Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...kaka mkubwa nauliza kwa lengo la kujielimisha...kwa nini wazanzibar hawakujitoa kuipigania serikali na zanzibar yao dhidi ya uvamizi ulioratibiwa na kufanywa kwa kutokea nje( na wageni)....linanitatiza kidogo hili ...Baraghash,
John Okello hakupatapo kuwa ''kiongozi mkuu,'' wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Ukiwa huu ndiyo ukweli hiyo heshima ya jina lake lipewe mnara itakuwa haipo pia.
Ikiwa Okello ndiye ''kiongozi mkuu,'' Abdallah Kassim Hanga atachukua nafasi gani?
Oscar Kambona atapewa heshima gani?
Victor Mkello je?
Au Mohamed Omar Mkwawa nini nafasi zao katika mapinduzi ya Zanzibar?
Vipi kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah.
Vipi kuhusu Wayahudi waliokuwa wakiisaidia Afro-Shirazi Party?
Vipi kuhusu meli ya silaha kutoka Algeria?
Historia ya Mapinduzi ina mengi ambayo wengi hawayajui.
Ukitaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).
Hiki kitabu kipo ''online.''
Kisome uelimike.
Ndani ya kitabu hiki utakutana uso kwa uso na waliopanga mapinduzi na kila
mmoja nini ulikuwa mchango wake.
Okello hayumo katika hiyo orodha.
Inafurahisha sana na kwa hakika nimecheka kidogo ulipomfananisha Che Guevara
na Okello.
Che alikuwa Siera Maestra na Fidel Castro.
Okello hakuweko hata Kipumbwi na Mohamed Omari Mkwawa lilipotokea jeshi la
Wamakonde wakata mkonge kutoka shamba la Sakura walioingia Zanzibar na mapanga
kupindua serikali ya ZNP/ZPPP ya Mohamed Shamte.
hiki kitabu nilianza kukisoma nikaishiwa hamu mwanzoni kabisa baada ya kuona mwandishi pamoja na usomi wake anaelezea mchango wa waislam katika uhuru wa tanganyika na analalamika. Sasa uislamu na uhuru wapi na wapi???!!Ndumbayeye,
Link ni hii hapa:Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Harith Ghassany Free pdf download - 1156290 - DocDatabase.net
Nandera,hiki kitabu nilianza kukisoma nikaishiwa hamu mwanzoni kabisa baada ya kuona mwandishi pamoja na usomi wake anaelezea mchango wa waislam katika uhuru wa tanganyika na analalamika. Sasa uislamu na uhuru wapi na wapi???!!
Return......kaka mkubwa nauliza kwa lengo la kujielimisha...kwa nini wazanzibar hawakujitoa kuipigania serikali na zanzibar yao dhidi ya uvamizi ulioratibiwa na kufanywa kwa kutokea nje( na wageni)....linanitatiza kidogo hili ...
sio kwamba sipendi kusoma kitu kinachohusiana na uislam. Hata mwandishi angehusianisha harakati za uhuru na ukristo ningekihukumu. kwangu mimi kusema waislam walihusika sana na uhuru ni sawa na kusema "harakati za waislam katika kutibu magonjwa ya akili" kwa sababu bingwa wa magonjwa ya akili - dr. ayoub ni mwislamu. sipendi udini dini maana unanipa hisia flani za kibaguzi.Nandera,
Bahati mbaya sana kuwa hupendi kusoma kitu kinachohusiana na Uislam.
Historia ya Uislam katika uhuru wa Tanganyika ni somo muhimu sana na
ikiwa utautoa mchango wa Waislam katika historia hiyo hutokuwa na historia
ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Unauliza historia ya Uislam na uhuru wapi na wapi?
Jikaze uisome ndipo uweze kusema chochote kuhusu hilo.
Yapo mengi huyajui katika historia hiyo na ikiwa huyajui ndiyo utabaki kuwa
hujui na ujinga si sifa nzuri.
Uongo kwa maisha ya sasa ndio unaopendwa kuliko ukweli. Jaribu kwenda kumtongoza mwanamke kwa maneno ya kweli kama utampata. Au jaribu kwenda kuomba kazi na vyeti vya ukweli kama utapata na elimu ya darasa la saba. Na mwisho hebu andika mada ya ukweli juu ya serikali kama itakaa hapa kwenye jukwaa bila ya kufutwa. kwasababu ukweli unauma(unachoma ndipo).maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.
Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa ,andileni upya.....
kwa nini tunawafundisha watoto ...uwongo..
Nandera,sio kwamba sipendi kusoma kitu kinachohusiana na uislam. Hata mwandishi angehusianisha harakati za uhuru na ukristo ningekihukumu. kwangu mimi kusema waislam walihusika sana na uhuru ni sawa na kusema "harakati za waislam katika kutibu magonjwa ya akili" kwa sababu bingwa wa magonjwa ya akili - dr. ayoub ni mwislamu. sipendi udini dini maana unanipa hisia flani za kibaguzi.
Inasikitisha kuwa mwana historiakana wewe kuwa huwamini kuwa John Okello hakuwahi kuwa kiongozi wa Mapinduzi. Mimi kwa hili sihitaji kusoma kitabu chochote. Nimeona na nimesikiliza matangao yakeSoma hapa kidogo
John Okello - Wikipedia, the free encyclopedia
Baraghash,Inasikitisha kuwa mwana historiakana wewe kuwa huwamini kuwa John Okello hakuwahi kuwa kiongozi wa Mapinduzi. Mimi kwa hili sihitaji kusoma kitabu chochote. Nimeona na nimesikiliza matangao yake
1. labda nikukumbushe, tangazo la kwanza kutoka kwenye redio (sauti ya Zanzibar ni Okello kujitambulisha
2. Tangazo la pili alilitoaAli Muhsin, kiongozi wa Hizbu (ZNP) kuwataka wafuasi wake wautii utawala mpya na kuwataka wajisalimishe
3. Okello akimtaka Karume popote al;ipo ajitokeze kuja kuchukua uongozi wa nchi
Awali mwezi wa kwanza wa Mapinduzi Karume ndio alikuwa kiongozi mkuu wa baraza la Mapinduzi na Okello akiwa naibu wake. Baada ya muda mchache na baaada ya kuonekana kama kuyumba uongozi wa Karume katika baadhi ya maamuzi, Okello akamfuta kazi Karume na kumuweka naibu wake na hivyo akachukua hatamu ya uongozi wa baraza la mapinduzi. UOngozi wake ulidumu mpaka pale alipofanyiwa hila na akina Babu na Nyerere kwenda dar kwenye kikao na huko ukawa mwisho wake. Hakurudi tena Zanzibar.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. OKELLO HAKI YAKE APEWE
Baraghash,
Mapinduzi yanataka mipango na hao wanaopanga mipango humo ndipo wanapotoka viongozi.
Hakuna ushahidi katika historia ya Mapinduzi Zanzibar kuwa Okello alikuwa na kamati au kitu
kingine chochote unachoweza kukiita kamati au nini kuwa Okello alikuwa anaongoza katika hiyo
mipango ya mapinduzi.
Baada ya miaka 40 ndipo Dr. Ghassany akaja na kitu ambacho hakikuwa kinafahamika katika hii
historia ya mapinduzi.
Dr. Ghassany akaeleza kuwa mipango ya mapinduzi pamoja na fedha za kukamilisha hayo mapinduzi
ilikuwa Bara na kiongozi mkuu alikuwa Oscar Kambona kwa upande wa Tangayika na Abdallah
Kassim Hanga kwa upande wa Zanzibar.
Wengine waliohusika katika mpango huu alikuwa Ali Mwinyi Tambwe, Victor Mkello, Jumanne
Abdallah na Mohamed Omari Mkwawa.
Hayo mengine ulosema kuhusu Okello na hotuba zake na mengine ni katika vituko vyake ambavyo kwa
hakika ni vichekesho kama vile alivyokuwa akiamini kuwa yeye ni ''Field Marshall.''
Nilikuwa nikuzungumza kuhusu Okello na Badawy Qullatein yeye alikuwa kila akimtaja Okello anacheka.
Naamini ushajua kwa nini Qullatein alikuwa akimuona Okello ni kichekesho.
Okello hakupata kufika Kipumbwi walikotoka wapiganaji wa mapinduzi wala hakuwa anajua kuwa huko
Sakura kulikuwa na kambi ya mamluki.
Itoshe tu hiki ni kioja kuwa Okello awe kiongozi wa mapinduzi lakini awe hajui Karume yuko wapi na
kumpata amtafute kupitia kwenye radio.
Yako mengi sana katika vichekesho vya Okello.
In Sha Allah taratibu tutaelezana.

Chizi Maarifa,Karume alikimbia kujificha kipindi akina okello wanafanya Mapinduzi. Jaman kwa nini tunamchukia hivi JOHN OKELLO? Mtu ambaye tulipaswa sana kumshukuru ingawa kama binadamu alikuwa na mapungufu yake. hatujiulizi kwa nini huyu ndo alikuwa na mamlaka ya kutangaza mapinduzi? yaani wapindue akina karume ahlafu okello awe mzungumzaji kwenye radio? mbona hii haiingi akilini hata kidogo?
mambo mengine tunajidhalilisha tu. OKELLO NDO ALIYEIOKOA ZANZIBAR KUTOKA KWA WANYONYAJI, WAKANDAMIZAJI, WAHUNI NA AGENTS WA SHETANI. HATIMAYE IKAWA HURU CHINI YA MWAFRIKA MPAKA LEO TUNALINDA MAPINDUZI HAYA MWARABU ASIRUDI ZANZIBAR.
Baraghash,[
Pole ndugu yangu! unakichukulia kitabu cha Ghasany kama Quraan. Kitabu hicho kiliegemea upande mmoja tu na hukutaka upande wa pili unasemaje. Kwa kukusaidia soma kitabu kiitwacho Zanzibar revolution and its aftermath, kilichoandikwa na Kamishna mzungu wa Magereza wa wakati huo, kitakueleza vipi Karume alivyokimbia Mapinduzi nakujificha na ukweli alikuwa alishakwenda kwa Kamishna wa Polisi wa kizungu kumjuulisha kuwa kuna watu wanataka kufanya fujo tarehe 12 Januari 1964 na yeye hahusiki.
Kuhusu mazungumzo na Qulatein inawezekana kwa sababu kwanza yeye alikuwa chama cha Umma party cha Babu waliotaka kuyateka nyara Mapinduzi kwa kuwatumia vijana ambao ndio kwanza wamerejea kutoka Cuba walikopata mafunzo ya kijeshi. Ni kweli kwa wao Okello ni kichekesho lakini aliwawahi. Kwa sababu hata hao akina Qultein walikuwa na azma ya kupindua
Lakini kubwa zaidi ni bado viongozi wa mapinduzi waliokuwa kwenye kamati ya watu 14 wengine bado wako hai. Kama vile, Waziri kiongozi mstaafu, Ramadhan Haji Faki , mzee Hamid Ameir.
Sisi tuliokuwepo Zanzibar wakati wa mapinduzi tunajua kuwa mkuu wa nchi wakati huo alikua Okello na ndio akipita barabrani tulikuwa tunalazimika kuonesha vidole viwili V!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. OKELLO HAKI YAKE APEWE
Kwani reference lazima iwe kitabu kimoja tu? Hata biblia ina vitabu kadhaa ambavyo ukisoma kimoja kimoja au mstari mmoja mmoja pekee, unaweza either usielewe vyema au ukapata maudhui yasiyokusudiwa, na ndio maana vitabu vyote vinaleta maudhui ya ujumla...
Ukitaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).
...
Sijamaliza kusoma michango yote ya jumamosi na jumapili lakini huyu okello hakujikuta zanzibar kibahati bali nae alitumiwa na wamagharibi kama nyerere na karume walivyotumika. mapinduzi hayakuwa wazo la wazanzibari kama ambavyo muungano haukuwa wazo la nyerere wala karume. lilikuwa wazo la "wakubwa", kwa hiyo binafsi sioni kwa nini okello au karume wasifiwe kwa kuchinja maelfu ya waarabu. Na huko juu ametajwa oscar kambona kama mtu aliyekuwa akisimamia hiyo kazi kifedha. Ni kambona huyu huyu alitimulia ughaibuni baada ya mpango wake na c.i.a wa kuwatumia wapiganaji wa a.n.c waliokuwa mazimbu kumpindua nyerere kushtukiwa. Na nadhani ni kutokana na uhusika wa magharibi kwenye "mapinduzi" ndo ulifanya mauaji hayo makubwa yasijulikane sana mpaka leo. Wazanzibari na wazanzibara tutatoana tu macho lakini mhandisi asiye m-bara wala m-bari amekaa pembeni anachora mipango. Tuendelee kuangalia sinema ya uchaguzi zanzibar.Inasikitisha kuwa mwana historiakana wewe kuwa huwamini kuwa John Okello hakuwahi kuwa kiongozi wa Mapinduzi. Mimi kwa hili sihitaji kusoma kitabu chochote. Nimeona na nimesikiliza matangao yake
1. labda nikukumbushe, tangazo la kwanza kutoka kwenye redio (sauti ya Zanzibar ni Okello kujitambulisha
2. Tangazo la pili alilitoaAli Muhsin, kiongozi wa Hizbu (ZNP) kuwataka wafuasi wake wautii utawala mpya na kuwataka wajisalimishe
3. Okello akimtaka Karume popote al;ipo ajitokeze kuja kuchukua uongozi wa nchi
Awali mwezi wa kwanza wa Mapinduzi Karume ndio alikuwa kiongozi mkuu wa baraza la Mapinduzi na Okello akiwa naibu wake. Baada ya muda mchache na baaada ya kuonekana kama kuyumba uongozi wa Karume katika baadhi ya maamuzi, Okello akamfuta kazi Karume na kumuweka naibu wake na hivyo akachukua hatamu ya uongozi wa baraza la mapinduzi. UOngozi wake ulidumu mpaka pale alipofanyiwa hila na akina Babu na Nyerere kwenda dar kwenye kikao na huko ukawa mwisho wake. Hakurudi tena Zanzibar.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. OKELLO HAKI YAKE APEWE
Kapwila Matulu,Kwani reference lazima iwe kitabu kimoja tu? Hata biblia ina vitabu kadhaa ambavyo ukisoma kimoja kimoja au mstari mmoja mmoja pekee, unaweza either usielewe vyema au ukapata maudhui yasiyokusudiwa, na ndio maana vitabu vyote vinaleta maudhui ya ujumla
Mbandeon,Hicho kitabu cha kwaheri ukoloni kwa heri uhuru, nadhani utakuwa unashare yako Sheikh sio bure. yaani kama kipofu aliyeona punda .
Yapinge kwa maandiko japo ya kukopi na kupesti ili uone #kazi yake.Hicho kitabu cha kwaheri ukoloni kwa heri uhuru, nadhani utakuwa unashare yako Sheikh sio bure. yaani kama kipofu aliyeona punda .