Mara ghafla Mbowe, Mnyika, Lissu na Heche wasimamishwa uongozi Chadema, msajili aridhia

Mara ghafla Mbowe, Mnyika, Lissu na Heche wasimamishwa uongozi Chadema, msajili aridhia

CDM wakifanyiwa uhuni wa NCCR ni rahisi sana ku-build case kwa wahisani na kueleweka zaidi, hasa ukizingatia credibility waliyo-jijengea kutokana na figisu za 2020 election. Itawafanya wahisani kuelewa jinsi serikali inavyotumia rushwa, hujuma, mamlaka yasiyo halali nk. Kiufupi watatengeneza crisis.
CDM ipo hapo kutokana na michango ya wengi ikiwemo ya baadhi ya wana CCM wenyewe, ambao wanaamini CDM ikifa hakutakuwa na upinzani imara na hvyo serikali isiyojali yeyote itazaliwa na wananchi wote watapoteza, Mfano-Kukosekana kwa chama imara cha kutetea maslahi ya wafanyakazi hupelekea au kuchangia maisha duni ya wafanyakazi kutokana na weak bargaining power.
Ni kichaa pekee mwenye maoni mafupi asiyeweza kuona faida ya strong opposing side mahala popote hasa kwenye siasa 🤣 🤣 , manake a strong opposition inamfaidisha mwananchi wa kawaida na wote katika nchi.
Hawa CCM hawaoni aibu, wanatamani kuifuta chadema hata Kesho, ila mbinu za Chadema ndiyo zinawashinda kila wanavyopanga mashambulizi yanabuma. Hata hivyo niwaase chadema na watanzania kwa ujumla tunao wajibu wa kupambania taifa hili dhidi ya mbinu za kijinga kama hizi. Taifa letu kwa sasa halima standards, sheria hazifuatwi, katiba inasiginwa hadharani na inaonekana kwao ni kawaida tu. Na haya mambo kadri tunavyoya-entertain ndivyo tunashindwa kuwa taifa lililostaarabika kisa tu maslahi ya watu wachache wanaofaidika na kuendesha uhuni kama huu.
 
Hii ni mbinu wanayoitumia CCM kwa vyama vya upinzani hivi sasa, wakiona chama cha upinzani kinawaletea 'ukaidi'

Waliitumia kwa Maalim na CUF kipindi kile baada ya Maalim kugomea uchaguzi kipindi kile, wameitumia kwa Mbatia baada ya Mbatia kupingana sana na Samia kwenye mambo mengi ikiwamo kumuunga mkono Ndugai na kukigomea TCD na kikosi kazi

Mbatia ambaye kwa Magufuli alikuwa 'mpinzani laini' hadi kutuhumiwa na Chadema kuwa anatumika, kwa Samia ameonyesha msimamo mkali na kurudisha urafiki na Chadema

Kwa Chadema watu wanaweza kudhani haiwezekani ila hakuna wanachoshindwa CCM

Wanatangaza amani huku wameshika mapanga, wanazuga kuwaita wapinzani kutoa maoni kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya siasa nchini, huku wakiwa wanawachinja wapinzani kwa silaha zile zile zinazojadiliwa

Kwa sasa Chadema kama kuna manung'uniko ya viongozi wao kuwa karibu sana na Ikulu, baadhi wakihisi 'amesha tulizwa' sasa CCM wanaweza kutumia manung'uniko hayo hayo ukashangaa wajumbe kadhaa wakapewa mlungula wengine ikafanyika forgery kama kawaida yao ukaitishwa mkutano, na hao watu kadhaa wakang'olewa na msajili akafanya hayo maamuzi kuwa 'official' na kuwaambia Chadema kama mna malalamiko nendeni mahakamani

Sababu za kuwang'oa unaambiwa ni 'kukisaliti chama na kuwa karibu ba ikulu' ili kuyafanya yaungwe mkono na wanachadema wanaolalamika sasa

Kuhusu Chadema iacheni wengi walijaribu kuiua chadema wakafa wao.
 
Wanaweza kuwa na mipango hiyo,lakini wanashindwa waiingieje.Maana CDM huanza na Mungu na kumalizia na Mungu.
 
Hii ni mbinu wanayoitumia CCM kwa vyama vya upinzani hivi sasa, wakiona chama cha upinzani kinawaletea 'ukaidi'

Waliitumia kwa Maalim na CUF kipindi kile baada ya Maalim kugomea uchaguzi kipindi kile, wameitumia kwa Mbatia baada ya Mbatia kupingana sana na Samia kwenye mambo mengi ikiwamo kumuunga mkono Ndugai na kukigomea TCD na kikosi kazi

Mbatia ambaye kwa Magufuli alikuwa 'mpinzani laini' hadi kutuhumiwa na Chadema kuwa anatumika, kwa Samia ameonyesha msimamo mkali na kurudisha urafiki na Chadema

Kwa Chadema watu wanaweza kudhani haiwezekani ila hakuna wanachoshindwa CCM

Wanatangaza amani huku wameshika mapanga, wanazuga kuwaita wapinzani kutoa maoni kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya siasa nchini, huku wakiwa wanawachinja wapinzani kwa silaha zile zile zinazojadiliwa

Kwa sasa Chadema kama kuna manung'uniko ya viongozi wao kuwa karibu sana na Ikulu, baadhi wakihisi 'amesha tulizwa' sasa CCM wanaweza kutumia manung'uniko hayo hayo ukashangaa wajumbe kadhaa wakapewa mlungula wengine ikafanyika forgery kama kawaida yao ukaitishwa mkutano, na hao watu kadhaa wakang'olewa na msajili akafanya hayo maamuzi kuwa 'official' na kuwaambia Chadema kama mna malalamiko nendeni mahakamani

Sababu za kuwang'oa unaambiwa ni 'kukisaliti chama na kuwa karibu ba ikulu' ili kuyafanya yaungwe mkono na wanachadema wanaolalamika sasa
Heche na Lissu ni pandikizi ya dola, yanajifanya kuwa mapinzani kumbe Kila siku yanatoa taarifa kijitonyama.
 
Madai yakijinga sana,wakati munawafukuza wakinaMdee mulimuita Kaimu msajili,sasa alivyoitwa NCCR kunaubaya gani?au kwa sababu atia Mbatia!
 
Kwa chadema hawataweza,wakifuta hawataweza kuzima kelele,chadema leo hata wakibadili jina la chama watafutwa na wafuasi wengi na watafuatwa na wafuasi wao maana wamejijenga. Tanzania hii ukisikia ile nyumba ni wapinzani kinachokuja akilini ni chadema .
 
Mbowe atawafurusha wote hao mmoja baada ya mmoja, chama cha ba’mkwe.
 
Back
Top Bottom