MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

Jamani si wataisha wote huko yakabaki magofu tu?
 
Haikawii kuambiwa amenunuliwa na tulimuona siku nyingi nyendo zake za kutaka kutusaliti kamati kuu ilikaa na kumuandia barua ya kujieleza lkn kabla ya kumfukuza kaamua kuondoka.

Mbona hamkusema haya mapema na mmengoja ameondoka ndiyo sasa mnatutapikia hivi? Kataeni muwezavyo ila CHADEMA kuna tatizo la msingi ambalo kama msipokuwa makini nalo kuna uwezekano hadi kufikia mwaka 2020 huko akabaki tu mwenye Chama chake Mzee Edwin Mtei na Dalali wake Mkuu Freeman Mbowe na Wabunge wote wakarudi CCM. Yaani badala ya Kutafakari kwanini mnakimbiwa nyie mlivyo na akili fupi neno lenu la Kwanza na la Kujitetea ni kuwa ' Wananunulika ' na Serikali kupitia Chama Tawala cha CCM.Tukiwashaurini mnatudharau acheni sasa ' mkomeshwe ' labda mawazo yetu ya Kiuhalisia mtayakumbuka sasa na kubadilika.
 
kitengo cha chadema kimelala? Wasiweze kulibaini mapema akafukuzwa
CHADEMA ya sasa hivi inafukuzana na vivuli tu. Kwa kifupi imepoteana.
Kwasasa CHADEMA ipo sababu upinzani dhidi ya serikali umeimarika sana na wapinzani halisi ni watu, hivyo CHADEMA inaishi kwa kivuli cha upinzani huu lakini wao kama chama na jinsi walivyo dhibitiwa na kubanwa kingekua kimeshajifia kitambo tu.
Ila nguvu watakayoamka nayo, ambayo watapewa na watu wa makundi yote itatisha sana
 
Mkuu mbona unashangaa? Magufuli ni rais mzuri mno,hana kasoro yoyote ile,na Tanzania haitapata rais bora kama Magufuli,tangu aingie madarakani uchumi wa Tanzania umepaa kwa 45%,ajira zimeongezeka kwa 38%, Demokrasia imeshamiri,Uhuru wa vyombo vya Habari umekua,sasa kwa nini wapinzani wasimuunge mkono?
Napendekeza Magufuli atawale milele.
CCM HOYEEEEEEEE......!!!
Haijalishi. Lichama letu chadema ndio linaporomoka hivyo aisee kamanda.
 
Hizi zamu zitapita na huu ujinga utapita tu.

Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.
Hoja inapate nguvu wakati wabunge wa upinzani wanapukutika tu
Chadema ndio imekufa kanda ya ziwa kwa ubinafsi wa Mbowe,.Bado huyo wa ukerewe anasubiri msiba uishe,chadema kinakua officially chama cha kikanda
 
Back
Top Bottom