Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Hii ni mbinu wanayoitumia CCM kwa vyama vya upinzani hivi sasa, wakiona chama cha upinzani kinawaletea 'ukaidi'
Waliitumia kwa Maalim na CUF kipindi kile baada ya Maalim kugomea uchaguzi kipindi kile, wameitumia kwa Mbatia baada ya Mbatia kupingana sana na Samia kwenye mambo mengi ikiwamo kumuunga mkono Ndugai na kukigomea TCD na kikosi kazi
Mbatia ambaye kwa Magufuli alikuwa 'mpinzani laini' hadi kutuhumiwa na Chadema kuwa anatumika, kwa Samia ameonyesha msimamo mkali na kurudisha urafiki na Chadema
Kwa Chadema watu wanaweza kudhani haiwezekani ila hakuna wanachoshindwa CCM
Wanatangaza amani huku wameshika mapanga, wanazuga kuwaita wapinzani kutoa maoni kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya siasa nchini, huku wakiwa wanawachinja wapinzani kwa silaha zile zile zinazojadiliwa
Kwa sasa Chadema kama kuna manung'uniko ya viongozi wao kuwa karibu sana na Ikulu, baadhi wakihisi 'amesha tulizwa' sasa CCM wanaweza kutumia manung'uniko hayo hayo ukashangaa wajumbe kadhaa wakapewa mlungula wengine ikafanyika forgery kama kawaida yao ukaitishwa mkutano, na hao watu kadhaa wakang'olewa na msajili akafanya hayo maamuzi kuwa 'official' na kuwaambia Chadema kama mna malalamiko nendeni mahakamani
Sababu za kuwang'oa unaambiwa ni 'kukisaliti chama na kuwa karibu ba ikulu' ili kuyafanya yaungwe mkono na wanachadema wanaolalamika sasa