Mapungufu niliyoyaona mechi ya jana Tanzania VS Sudan

Mapungufu niliyoyaona mechi ya jana Tanzania VS Sudan

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kwanza niwape pole wachezaji na Watanzania wote kwa ujumla kwa matokea ya kuumiza kidogo ambayo hatukuyatarajia japo mimi binafisi nilishaona tulichemsha mwanzo kabsa baada ya kuona timu ilitoitwa ikiwa na Striker mmoja. Baadhi walipingana na mtazamo wangu. km mnavyojua tena kuna tofauti kati ya shabiki na mpenzi wa mpira. Kuna mtu akishaona wachezaji anaowapenda wameitwa baaasi atakwambia timu imekamilika. Kwa mtazamo wangu Kamgomoli hizi ndio sababu za msingi zilizoighalimu timu yetu.
1.Timu ilikosa striker muuwaji( Terminator). Chilunda anahitaji kuendelea kujifunza. Ni striker mzuri lakn anakosa uzoefu na match Fitnes.
2. Wachezaji wetu bado hawezi kucheza OBJECTIVE FOOTBAL. Bado wachezaji wetu hawana uwezo wa kumsoma mpinzani wawapo uwanjani. Kubadili mbinu kulingana na vipindi vya dk 15 za mwanzo 30, au 15 za mwisho n.k . Huwezi cheza stail moja tu mwanzo mwisho kwa timu ngumu km Sudan. Kwenye Objective football mchezaji anatambua afanye nn katika eneo gani. Wachezaji wetu wanacheza vzr sn kuanzia nyuma mpaka eneo la katikati. Wanavyozidi kukaribia eneo la 18 mbinu ni km zinawaishia. Sehemu ya kutoa pasi atabutua jishutu na kinyume chake. Mtu anatakiwa aingie nayo zaidi ndani ya 18 au 6 anapiga cross au kutoa basi butu bila hata kuangalia wenzake wako wapi na wamejipanga vp mwishowe mpira unapotea kirahisi kabsa. Kwenye Objective footbal nafasi 2 moja goli. Sasa sisi nafasi 10 hadi 15 utakuta hakuna goli hata moja.
3. Timu ya taifa kwa sasa haina beki mzuri wa pembeni kulia ukimuondoa Shomari ambaye roho yake kwasasa haipo timu ya taifa kutokana na kutelekezwa na TFF baada ya kuumia na Simba wakabeba jukumu la kuhangaika nae hadi akapona. Huo ndio ukweli japo ni mchungu kuongea.
Bonifasi Maganga licha ya mapungufu yake mengi anatatizo kubwa la msingi km beki wa pembeni, kwanza hana speed,pili hawezi kupiga cross kabsa. Jana kapiga cross nje zaidi ya mipira 4 bila kubughudhiwa na mtu. Sielewi ni sifa ipi inayofanya Ndailagije aendelee kumuita timu ya taifa kwangu ni beki wa kawaida sn.
4.Kukosa umakini kwa Idi Nado. Idi ni mchezaji mzuri ila tatizo lake kubwa na ambalo sjui km kocha amewahi kumwambia ni kukosa utulivu. Papara nyingi mno!! Ni mchezaji mwenye juhudi sn akiwa uwanjani tatizo lake kubwa hana utulivu. Anapata chances nyingi sn lakni mipira mingi anapiga nje!
5. Km taifa lazma tutafte washambuliaji wenye maumbo ya kina Mwaikimba. Baada ya Afcon kupita yalisemwa mengi sn kuhusiana maumbo ya wachezaji wetu. Jana tuliwaona Wasudani jinsi walivyo warefu.Mipira mingi wa juu waliicheza wao. Scouting ya nguvu inatakiwa ili kuwapata wachezaji wa maumbo makubwa ili tuweze kupambana na adui wa kila aina la sivyo tutaishia kusema tumeupigwa mwingi huku tumepoteza mechi.
 
Asante mkuu.
Mi niliumia sana kupoteza mechi wakati kipindi cha kwanza tulitawala game. Mbele hakuna muunganiko kabisa.

Lkn kilichoniuma zaidi ni kuipoteza jero yangu kwenye banda umiza.
 
Hahaha shida ni moja tuu....tukamuombe mwinyi atengue kauli yake ya kichwa cha mwendawazimu kabla hajafa.
 
Timu haijui inataka nini, wanachowaza wao ni kucheza na ‘Jukwaa’ tu.

Nado ni mchezaji ‘Machachari’ lakini si Mchezaji ‘Hatari’ na mara nyingi hyo inasababishwa na kukosa uzoefu ukijulimshwa kutofundishwa mbinu za mpira wakiwa katika umri sahihi.

Kwa Chilunda dah,jamaa anatuangusha kabisa kabisa. Anatumia muda mwingi kucheza nje ya kisanduku cha adui na ni moja ya kitu kilichosababisha tupoteze nafasi nyingi.

Yote kwa yote kama tunahitaji kuwa na timu nzuri hatuna budi kumvumilia mwalimu afanye kile alichojaaliwa.

Lazima tukubali uwezo wetu wa kimpira upo chini na tusitegemee matokeo mazuri kwa ghafla ghafla tu.
 
Sehemu ya mtu kuruka kwa kupiga mpira kichwa anashindwa eti anakaa kuusuburia mpira autulize na mguu kisha ndio atowe pasi. Sa sijui ndio ufupi?

Hili ndio tatizo lengine...makocha wapo wengi hii tz hahabaha.
 
Mtoa mada, namba 2 na 3 umeeleza vizuri sana, namba 1 tatizo liko palepale, hatuna mshambuliaji wa asili yule namba 9 wa kizamani, nikikuambia uwataje wengine hutaona aliye juu ya Chilunda kiuwezo, ki exposure na kiuzoefu, yupo mmoja tu John Boko ambae anaumwa, tunaposikia mfungaji bora ni Kagere au mchezaji toka nje hili si jambo LA kufurahia athari zake ndio hizi, tunatakiwa tuanze kuwa jicho LA kitafiti wakijitokeza washambuliaji chipukizi tuwasafishie njia kwa Kuwaita mapema na kuwapa uzoefu mapema
 
Mtoa mada, namba 2 na 3 umeeleza vizuri sana, namba 1 tatizo liko palepale, hatuna mshambuliaji wa asili yule namba 9 wa kizamani, nikikuambia uwataje wengine hutaona aliye juu ya Chilunda kiuwezo, ki exposure na kiuzoefu, yupo mmoja tu John Boko ambae anaumwa, tunaposikia mfungaji bora ni Kagere au mchezaji toka nje hili si jambo LA kufurahia athari zake ndio hizi, tunatakiwa tuanze kuwa jicho LA kitafiti wakijitokeza washambuliaji chipukizi tuwasafishie njia kwa Kuwaita mapema na kuwapa uzoefu mapema
Tanzania kwa sasa ina washambuliaji namba 9 chipukizo wengi sema hawapewi nafasi.. kocha yupo radhi kilazimisha beki acheze namba 9 lakini sio kuwaita hawa chipukizi.

Kelvin John

Andrew simchimba

Onesmo mayaya

Salim aye

Hawa ni vijana wazuri sana kwa kufumania nyavu na wameomyesha uwezo wa hali ya juu sana kwenye timu za vijana.

Kwanini makocha hawataki kuwamini vijana hawa.

Mbele ya goli ni akili ya striker.. na sio umbo la mtu.
 
Itapendeza zaidi kama tutakaa na kocha kwa muda mrefu zaidi.. sio kufukuza hovyo.
 
Tofauti kubwa kati yetu na Sudan wao wachezaji wao wazuri wanacheza ligi yao!! kwa sasa Tanzania nguvu yetu pale mbele inategemea uwepo wa Samata na Msuva!! Tatizo lingine kwa wachezaji waliochaguliwa kulikua hakuna plan B, kwa vimo vya wachezaji wetu krosi zile za Maganga ni kazi bure
 
Kuna watu niliwaambia acheni kumu_overrate Kaseja kipimo chake kinanza na Sudan ngoja nifukue makaburi sasa
 
mengi yatasemwa.. lakini bado nasema huo uwanja haufai kwa sasa una gungu/nuksi/mikosi katika mechi za mashindano za kimtaifa
kuna timu imeuharibu huo uwanja kwa mambo yao ya hovyo
 
mengi yatasemwa.. lakini bado nasema huo uwanja haufai kwa sasa una gungu/nuksi/mikosi katika mechi za mashindano za kimtaifa
kuna timu imeuharibu huo uwanja kwa mambo yao ya hovyo
 
Back
Top Bottom