MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

duhhhh haya nadhani sasa hivi watapita kwa kishindooo kikubwa kabisaaa maana hakuna CHADEMA tena
 
Wanatukumbusha enzi za karne ya 17
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Dreamliner na daraja la Tazara. Sikutegemea Tanzania itakuja kuwa kituko kiasi hiki 21st century watu wanakimbiza na mambo ya kawaida?
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Nini kinaendelea CHADEMA?
 
Hili jamaa jinga kweli. Eti mchagueni mwakilishi wakati keshaahidiwa tayari
 
Hoyeeeeeeeeee
Mkuu mbona unashangaa? Magufuli ni rais mzuri mno,hana kasoro yoyote ile,na Tanzania haitapata rais bora kama Magufuli,tangu aingie madarakani uchumi wa Tanzania umepaa kwa 45%,ajira zimeongezeka kwa 38%, Demokrasia imeshamiri,Uhuru wa vyombo vya Habari umekua,sasa kwa nini wapinzani wasimuunge mkono?
Napendekeza Magufuli atawale milele.
CCM HOYEEEEEEEE......!!!
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:

​
Hata muonekano wake ni wa kilumumba
FB_IMG_1538081501544.jpeg
 
Taarifa zilizopo ni kua mbunge huyo amejivua uanachama wa chadema na kuhamia CCM

Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.

Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.

Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.

By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.
Unachosema ni kwamba demokrasia ni Gharama tuamue kutokua Na uchaguzi kwasababu ni Gharama?
 
Back
Top Bottom