
Tatizo ni kuwa ukweli wa mapinduzi anaujua Mohamed Said na Harith watu wengine wote walikuwa wajinga na vipofu wakati mapinduzi yanatokea


SoNotorious,
Unatukebehi.
Hii si dalili nzuri kwako.

Inaonyesha kushindwa na hoja zangu.
Mimi huwa sizungumzi kile nisichokijua naogopa kufedheheka.

Tungejuaje historia ya mapinduzi kama wale walioshiriki hasa
wasingetukalisha chini na kutusomesha?

Tungeliyakuaje ya Kipumbwi na Sakura kama Victor Mkello na
Mzee Mkwawa wasingetufungulia milango ya siri ile nzito ya
mamluki wa Kipumbwi?

Dr. Ghassany alifanya utafiti wa miaka.

Kapita maktaba nyingi Amerika na Uingereza hadi nyumbani kwa
Mzee Mkwawa Makorola Tanga na Nguvumali.

Huko hakuonyeshwa nyaraka.

Kule alielezwa kuhusu kambi ya askari mamluki wa Kimakonde
wakata mkonge kutoka shamba la Sakura waliokuwa wakifanya
mazoezi ya kuvamia Zanzibar porini.

Regional Commissioner Jumanne Abdallah na Area Commissioner
Ali Mwinyi Tambwe wote wakisimamia mpango ule.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mmoja wa watu ambao hawakutaka
ijulikane kuwa alihusika katika mapinduzi.

Ali Mwinyi Tambwe alikataa kuzungumza na marehemu Prof.
Haroub Othman
alipomgusia habari ya mapinduzi.

Nafsi yake iliingia hofu kubwa alipokujajua watu waliouliwa katika
mapinduzi yale.

Dr. Ghassany hakuyakuta haya ya Sakura, Kipumbwi na mamluki
wa Kimakonde katika utafiti wake Library of Congress Washington
wala Rhodes House Oxford.

Haya kaja elezwa Tanga Makorola na Nguvumali na watu ambao
hakuna aliyekuwa anajua mchango wao.

Hakika kwa kiasi chetu tunaijua historia ya mapinduzi.

Ilimchukua miaka mitatu kwa Dr. Ghassany kuweza kumshawishi
Victor Mkello kumuamini kuwa likuwa ni mtafiti wa kweli na wala
hatoki International Criminal Court (ICC) Hague ndipo alipokubali
kuongea.

Mimi nilikuwapo katika mahojiano yote ya miaka mitatu ya nyuma
isipokuwa huu wa mwisho alipofunguka na kueleza ukweli wa yale
waliyofanya katika kuivamia Zanzibar kutoka Kipumbwi.

Mimi nilibaki nje nimeegesha gari yangu msikitini.

Nilijua kuwa hii ndiyo ile kubwa yake nilitaka Dr. awe na ''one on
one,'' na Mzee Mkello.

Baadae Dr Ghassany aliniambia kuwa mama yetu mkewe Mzee
Mkello
alikuwapokatika mazungumzo yale na sababu yake ni kuwa
Mzee Mkello alitaka ili akikosea au kusahau jambo amkumbushe.

Soma ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' umsikilize nini Mkello
alisema.

Baada ya Dr. Ghassany kueleza yale yaliyopitika Kipumbwi kati
ya 1961 na 1964 kwa watu kuvushwa kutoka Tanganyika kwenda
kuipigia kura ASP watafiti wengi wa nje wakataka kuja Tanga
kufanya uthibitisho.

Picha hiyo hapo chini mmoja wa watafiti kutoka Marekani akimhoji
Mama Mkello nyumbani kwake Nguvumali, Tanga.

20130830_103414.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

==============



Video ikimwonesha Okello,Karume na Babu masaa machache baada ya Mapinduzi



Philomon Mikael,
Nakuomba hebu linganisha maelezo uliyobandika na jibu langu kwa
SoNotorious.

Naamini utaona mpishano uliokuwapo.
Mapinduzi ya Okello ni mapinduzi ya kuzuka usiku mmoja.

Mapinduzi niliyoeleza mimi kwa kumnukuu Dr. Harith Ghassany ni
mapinduziyaliyopangwa na kuratibiwa na wajuzi wa mipango -
Abdullah Kassim Hanga,Oscar Kambona juu kwenye kinara.

Chini yao kwenye ''Zone of Operation,'' kuna maofisa wa serikali ya
Tanganyika-Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe.

Chini ya hawa kuna Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello.

Hawa ndiyo walikuwa wakiwasiliana na mamluki wa Sakura na
Kipumbwi.

Nadhani hii ''Chain of Command,'' unaiona.
Nani anawajibika kwa nani na kwa kipi.

Mzee Mkwawa anasema hata siku moja Kambona wala si Hanga
walifika kambini Kipumbwi kuzungumza na ''askari.''

Simlazimishi mtu kuamini yale aliyoeleza Dr. Ghassany kwenye
kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' lakini Waswahili
tuna msemo, "Penye ukweli uongo hujitenga.''
 
Last edited by a moderator:
Philomon Mikael,
Nakuomba hebu linganisha maelezo uliyobandika na jibu langu kwa
SoNotorious.

Naamini utaona mpishano uliokuwapo.
Mapinduzi ya Okello ni mapinduzi ya kuzuka usiku mmoja.

Mapinduzi niliyoeleza mimi kwa kumnukuu Dr. Harith Ghassany ni
mapinduziyaliyopangwa na kuratibiwa na wajuzi wa mipango -
Abdullah Kassim Hanga,Oscar Kambona juu kwenye kinara.

Chini yao kwenye ''Zone of Operation,'' kuna maofisa wa serikali ya
Tanganyika-Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe.

Chini ya hawa kuna Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello.

Hawa ndiyo walikuwa wakiwasiliana na mamluki wa Sakura na
Kipumbwi.

Nadhani hii ''Chain of Command,'' unaiona.
Nani anawajibika kwa nani na kwa kipi.

Mzee Mkwawa anasema hata siku moja Kambona wala si Hanga
walifika kambini Kipumbwi kuzungumza na ''askari.''

Simlazimishi mtu kuamini yale aliyoeleza Dr. Ghassany kwenye
kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' lakini Waswahili
tuna msemo, "Penye ukweli uongo hujitenga.''

Nmekisoma kitabu cha Dr.Ghassany nmejifunza mambo mengi kwenye icho kitabu...hata wewe mwenyewe nmesoma vitabu vyako nmejifunza mambo mengi....

Lakini mpo wabinafsi sana na hiyo inawezekana kwa makusudi au kutokana na historia ya maonevu ambayo umeyapointi kwenye maandiko yako mengi...mfano pale unaposema eti Okello akuweza kuandika kitabu kama kile napata wasiwasi na wewe.....hivi kuna tofauti gani kati ya kuandika wewe mwenyewe na kumuadithia mtu akaandika kile unachokijua...na wewe unatupa sababu gani ili tuziamini sources zako.

Historia imeamua iwe hivyo na kamwe hamuwezi kuibadilisha...niliposomaga kitabu cha mabadiliko cha uchina ya kale #i_ching nilijifunza mambo mengi sana.

Dr.ghassany na wewe ni wanaharakati wa kiislamu na icho kitu dunia imeshajua....pro Islamic wahhabism.

Ndio maana kila mnachoonge lazima mtaje uislamu.....ying yang....mmeshindwa kwa karne nyingi na huo ndio ukweli..
 
Nmekisoma kitabu cha Dr.Ghassany nmejifunza mambo mengi kwenye icho kitabu...hata wewe mwenyewe nmesoma vitabu vyako nmejifunza mambo mengi....

Lakini mpo wabinafsi sana na hiyo inawezekana kwa makusudi au kutokana na historia ya maonevu ambayo umeyapointi kwenye maandiko yako mengi...mfano pale unaposema eti Okello akuweza kuandika kitabu kama kile napata wasiwasi na wewe.....hivi kuna tofauti gani kati ya kuandika wewe mwenyewe na kumuadithia mtu akaandika kile unachokijua...na wewe unatupa sababu gani ili tuziamini sources zako.

Historia imeamua iwe hivyo na kamwe hamuwezi kuibadilisha...niliposomaga kitabu cha mabadiliko cha uchina ya kale #i_ching nilijifunza mambo mengi sana.

Dr.ghassany na wewe ni wanaharakati wa kiislamu na icho kitu dunia imeshajua....pro Islamic wahhabism.

Ndio maana kila mnachoonge lazima mtaje uislamu.....ying yang....mmeshindwa kwa karne nyingi na huo ndio ukweli..

Chuma Cha Reli,
Hakika mimi ni Muislam na natafakhari na kumshukuru Allah kwa kunijaalia
Uislam iwe dini yangu.

Hilo kuwa mimi ni Mhabi...
Siyo na ningelikuwa ningelikufahamisha bila wasiwasi wowote.

Huwa sifichi kile ninachokiamini.

Kuwa mimi ni mbinafsi hilo umesema wewe na ni fikra zako siwezi kabisa
kukuingilia.

Ikiwa sasa unasema kuwa Okello hakuandika kitabu kile ila alimhadithia
mtu na yeye akaandika hapo tumekwenda kwengine.

Wewe umesogea mbele kutoka Okello mwandishi kwenda kwa Okello
muhadithiaji stori.

Hili la kuwa alimhadithia mtu yale aliyofanya Zanzibar sikuwa na haja ya
kuelezwa na mtu kwani lilikuwa dhahiri.

Alex Hailey aliandika "biography" ya Malcolm X...
Alibadilisha mambo mengi sana alipokufa Malcolm.

Hii ndiyo hatari ya kuandikiwa.
Nadhani sasa umenielewa.
 
Je Mwanamalundi vipi alifungwa kisiwa cha mwanamalindi pale bahari ya hindi si mbali sana na Dar lakini akaonyesha maajabu makubwa ya kutembea juu ya bahari kwenda Dar na kurudi, pia alipanda viazi vikakomaa kwa usiku mmoja tu. ndipo wakoloni walipoona power yake wakaamua kumuachia.
huyu ni shujaa wa kWELI MWANAMALUNDI . Alikuwa na uwezo wa kukusha miti kwa kunyoosha kidole tu yaani hizi historia zimefunikwa funikwa suji kwa nini. jamani tusaidiane kuziweka sawa.
 
YAITWAYO "MAPINDUZI"​

John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.

Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!

Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!

Besty,
Sheikh Ali Muhsin Barwani wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar
alikuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) vilevile chama
hiki kikijulikana kama Hizbu. Kwa mapenzi makubwa wanachama
wa Zanzibar walikuwa wanamwita, "Zaim" yaani Kiongozi.

Ilikuwa ni ya Sheikh Ali Muhsin Zanzibar ipiganie uhuru wake chini
ya chama kimoja cha kizalendo chenye nguvu chama cha kitaifa
badala ya vyama vilivyojijenga katika misingi ya rangi.

Ilikuwa pigi kubwa sana kwake Abeid Amani Karume alipoasisi
Afro Shirazi Party, chama kilichosimama kwa maslahi ya Waafrika
na Washirazi.

Sheikh Ali Muhsin alipigania uhuru wa Zanzibar mpaka ukapatikana
tarehe 10 December 1963.

Sheikh Ali Muhsin alishiriki katika mkutano wa katiba Lancaster
House.

Baada ya mapinduzi yaliyotokea Zanzibar tarehe 12 Januari 1964
Sheikh Ali Muhsin alikamatwa na kusafirishwa Tanganyika ambako
alifungwa Ukonga na jela nyingine kwa kipindi cha miaka 10 na
miezi michache.

Katika kipindi alichokuwa kifungoni Sheikh Ali Muhsin aliandika
miswada kadhaa ambayo alikuja kuichapa kama vitabu baada ya
kutoka kifungoni.

Kabla hajafa mwaka 2006 Sheikh Ali Muhsin aliandika kitabu cha
maisha yake, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,'' ambacho kilikuja
kufasiriwa kama ''Kujenga na Kubomolewa Zanzibar.''

Katika kitabu hiki cha maisha yake Sheikh Ali Muhsin anaeleza
yaliyopitika Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi.

Baada ya kushindwa kupata pasi ya kusafiria, Sheikh Ali Muhsin
alitoroka nchini mwaka 1974.

Hadi anafariki siku zote Sheikh Ali Muhsin alikuwa akisema yale
hayakuwa mapinduzi bali mavamizi.
 
Philomon Mikael,
Nakuomba hebu linganisha maelezo uliyobandika na jibu langu kwa
SoNotorious.

Naamini utaona mpishano uliokuwapo.
Mapinduzi ya Okello ni mapinduzi ya kuzuka usiku mmoja.

Mapinduzi niliyoeleza mimi kwa kumnukuu Dr. Harith Ghassany ni
mapinduziyaliyopangwa na kuratibiwa na wajuzi wa mipango -
Abdullah Kassim Hanga,Oscar Kambona juu kwenye kinara.

Chini yao kwenye ''Zone of Operation,'' kuna maofisa wa serikali ya
Tanganyika-Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe.

Chini ya hawa kuna Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello.

Hawa ndiyo walikuwa wakiwasiliana na mamluki wa Sakura na
Kipumbwi.

Nadhani hii ''Chain of Command,'' unaiona.
Nani anawajibika kwa nani na kwa kipi.

Mzee Mkwawa anasema hata siku moja Kambona wala si Hanga
walifika kambini Kipumbwi kuzungumza na ''askari.''

Simlazimishi mtu kuamini yale aliyoeleza Dr. Ghassany kwenye
kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' lakini Waswahili
tuna msemo, "Penye ukweli uongo hujitenga.''

Mzee Said anabishana na video mbona Kambona na Hanga hatuwaoni hapo au ilikuwa haramu wao kujitokeza hadharani kuwa walisimamia mapinduzi na si Okello ? The problem the old guy wants to establish islamic connection in erything, hii sio sawa.
 
Mzee Said anabishana na video mbona Kambona na Hanga hatuwaoni hapo au ilikuwa haramu wao kujitokeza hadharani kuwa walisimamia mapinduzi na si Okello ? The problem the old guy wants to establish islamic connection in erything, hii sio sawa.

SoNotorious,
Hili la ''old guy wants to establish islamic connection in erything
(everything), hii sio sawa...''

Jibu la hilo ni dogo na fupi.

Ikiwa wewe una wengine zaidi waliofanya haya ambao si Waislam
tueleze weka taarifa zao hapa JF tutazisoma lakini usinilaumu mimi
kwa kuandika historia za watu ambao mimi nakua katika mitaa ya
Dar es Salaam nawaona na wengine wakiingia hadi majumbani kwa
wazee wetu.

Unauliza kwa nini Kambona na Hanga huwaoni kujitokeza hadharani...
Labda na mimi nikuongozee wengine kidogo ambao hawajajitokeza
hadharani hadi hii leo ingawa wako hai.

Hanga na Kambona wangelijitokeza hadharani kabla au baada ya
mapinduzi ingelijulikana kuwa Zanzibar ilivamiwa na mamluki kutoka
mashamba ya mkonge ya Sakura kwenda kupindua serikali ambayo
ilichaguliwa kihalali.

Isingeishia hapo dunia ingelitaka kujua nani alimtuma Kambona
kufanya yote aliyofanya na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu.

Isingeishia hapo tu dunia ingelijua nani aulizwe kuhusu mauaji yale
yaliyotokea.

Hiki ndicho kilikuwa kitisho kikubwa.

Hii ndiyo sababu wote walikaa kimya pamoja na Victor Mkello,
Ali Mwinyi Tambwe
na Jumanne Abdallah.

Lililowatisha ni kuwa hawakutegemea kiasi kile cha mauaji.

Okello hakuwa chochote.
Okello alikuwa mpiga tarumbeta tu pale Raha Leo.

Viongozi wa mapinduzi na waliopanga mapinduzi yale Dr. Harith
Ghassany
kawaeleza katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru.''

La mwisho.

Utapata tabu sana ikiwa kila unapoona majina ya Waislam katika
historia ya Tanganyika moyo unakuchoma.

Huwezi kuibadili historia hii.

Siku moja nilikuwa nazungungumza na Hamza Aziz basi kidogo
nikamchokoza kuhusu mapinduzi nikamwambia, ''Baba hebu nieleze
ukweli.''

Sikiliza jibu lake:

''Mimi nimekula kiapo cha kutunza siri siwezi kusema kitu ama
sivyo watanifunga. Mimi sasa nina miaka 74...''

Wakati ule wa mapinduzi Hamza Aziz ndiye alikuwa Inspector
General of Police (IGP).
 
SoNotorious,
Hili la ''old guy wants to establish islamic connection in erything
(everything), hii sio sawa...''

Jibu la hilo ni dogo na fupi.

Ikiwa wewe una wengine zaidi waliofanya haya ambao si Waislam
tueleze weka taarifa zao hapa JF tutazisoma lakini usinilaumu mimi
kwa kuandika historia za watu ambao mimi nakua katika mitaa ya
Dar es Salaam nawaona na wengine wakiingia hadi majumbani kwa
wazee wetu.

Unauliza kwa nini Kambona na Hanga huwaoni kujitokeza hadharani...
Labda na mimi nikuongozee wengine kidogo ambao hawajajitokeza
hadharani hadi hii leo ingawa wako hai.

Hanga na Kambona wangelijitokeza hadharani kabla au baada ya
mapinduzi ingelijulikana kuwa Zanzibar ilivamiwa na mamluki kutoka
mashamba ya mkonge ya Sakura kwenda kupindua serikali ambayo
ilichaguliwa kihalali.

Isingeishia hapo dunia ingelitaka kujua nani alimtuma Kambona
kufanya yote aliyofanya na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu.

Isingeishia hapo tu dunia ingelijua nani aulizwe kuhusu mauaji yale
yaliyotokea.

Hiki ndicho kilikuwa kitisho kikubwa.

Hii ndiyo sababu wote walikaa kimya pamoja na Victor Mkello,
Ali Mwinyi Tambwe
na Jumanne Abdallah.

Lililowatisha ni kuwa hawakutegemea kiasi kile cha mauaji.

Okello hakuwa chochote.
Okello alikuwa mpiga tarumbeta tu pale Raha Leo.

Viongozi wa mapinduzi na waliopanga mapinduzi yale Dr. Harith
Ghassany
kawaeleza katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru.''

La mwisho.

Utapata tabu sana ikiwa kila unapoona majina ya Waislam katika
historia ya Tanganyika moyo unakuchoma.

Huwezi kuibadili historia hii.

Siku moja nilikuwa nazungungumza na Hamza Aziz basi kidogo
nikamchokoza kuhusu mapinduzi nikamwambia, ''Baba hebu nieleze
ukweli.''

Sikiliza jibu lake:

''Mimi nimekula kiapo cha kutunza siri siwezi kusema kitu ama
sivyo watanifunga. Mimi sasa nina miaka 74...''

Wakati ule wa mapinduzi Hamza Aziz ndiye alikuwa Inspector
General of Police (IGP).

Duh kumbe Sultan hakuwa mkoloni ? Kama alikuwa mkoloni kwa nini uone aibu na ujifiche kwa kufanya kitendo cha kishujaa cha kumtoa nduki mkoloni na kuwa Zanzibar huru ? Okello alivyojitokeza kama kiongozi wa mapinduzi mbona hakuguswa na mambo waliogopa kina Kambona na Hanga ? Hili la Aziz unamsingizia sijawahi kuona dying citizen at the age of 74 ambae hana cha kupoteza kuogopa jela tena mtu wa imani ambayo usipokuwa suicidal unakuwa assasin disciple.
 
SoNotorious,
Huko nyuma nilishamueleza Okello na nilisema alikuwa mtu mjinga...

Wajanja wote walikaa kimya.

Mtu mwerevu hajigambi katika hali ya mauaji kama yale yaliyotokea
Zanzibar.

Na kama Okello angeliendelea kuishi Zanzibar huenda angeliuliwa kwa
kulipiza kisasi.

Mimi sikulazimishi uniamini hata kidogo ikiwa unapenda kuamini kuwa
Hanga na Kambona sio walopanga mapinduzi au kambi ya Sakura na
Kipumbwi, Tanga haikuwako au mamluki wa Victor Mkello ni ndoto
zangu.

Yote kwangu sawa.

Lakini kaa ukijua pasi na shaka kuwa kuna watu wengi sana wanaamini
ninachowaeleza katika historia ya Tanganyika.
 
SoNotorious,
Huko nyuma nilishamueleza Okello na nilisema alikuwa mtu mjinga...

Wajanja wote walikaa kimya.

Mtu mwerevu hajigambi katika hali ya mauaji kama yale yaliyotokea
Zanzibar.

Na kama Okello angeliendelea kuishi Zanzibar huenda angeliuliwa kwa
kulipiza kisasi.

Mimi sikulazimishi uniamini hata kidogo ikiwa unapenda kuamini kuwa
Hanga na Kambona sio walopanga mapinduzi au kambi ya Sakura na
Kipumbwi, Tanga haikuwako au mamluki wa Victor Mkello ni ndoto
zangu.

Yote kwangu sawa.

Lakini kaa ukijua pasi na shaka kuwa kuna watu wengi sana wanaamini
ninachowaeleza katika historia ya Tanganyika.

Mm mmoja wapo ktk mamilion ya watu tunaokuamini kwa parsent kubwa ya yale unayo tueleza na kukusoma ktk maandishi yako...m/zimungu akupe umri mrefu na afya njema zaidi akuzidishie upeo na ujasiri wa kutoficha ukweli amen.
 
maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni. Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa ,andileni upya..... kwa nini tunawafundisha watoto ...uwongo..
Historia ipi ya nchi hii?si ndio hao maprofeseri waliobadilisha wauza watumwa kuwa mashujaa wetu.Historia hiyo ilindikwa sijui na wamanyema dar.Eti Mkwawa,kinjekitile,Abushir,Mirambo na makundi mengi ya kikabila km wamanyema, wayao etc walivyokuwa active kuuza watumwa na vita zao zilikuwa za kutetea uuzaji huo wa watumwa.Hadi leo Manyema wanajiona kuwa superior na miaka yao yote walijitenga na wabantu wengine kwa kujiona kuwa wao ni masters.Hadi leo hiyo tabia ya kuwapa majina mazuri maharamia ipo ndani ya ccm ..mafisadi,majambazi,wabakaji,wauaji wa wengine kwa risasi hadharani,etc ndio wanaoandika katiba,ndio wanaosimamia tume ,ndio wasafi.Wanaoamsha wengine kuhusu hayo,wanaitwa wazushi,wanaona wivu,wachonganishi na wanaotaka poteza amani yetu.Yote haya yameanzia ktk chuo cha kishetani UDSM chuo cha propaganda na tafiti za kisanii.
 
John Okelo hana historia wala ushujaa wowote - ni mwizi na jambazi ambae alipata fursa ya 'kupindua' serikali ya Zanzibar sababu ya hiana za waingereza tu.
 
Mnara mpya wa Michenzani wa kumbukumbu ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar mwaka 1964 uliogharimu mabilioni ya shilingi ungesherehesha zaidi kama ukapewa heshima ya jina la kiongozi mkuu wa Mapinduzi, Field Marshall John Okello. Mtu aliejitolea hali na mali kuwakomboa waafrika wenzake.

Historia itatuhukumu tukiliacha jina lake kupotea katika kumbukumbu za Mapinduzi ya Zanzibar. Kama Mapinduzi yale yasingelifanikiwa kichwa cha John Okello kingelikuwa cha kwanza kuchinjwa na kuangamizwa.

Nkweli yeye alikuwa si mzanzibari lakini mchango wake hauwezi kubezwa katika ukombozi na Mapinduzi ya Zanzibar.Che Guevara, mwana mapinduzi mwenzake kule Cuba amejengewa mnara wa kumbukumbu, kuthamini mchango wake wakati nae pia alikuwa sio Mcuba.
 
Last edited by a moderator:
Field Marshal John Okello ni "K.a.f.i.r.i" alieitoa Nchi ya Kislamu kutoka utumwani mwa Waislamu wenzao. Wampe haki yake.
 
Ngoja waje, shauri yako...unamzungumzia Yohana Mpambanaji John Okello aliyewasaidia waislamu watoke mikonon mwa utumwa wa waislamu wenzao? Huyu ------ mpambanaji aliyekuwa na upendo wa ajabu kwa watu ambao baada ya mapinduzi waliamua kumchukua na kumfuta kwenye historia yao? Laana hii itawaandama sana na mpaka siku wakija kutubu na kuutambua mchango wa yohana mpambanaji kidume ,jibaba mkombozi wa visiwa vya unguja na pemba.
 
Back
Top Bottom