MAPYA YAIBUKA KUKWAMA UJENZI WA MELI KIGOMA, MZABUNI ALILIPWA ZAIDI YA ASILIMIA 15

MAPYA YAIBUKA KUKWAMA UJENZI WA MELI KIGOMA, MZABUNI ALILIPWA ZAIDI YA ASILIMIA 15

Oneonone

Member
Joined
May 5, 2026
Posts
17
Reaction score
17
MAPYA YAIBUKA KUKWAMA UJENZI WA MELI KIGOMA, MZABUNI ALILIPWA ZAIDI YA ASILIMIA 15

Siku chache baada ya kuandikwa habari kuhusu kukwama kwa meli ya abiria 600 kutokana na ubadhirifu mkubwa wa fedha, mapya yaibuka.

Ujenzi wa meli hiyo kama utafanyika kwa mjibu wa mkataba ulivyosainiwa kwa siri ofisini kwa Mkurugenzi wa kampuni ya meli Tanzania - TASHICO mkoani Mwanza utagharimu zaidi ya bilioni 150.

Mwaka jana mwezi wa nne mkandarasi Kampuni ya M/S Gas Entec CO, LTD, ililipwa zaidi ya asilimia 15 ya fedha za mkataba wa ujenzi wa meli hiyo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa baada ya habari hii kuandikwa, Kampuni ya Meli Tanzania TASHICO, kupitia Mkurugenzi wake, Eric Hamis, ilimtafuta mwandishi wa habari hizi na kumtumia video fupi iliyoambatana na maneno nanukuu “HIVI NDIVYO MELI MPYA YA TASHICO INAVYOJEGWA KIGOMA”.

Lakini ukweli ni kwamba video hiyo ilitengenezwa oktoba 30 mwaka huu ili kuaminisha umma kuwa kazi inaendelea jambo ambalo sio kweli kwa kuwa eneo la kazi mkoani Kigoma hakuna mkandarasi wala mkandarasi mshauri.

Kwa mjibu wa vyanzo vya ndani vya kampuni ya meli Tanzania na kupitia video iliyotumwa inaonyesha kazi ya ukataji wa vyuma (steel cutting) umeanza oktoba 30 mwaka huu.

Pamoja na kutolewa kwa video hiyo fupi kuaminisha watanzania ukweli ni kwamba hakuna ukutaji wa vyuma ambao unaendelea nchini Korea kusini.

Pia kwa mjibu wa wataalamu kabla ya kuanza ukataji wa vyuma inapaswa mchoro uwe umekamilika asilimia 100 na uwe umepitishwa na umoja wa kimataifa wa mashirika ya uainishaji wa meli na ubora wake.

Katika mradi huo, ilichaguliwa kampuni ya Lloyds Regester ili aweze kushirikiana na mkandarasi mshauri ambaye hajapatikana mpaka sasa.

Kutokana na vitu hivyo kutofanyika ni dhahiri video hiyo ni ya kubumba kwa kuwa Lloyds Regester na mkandarasi mshauri hawapo kushuhudia ukataji na kugonga mihuri vyuma vinavyotajwa kukatwa na Mkurugenzi, Eric Hamis.

Wasiwasi umeibuka kukosekana kwa Lloyds Regester na mwenzake mkandarasi mshauri kunaweza kusababisha Mkandarasi mkuu kuchukua vyuma ambavyo havina ubora kama mkataba unavyoelekeza.

Kwa mjibu wa mkataba uliotolewa na TASHICO kwenda kwa Mkandarasi kampuni ya M/S Gas Entec Co, LTD inaonyesha itakuwa na uzito wa vyuma wa tani 4208.

Cha kusikitisha kwa mjibu tangazo lililotolewa jana lineonyesha uzito wa vyuma ni 2900 wakati serikali imelipia fedha za uzito wa tani 4208.

Kutokana na mchezo huo wa upigaji unaofanyika, tunaiomba serikali kuhakikisha inachukua hatua za haraka kuokoa fedha za umma kwa kuwa mpaka hakuna kinachoendelea mkoani Kigoma.

Juhudi za kuwatafuta Lloyds Regester ili waweze kudhibitisha michoro ya meli na ukataji wa vyuma vya meli hiyo kama unafanyika.

Hapo chini ni kampuni ya M/S gas Entec Co, LTD ambayo ilipewa zabuni kwa upendeleo kwa gharama kubwa ikilinganishwa na kampuni mbili ikiwemo ya kizalendo ya Songoro ambayo ilikusudia kujenga meli hiyo kwa dollar milioni 38.
 

Attachments

Songoro marine hawajawahi kutengeneza meli ya masafa marefu hivyo kukosa kigezo cha uzoefu.
Haingekuwa sahihi kuwapa kazi ya kujenga meli hii.

Songoro marine kilichowaangusha ni ukosefu wa uzoefu wa kujenga meli za masafa marefu.
Kwa hiyo aliyefanya technical evaluation atakuwa aliwaona kuwa hawakuwa technically compliant, kwa iyo bid yao isingeweza kwenda kwenye next step ya financial evaluation.
Au mlitaka Songoro apewe kazi kubwa ili baadae yaje yatokee ya MV Bukoba?
 
TAKUKURU wapo wapi?
Mambo kama haya yanatokea Afrika kule China hao wabadhirifu wangeshakuwa marehemu
 
Tanganyika yangu inatafunwa mno. Hii yote ni CCM.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom