Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

C15J-xiWQAAHPhF.jpg

“UNGUJA iliipindua Serikali ya Sultani kibaraka, kwa marungu mama, kwa mapanga mama, mwisho wake wakafaulu.”

Kwenye miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa ni rahisi kusikia nyimbo za kumbukizi la Mapinduzi ya Zanzibar ambayo leo Januari 12, yanatimiza miaka 53.

Mapinduzi hayo ambayo yalijumuisha mambo mengi baadhi yakiwa kwenye kumbukumbu rasmi za kihistoria lakini baadhi yamekuwa yanawekwa pembezoni na hivyo uelewa juu yake kuwa wa juu juu.

Miongoni mwa mambo hayo ni kukosekana kutajwa au kukumbukwa kwa mshiriki mmojawapo kwenye Mapinduzi hayo hali inayoonesha kugubikwa na mwangwi wa kibaguzi ndani ya kumbukumbu za tukio hilo muhimu ambalo limekuwa linaelezwa kuwa ndio chimbuko la kuondoa utumwa na utwana.

Ambaye anaonekana kuwekwa pembeni ni Field Marshal John Okello ambaye kwenye kumbukumbu za kihistoria inaelezwa kuwa aliingia Zanzibar mwaka 1963 na kuwa na mawasiliano na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP).

Vijana hao wa ASP inaelezwa kuwa wakiwa wanapanga mbinu za kuuondoa utawala wa Waarabu, Okello kwa upande wake akiwa mwanachama wa chama cha wapiga rangi – akiwa anapaka rangi majumba mbalimbali, katika muda wake wa ziada aliunda kikundi kidogo cha askari wa Kiafrika.

Kikundi hiki cha kijeshi kilishika na kufuata amri alizozitoa Okello kama kiongozi ambazo ni pamoja na kutojihusisha na masuala ya ngono, kutokula nyama mbichi na kutokunywa pombe.

Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini na aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto ili aweze kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha Serikali ya Mapinduzi ya Unguja na Pemba.

Hali kadhalika inaelezwa kuwa usiku mmoja kabla ya Mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.

Januari 12, 1964 inaelezwa Okello na kikosi chake waliingia Mji Mkongwe, Zanzibar, maskani ya Sultani, lakini Sultani mwenyewe alikuwa ameshakimbilia mafichoni nchini Uingereza.

Hata hivyo baada ya kufanikiwa kwa Mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa Waziri Mkuu. Baadaye alikuwa Makamu wa Rais.

Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu Mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.

Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.

Hatimaye inaelezwa kuwa alirudi kwao mara ya mwisho alionekana akiwa na kiongozi wa Uganda Idd Amin Dada mwaka 1971 na baadaye alipotea.

Katika kitabu cha ‘Revolution on Zanzibar’ kilichoandikwa na Don Petterson inadhaniwa kuwa Idd Amin alimwona Okello kuwa ni tishio kwake na mara nyingine inaelezwa kuwa baada ya Amin kujipandisha cheo na kuwa Filed Marshal, inaelezwa kuwa Okello alisema kwa dhihaka, “Uganda hivi sasa ina Field Marshal wawili.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Idd Amini alipanga mipango ya mauaji dhidi ya Okello, lakini pamoja na hali hiyo kifo chake kimebakia kuwa ni cha utata.

Wapo waliofanya mambo yanayofanana na Okello. Mfano Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye Mapinduzi ya Cuba akiwa ni raia wa Argentina.

Wapo wanaomuona Okello kuwa ni kama askari wa kukodiwa na siku zote askari wa aina hiyo wakimaliza kazi waliyolipwa kufanya huondoshwa haraka.

Yanaweza kuwapo mawazo mengi kinzani kuhusu Mapinduzi lakini yalikuwa muhimu ili kuleta uwiano wa maendeleo kwa jamii ya Zanzibar ndio maana siku zote kauli mbiu mama imekuwa “Mapinduzi Daima.”
 
Juzi nimemsikia Balozi Karume akimtaja Okello kama alikuwa kiongozi wao wa mapinduzi......ila akamtetea mzee Karume kuwa aliondoka Zbar usiku wa mapinduzi kuja dar kuhakikisha watoto wake wamefika salama na wanaenda shule kesho yake......na yeye alirudi zbar j3 yaani siku 1 baada ya mapinduzi......!!!
 
kuna nini hpo sasa
 
ASITAKE KUDANGANYA WATU, WATOTO WAKE KWENDA SHULE HIKI NI KICHEKESHO!!

KARUME MWENYEWE NDIYE ALIMUOMBA NYERERE AMUONDOE OKELLO ZANZIBAR, NAFIKIRI OKELLO NA KARUME HAWAKUELEWANA KISWAHILI NASIKIA KUNA WAKATI OKELLO ALINTOKEA MANENO MAKALI KARUME, MZEE WA WATU AKAMSHTUKIA NA KUOMBA MSAADA KWA NYERERE, KAMBARAGE ALITUMIA MBINU YA HALI YA JUU KUMZUGA OKELLO MPAKA AKAINGIA KINGI AKASAFIRI KUJA DAR KUFIKA TU KATIWA MBARONI KASAFIRISHA KUPITIA KENYA KWENDA UGANDA, NYERERE ALIMUOMBA MZEE KENYATTA KWAMBA OKELLO HASIRUHUSIWE KUISHI KENYA, KENYATTA ALIJUBALI OMBI LA KAMBARAGE.
 
View attachment 458696
“UNGUJA iliipindua Serikali ya Sultani kibaraka, kwa marungu mama, kwa mapanga mama, mwisho wake wakafaulu.”

Kwenye miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa ni rahisi kusikia nyimbo za kumbukizi la Mapinduzi ya Zanzibar ambayo leo Januari 12, yanatimiza miaka 53.

Mapinduzi hayo ambayo yalijumuisha mambo mengi baadhi yakiwa kwenye kumbukumbu rasmi za kihistoria lakini baadhi yamekuwa yanawekwa pembezoni na hivyo uelewa juu yake kuwa wa juu juu.

Miongoni mwa mambo hayo ni kukosekana kutajwa au kukumbukwa kwa mshiriki mmojawapo kwenye Mapinduzi hayo hali inayoonesha kugubikwa na mwangwi wa kibaguzi ndani ya kumbukumbu za tukio hilo muhimu ambalo limekuwa linaelezwa kuwa ndio chimbuko la kuondoa utumwa na utwana.

Ambaye anaonekana kuwekwa pembeni ni Field Marshal John Okello ambaye kwenye kumbukumbu za kihistoria inaelezwa kuwa aliingia Zanzibar mwaka 1963 na kuwa na mawasiliano na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP).

Vijana hao wa ASP inaelezwa kuwa wakiwa wanapanga mbinu za kuuondoa utawala wa Waarabu, Okello kwa upande wake akiwa mwanachama wa chama cha wapiga rangi – akiwa anapaka rangi majumba mbalimbali, katika muda wake wa ziada aliunda kikundi kidogo cha askari wa Kiafrika.

Kikundi hiki cha kijeshi kilishika na kufuata amri alizozitoa Okello kama kiongozi ambazo ni pamoja na kutojihusisha na masuala ya ngono, kutokula nyama mbichi na kutokunywa pombe.

Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini na aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto ili aweze kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha Serikali ya Mapinduzi ya Unguja na Pemba.

Hali kadhalika inaelezwa kuwa usiku mmoja kabla ya Mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.

Januari 12, 1964 inaelezwa Okello na kikosi chake waliingia Mji Mkongwe, Zanzibar, maskani ya Sultani, lakini Sultani mwenyewe alikuwa ameshakimbilia mafichoni nchini Uingereza.

Hata hivyo baada ya kufanikiwa kwa Mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa Waziri Mkuu. Baadaye alikuwa Makamu wa Rais.

Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu Mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.

Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.

Hatimaye inaelezwa kuwa alirudi kwao mara ya mwisho alionekana akiwa na kiongozi wa Uganda Idd Amin Dada mwaka 1971 na baadaye alipotea.

Katika kitabu cha ‘Revolution on Zanzibar’ kilichoandikwa na Don Petterson inadhaniwa kuwa Idd Amin alimwona Okello kuwa ni tishio kwake na mara nyingine inaelezwa kuwa baada ya Amin kujipandisha cheo na kuwa Filed Marshal, inaelezwa kuwa Okello alisema kwa dhihaka, “Uganda hivi sasa ina Field Marshal wawili.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Idd Amini alipanga mipango ya mauaji dhidi ya Okello, lakini pamoja na hali hiyo kifo chake kimebakia kuwa ni cha utata.

Wapo waliofanya mambo yanayofanana na Okello. Mfano Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye Mapinduzi ya Cuba akiwa ni raia wa Argentina.

Wapo wanaomuona Okello kuwa ni kama askari wa kukodiwa na siku zote askari wa aina hiyo wakimaliza kazi waliyolipwa kufanya huondoshwa haraka.

Yanaweza kuwapo mawazo mengi kinzani kuhusu Mapinduzi lakini yalikuwa muhimu ili kuleta uwiano wa maendeleo kwa jamii ya Zanzibar ndio maana siku zote kauli mbiu mama imekuwa “Mapinduzi Daima.”
Marekebisho kidogo, Okello aliingia Zenji mwaka 1954 sio 1963. Ni kweli kwamba ni yeye ndiye alikua mhusika mkuu wa mapinduzi na yeye ndiye alimpandisha boti Karume aje bara usiku wa mapinduzi. Baada ya mapinduzi alibaki kama kiongozi wa kijeshi wakati Karume akiwa kiongozi wa kivita. Miaka ya 1960's wakati akipanda ndege kuelekea Zenji kutokea bara maofisa usalama walimpakia ndege ya kwenda Kenya. Inadaiwa kulikua kuna hofu kwamba huenda akapindua tena nchi pia hakua pia akisapoti sana muungano
 
Habari wakuuu naomba kujua kwa mwenye kujua historia ya john okello aliyeongoza mapindunzi huko Zanzibar! Ikiwa Leo wazanzibari wanafurahia miaka 53 ya mapindunzi je " field Marshall OKELLO anakumbukwa vipi? Na baada ya mapindunzi aliishi wapi au alienda wapi?
 
Naunga mkono hoja, tuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuenzi matokeo chanya ya Mapinduzi hayo ambao ni Muungano wetu adhimu ulituzalishia taifa moja tuu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kule Zanzibar wao wana msemo wao was
Mapinduzi Daima
Na sisi Watanzania katika umoja wetu tunasema kwa kauli moja
Tutaulinda Muungano kwa gharama yoyote, na hata kama gharama yenyewe ni kutengua demokrasia kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi wa Zanzibar, for the sake of union, demokrasia na itenguliwe! .

Nawatakia mapumziko mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Wewe si Mzanzibar unayaenzi Mapinduzi kwani ni ya kazi gani kwako????

Wewe kapiganie debe la mahindi literemke bei kutoka shilingi 90 000 walau lifike 50 000

Lakini LAZIMA utasema hivi kwani ndio malengo ya kanisa lako la kikatoliki hayo.
 
Tukiifuatilia historia ya maisha yake na harakati zake, tunapata uhalisia ya kuwa John Okello ni moja ya watanzania wanaostahili kutangazwa Watakatifu. Nje ya mapambano.

Afande JOHN OKELLO

Ndio alikuwa DAUDI wa Zanzibar kwa kumuangusha Goliati(Utawala wa kisultan). Okello angetakiwa kupewa cheo kikubwa sana wakati ule kwa mjibu wa kujitolea kuirudisha Zanzibar. Zanzibar ilipashwa kumpa Heshima kubwa sana kipindi hiki Hayati John Okello. Kwangu Mimi Okello ni MTAKATIFU wa kwanza kutoka Tanzania aliyeifia Inchi yake na akatelekezwa.

Kipindi hiki tusiige mfumo wa kipindi kile Bali tuwe tuna wasapoti wale waliotusaidia kuleta chanzo cha mabadiliko.

Deogratius Kisandu.
 
Hakuna binadamu aliye mkamilifu
Hizo ni divination
 
wew jamaa kwanza Okello hakuwa mtanzania na wala Tanzania haikuwa nchi yake kama ulivosema...

Hivi huo utaratibu wa kanisa lenu kuwapa utakatifu binadamu wanaostahili kuomba toba kila saa huwa mnazingatia nini?
 
Mna hicho kifaa cha saintmeter mpaka mumtunikie UTAKATIFU? Mnajua maisha yake ya sirini?

Achen kuchukua nafasi ya Mungu
 
Tukiifuatilia historia ya maisha yake na harakati zake, tunapata uhalisia ya kuwa John Okello ni moja ya watanzania wanaostahili kutangazwa Watakatifu. Nje ya mapambano.

Afande JOHN OKELLO

Ndio alikuwa DAUDI wa Zanzibar kwa kumuangusha Goliati(Utawala wa kisultan). Okello angetakiwa kupewa cheo kikubwa sana wakati ule kwa mjibu wa kujitolea kuirudisha Zanzibar. Zanzibar ilipashwa kumpa Heshima kubwa sana kipindi hiki Hayati John Okello. Kwangu Mimi Okello ni MTAKATIFU wa kwanza kutoka Tanzania aliyeifia Inchi yake na akatelekezwa.

Kipindi hiki tusiige mfumo wa kipindi kile Bali tuwe tuna wasapoti wale waliotusaidia kuleta chanzo cha mabadiliko.

Deogratius Kisandu.
mie nikadhani umeweka hapa na picha yake ili tumjue japo hata kwa sura? weka hiyo picha
 
Nimeona mtu anaitwa Mohamed Shamte Hamad ambaye alikuwa waziri mkuu je na yule anayeitwa AbdulJamshid alikuwa ni nani? Pia ni nani alikimbilia uingereza baada ya mapinduzi? Msaada tafazali.
 
Back
Top Bottom