Mara: Abiria 16, Dereva na Kondakta wakamatwa kwa tuhuma za kumpiga Askari wa Usalama Barabarani

Mara: Abiria 16, Dereva na Kondakta wakamatwa kwa tuhuma za kumpiga Askari wa Usalama Barabarani

Halali yake,waonevu sana!
Usichojua hadi muda huu waliohusika watakuwa wametepeta kwa kipigo. Baadhi yao jela wataenda. Dereva na mwenye gari wanaweza kuwa na wakati mgumu zaidi baada ya hili tukio. Kimsingi kuna familia kadhaa zitapita kwenye msukosuko mkali mno. Nyie mashujaa wa mtandaoni endeleeni kusifia ujinga watu wazidi kuingia kwenye matatizo.
 
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18, wakiwemo dereva, kondakta na abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, saa 12 jioni katika mkoa wa Mara.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo, amesema kuwa askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari. Hata hivyo, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia askari huyo.

“Askari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke. Lakini ghafla walimzonga kwa maneno ya kebehi, na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?” alisema Mwambelo.
=============
Wananchi wanahasira sana hadi kufikia hatua ya kumtwaga askari mh tunapoelekea sasa ni balaa tupu!

Soma Pia: Abiria watakiwa kupaza sauti kwa Madereva wasiofuata Sheria za Usalama Barabarani

Kwani yeye ni mahakama Hadi aseme abiria wataenda gerezani?

Mahakama ndiyo yenye kupeleka watu gerezani yeye hayk mamlaka ya kupeleka watu gerezani kayatoa wapi?
 
Usichojua hadi muda huu waliohusika watakuwa wametepeta kwa kipigo. Baadhi yao jela wataenda. Dereva na mwenye gari wanaweza kuwa na wakati mgumu zaidi baada ya hili tukio. Kimsingi kuna familia kadhaa zitapita kwenye msukosuko mkali mno. Nyie mashujaa wa mtandaoni endeleeni kusifia ujinga watu wazidi kuingia kwenye matatizo.
Umemaliza? Wewe ni nani kunihariri kipi niseme ama nisiseme?
 
Kuna vitu vya msingi vya kujiuliza hapa, hilo gari la safari ndefu au fupi?

Kama fupi kwanini washushwe? Sijawahi ona haya Dar yakitokea au Dar sio Tanzania maana watu wanajaa kwenye magari mpaka huwezi kugeuka. Kwanini double standard?

Kama la safari ndefu, alikua anawashusha awatafutie ustaarabu gani? nani asiyejua unaweza shushwa kwenye gari ukaokotwa maiti?

Kumpiga polisi ni kosa kisheria pia kumpiga raia, kumtesa na kuua ni kosa kisheria. Hakuna raia anayeamini polisi saivi na haya ni matokea ya kazi zao wenyewe.

Kutumia ubabe hakutawasaidia polisi. Mtawapiga, mtawafunga, mtawafungia leseni ila mkiiendelea hamtawamaliza.
 
Acha iwe vyovyote vile chief. Tulipofikia hata usipowarushia ngumi, wanakuvalisha pingu wanaenda kukuua wakutupe ununio. Bora iwe rabsha rabsha na kashikashi hivi hivi.
Kwa hii kesi ya abiria kusimama kwenye gari?! au hizo issues nyingine hizo sijasemea mkuu wangu.
 
Kwanza askari kupigwa na wananchi ni aibu, habari kama hizi wazifiche huko huko vijijini, wavulana wa Dar don't try this at DAR.
Niko againsts askari kupigwa, si jambo zuri lakini kutokana na matukio ya hivi karibuni. Raia hawana imani , ile trust ya jamii kwa polisi imeshuka mno, na hii ni red alert
 
Niko againsts askari kupigwa, si jambo zuri lakini kutokana na matukio ya hivi karibuni. Raia hawana imani , ile trust ya jamii kwa polisi imeshuka mno, na hii ni red alert
Hawa Polisi ndio wanaopush polisi jamii, tusisahau mwezi huu katika maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la polisi walihamasisha kufanya matendo yatakayo rudisha imani katika jamii kama vile kutoa misaada kwenye vituo vya yatima, kufanya usafi, kuchangia damu, leo hii hata wiki haijaisha wako barabarani wanaonyesha magari yao yakurusha maji ya washa washa ? Hivi strategist wa nyie polisi ni nani ? Mkuu halafu kama sijakosea ulisoma BALE ? mmeshindwa kulisaidia jeshi la polisi ? kwenye hizi tabia za jeshi la kikoloni wakisahau watanzania ni baba zao, mama zao, dada zao na sisi kwa kodi zetu ndio tunawafanya wanunue hata mafuta ya kupaka sura zao ngumu.
 
wHawa Polisi ndio wanaopush polisi jamii, tusisahau mwezi huu katika maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la polisi walihamasisha kufanya matendo yatakayo rudisha imani katika jamii kama vile kutoa misaada kwenye vituo vya yatima, kufanya usafi, kuchangia damu, leo hii hata wiki haijaisha wako barabarani wanaonyesha magari yao yakurusha maji ya washa washa ? Hivi strategist wa nyie polisi ni nani ? Mkuu halafu kama sijakosea ulisoma BALE ? mmeshindwa kulisaidia jeshi la polisi ?
Wanahitaji ku reform policy yao. Ukiwa mtu wa kutumia nguvu, na raia wata adopt, wata respond the same. Result ni mgogoro btn polis na raia.
Wanatakiwa waondoke kwneye mentality ya kutumia maguvu in evetything, kizazi cha sasa kina learn na ku adopt haraka, mwishowe watajiwekea mazingira magum ya ufanyaji kazi
 
Japo hao askari wa barabarani wanaosemekana kutusaidia ni wala rushwa kupita kiasi, na pia sidhani kama kulikua kuna haja ya jamii forum kuchapisha habari kama hii kwa sababu imeegamia upande mmoja sana ya kutaka kutuonyesha dereva na raia au abiria wanamakosa pekee yao ingependeza tungesikia na upande wa pili ili tujue walifikiaje hatua ya kumshambulia askari, maana tumekua involved in more than one event ambapo dereva anashushwa na trafiki na wanaenda nje kuongea muda mrefu na muda mwingine gari unakuta limeegeshwa sehemu hatarishi na hatujawahi ingilia maongezi yako, kwa io swali hapa ni kwa nn raia aingilie au ampige askari, lazima tatizo lilianzia kwa askari mwenyewe
 
Back
Top Bottom