Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Kwamsaada zaidi>>>> Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungejuwa tusivyolipenda hili swali usingeuliza. Usirudie tena.Kwani walio Pindua walimpindua nani ? ? I
Sasa kama hicho kitabu kinataja waliopigana vita ya maneno halafu hakimtaji yeye aliyeingia vitani physically kuna haja gani ya kukiamini... Kiko biased
Habi Alex,Kitabu kiko biased sana kuna vitabu vingi Vya rejea kukupa ukweli. Wote wanaojifanya wanamapinduzi wanapepeta madomo tu. Mchango wa okelo ni mkubwa
Yericko,Mkuu unachanganya sana, ama kwakujua au kwakutokujua.
Mapinduzi ya Znb haya tunayoyaona leo hayahusiani na hao uliowataja, si nyerere si karume si babu wala nani,
Kulikuwa na makundi matatu yote yakipanga mapinduzi, kundi la kwanza ni la Umma Party chini ya Abdulahman Babu, kundi la pili ni la ASP chini ya Karume akisaidiwa na Julius Nyerere kupitia Kipumbwi kule Tanga, na kundi la tatu ni la Okello na vijana wake (askari wa staafu wa kikoloni)
Kundi lililofanikiwa kufanya mapinduzi ni la Okello, na halikuwa na chama kabisa.
Karume na Nyerere na Babu wakapora mapinduzi hayo yani wakafanya mapinduzi ndani ya mapinduzi lakini bila umwagaji damu.
Ghasany ameandika mengi, lakini ameshindwa kung'amua kwamba kulikuwa na makundi matatu yakifanya mipango ya mapinduzi, na kundi la okello ndilo likafanikiwa.
Yericko,Unadanganya, silaha toka Algeria kwa Ben Bela alizokwenda kuomba Abdulhman Babu zilichelewa Bandari ya Dar, zikafika Znb washamaliza kazi kwakutumia silaha zilezile za Sultan walizoziteka Okello na jeshi lake. Kwaujumla msaada wa ben bela haukuingia Zanzibar.
Ni lazima tu hamna jinsi kazima uandikwe okelo.yeye ndie aliegawa silaha 854 kwa watu wasiojua kutumia silaha ambao hata mtu akiwa amejisalimisha walimuua kinyume na tamko la umoja wa mataifa lilopitishwa kala ya hayo mapinduziBaraghash,
John Okello hakupatapo kuwa ''kiongozi mkuu,'' wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Ukiwa huu ndiyo ukweli hiyo heshima ya jina lake lipewe mnara itakuwa haipo pia.
Ikiwa Okello ndiye ''kiongozi mkuu,'' Abdallah Kassim Hanga atachukua nafasi gani?
Oscar Kambona atapewa heshima gani?
Victor Mkello je?
Au Mohamed Omar Mkwawa nini nafasi zao katika mapinduzi ya Zanzibar?
Vipi kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah.
Vipi kuhusu Wayahudi waliokuwa wakiisaidia Afro-Shirazi Party?
Vipi kuhusu meli ya silaha kutoka Algeria?
Historia ya Mapinduzi ina mengi ambayo wengi hawayajui.
Ukitaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).
Hiki kitabu kipo ''online.''
Kisome uelimike.
Ndani ya kitabu hiki utakutana uso kwa uso na waliopanga mapinduzi na kila
mmoja nini ulikuwa mchango wake.
Okello hayumo katika hiyo orodha.
Inafurahisha sana na kwa hakika nimecheka kidogo ulipomfananisha Che Guevara
na Okello.
Che alikuwa Siera Maestra na Fidel Castro.
Okello hakuweko hata Kipumbwi na Mohamed Omari Mkwawa lilipotokea jeshi la
Wamakonde wakata mkonge kutoka shamba la Sakura walioingia Zanzibar na mapanga
kupindua serikali ya ZNP/ZPPP ya Mohamed Shamte.
Ni lazima tu hamna jinsi kazima uandikwe okelo.yeye ndie aliegawa silaha 854 kwa watu wasiojua kutumia silaha ambao hata mtu akiwa amejisalimisha walimuua kinyume na tamko la umoja wa mataifa lilopitishwa kala ya hayo mapinduzi
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.
Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.
Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]
Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?
Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?
==============
Video ikimwonesha Okello,Karume na Babu masaa machache baada ya Mapinduzi
Phillemon Mikael,http://home.globalfrontiers.com/zanzibar/nine hour revolution.htm
endelea kuangalia hapa chini ,HISTORIA YA MAISHA YA OKELLO,namna alivyopindua na kisha kutimuliwa na karume na baadaye akaishia kwenye mikono ya iddi AMIN.....hiii KALI ZAIDI
en.wikipedia.org/wiki/john_okello
sasa nani anayo historia inayotambulika duniani inayosema tofauti na hii .aweke hapa....
Chakochangu,Waungwana mmoja kati ya wale viongozi wa juu wa iliyokua ASP wakati wa matayarisho hadi mapinduzi yanafanyika si bado yupo hai pale mjimwema mafichoni Mzee ABDUL MWINYI JUMBE . Mtafuteni awapeni undani wake siyo watu mnazunguka humu kutoana macho.
Chakochangu,
Aboud Jumbe hakuwa anajua lolote katika mipango ya mapinduzi.
Haya yako katika kitabu cha Harith Ghassany:
''Amekiri Mzee Jumbe katika kitabu chake The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union: 30 Turbulent Years pale alipoandika kwenye kurasa 9–10 kuwa “ijapokuwa nilikuwa Katibu wa Mipango wa chama cha Afro-Shirazi, sikujuwa vizuri [kuhusu Mapinduzi] asubuhi ya tarehe 12 Januari 1964. Ilikuwa ni siri iliyohifadhiwa vizuri ambayo ilifahamika na uongozi wake [Karume] tu.'' (Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru uk.23).
Field Marshall John Okello.
Hili jitu halitafutika Zanzibar hata iwejee
Huo mnara kama kweli ni wakimapindizi basi angalau waweke Picha ya huyo zaidi ya Komandoo yaani Field Marshal. Itakua wamemtandeha haki japo kiduchu.
Field Marshall John Okello.
Hili jitu halitafutika Zanzibar hata iwejee
Huo mnara kama kweli ni wakimapindizi basi angalau waweke Picha ya huyo zaidi ya Komandoo yaani Field Marshal. Itakua wamemtandeha haki japo kiduchu.
Upewe Jina la Jecha Salim Jecha
Kweli michango ni mingi ila huu sasa utakua ni mnyoo.
Ngoja waje, shauri yako...unamzungumzia Yohana Mpambanaji John Okello aliyewasaidia waislamu watoke mikonon mwa utumwa wa waislamu wenzao? Huyu ------ mpambanaji aliyekuwa na upendo wa ajabu kwa watu ambao baada ya mapinduzi waliamua kumchukua na kumfuta kwenye historia yao? Laana hii itawaandama sana na mpaka siku wakija kutubu na kuutambua mchango wa yohana mpambanaji kidume ,jibaba mkombozi wa visiwa vya unguja na pemba.
weka linkAhsante nimesoma Wikipedia na rejea zake ambamo wamo wasomi maarufu.
Kitu kimoja ambacho nitakufahamisha ni kuwa hao wote hakuna aliyepata bahati
ya kupata nyaraka na kauli ya watendaji wenyewe katika sakata zima la mapinduzi
kama Dr. Harith Ghassany.
Msome Dr. Ghassany utaelewa nini nakueleza.
Ikutoshe tu ni yeye peke yake katika watafiti baada ya zaidi ya miaka 40 ndiye aliyeleta
habari kuwa kulikuwa na askari mamluki kutoka mashamba ya mkonge waliovamia
Zanzibar kuja kupigana upande wa ASP.
Msome Ghassany yapo mengi utajifunza.
Ndumbayeye,weka link