Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Baraghash,
John Okello hakupatapo kuwa ''kiongozi mkuu,'' wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Ukiwa huu ndiyo ukweli hiyo heshima ya jina lake lipewe mnara itakuwa haipo pia.

Ikiwa Okello ndiye ''kiongozi mkuu,'' Abdallah Kassim Hanga atachukua nafasi gani?
Oscar Kambona atapewa heshima gani?

Victor Mkello je?
Au Mohamed Omar Mkwawa nini nafasi zao katika mapinduzi ya Zanzibar?

Vipi kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah.
Vipi kuhusu Wayahudi waliokuwa wakiisaidia Afro-Shirazi Party?

Vipi kuhusu meli ya silaha kutoka Algeria?
Historia ya Mapinduzi ina mengi ambayo wengi hawayajui.

Ukitaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).

Hiki kitabu kipo ''online.''
Kisome uelimike.

Ndani ya kitabu hiki utakutana uso kwa uso na waliopanga mapinduzi na kila
mmoja nini ulikuwa mchango wake.

Okello hayumo katika hiyo orodha.

Inafurahisha sana na kwa hakika nimecheka kidogo ulipomfananisha Che Guevara
na Okello.

Che alikuwa Siera Maestra na Fidel Castro.

Okello hakuweko hata Kipumbwi na Mohamed Omari Mkwawa lilipotokea jeshi la
Wamakonde wakata mkonge kutoka shamba la Sakura walioingia Zanzibar na mapanga
kupindua serikali ya ZNP/ZPPP ya Mohamed Shamte.
mchango wa okello hapa una changanya kuna victor mkello na huyu okello raia wa uganda ,mchango wa victor mkello aliyekuwa katibu mkuu wa vyama vya wafayakazi mashambani ni mkubwa ukiilinganisha na huyu mganda okello jukumu lake lilikuwa ni kutangaza na walimpa nafasi hiyo kutokana na kuwa na sauti nzito ,kimsingi anayetakiwa kuenziwa hapa ni victor mkello huyu mbondei wa muheza kwa mchango wake katika mapinduzi ya zanzibar.rejea simulizi kutoka katika kitabu cha kwaheri uhuru karibu ukoloni cha Dr harith ghassan
 
1453839390575.jpg
 
Sijui kwanini waliamua kutuficha!!!!

Niliwahi kusikia kuwa kuna kitabu kiliandikwa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na muhusika mkuu alikuwa John Okelo ila eti kilifichwa,sijui ukweli wake zaidi
 
Sijui kwanini waliamua kutuficha!!!!

Niliwahi kusikia kuwa kuna kitabu kiliandikwa kuhusu mapinduzi ya Zanzibar na muhusika mkuu alikuwa John Okelo ila eti kilifichwa,sijui ukweli wake zaidi


Ukweli ni kwamba huyu jamaa ni katika wachache sana duniani ambao wameongoza mapambano ya kuipindua serikali halafu akaachwa hai.
 
huyu ni "che guavara" wa afrika, sio hawa maboya wenu wanaocheka cheka tu!
 
Ukweli ni kwamba huyu jamaa ni katika wachache sana duniani ambao wameongoza mapambano ya kuipindua serikali halafu akaachwa hai.

walikuwepo akina Samuel wakaleta taabu na yule jamaa mwingine wa Misri ambae alizuiwa kambini.
wanasiasa huwa na wasiwasi kuwa wakiachwa huwa wanaona ile nchi waliyoikomboa ni mali yao na kuanza kujenga kibri
 
Siku ya mapinduzi inasemekana Karume alikuwa kajificha Dar wakati mashujaa wasioimbwa wakipambana.
 
Back
Top Bottom