Habari za mchana
Nina mapungufu mengi nikiwa kwenye mahusihano moja ni kutojua kufoka yaani nashindwaga kabisa kumfokea mtu nilie nae kwenye mahusihano
Na Kama amenikosea basi nikiaza kumuelekeza kwa upole naamini ndio njia rahisi na mzuri bas anapanda juu na Mimi nikiona mtu kapanda juu basi natulia na msikiliza yeye now nina history nying za waty ambao tumeachna Sababu hiyo mm huwa sipend kufoka na kupiga
Yaani kifupi mimi sio mkali ata akinikosea mimi basi naomba msamaha nisaidie nifanye nini? I need to change na nahitaji ushauri mzuri na sio matusi wala kejeli
Kushindwa kufokea na kupiga kisha wewe kuachwa, ni maajabu haya!
Hilo laweza kubeba madhaifu yako mengine ambayo haujayaeleza hapa, ambayo unatakiwa ujitathimini, yaani kuanzia "show" zako pamoja na huduma kwa mamsap.
Wanawake wengi katika mahusiano hawapendi kukelembeshwa kwa maneno pamoja na kudundwa, iweje kwako iwe kinyume?
Waweza kuwa mpole na "msikivu", lakini kama haujipindi kiume kutoa shoo za kibabe, ukawa mchoyo wa kuhesabu finyango za nyama jikoni, hauna stori za maana chumbani, muda wote wewe ni kimya tu hauongeleshi, "mkono wa birika",kutoa matumizi kwa mbinde, kama unazo sifa hizo yakupasa ujirekebishe pakubwa, maana upole wako kwa madhaifu hayo hutoboi.
Ukisikia mwanamme mpole kwa mwanamke, ujue ana kauli thabiti za kimahaba kwa mkewe na anampenda kwa dhati, lakini si mpole kitandani hilo ulijue!
Kama una sifa nilizozieleza hapo juu, jitathimini na uchukue hatua broda.