Hivi kipindi kile kina Lowassa, Sumaye, Nyarandu na wengine wengi wanahamia upinzani kuunga mkono hazikuwa zama za ujinga?Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.
Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.
Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Hizi zama zitapita na huu ujinga utapita tu.
Hoja ya Zitto kuhusu kile kifungu inazidi kupata nguvu kadri siku zinavyokwenda.
Kamwe hamtakuja kuniona namuunga mkono huyu mtu maana ni sawa na mhujumu uchumi.
Sisiem ni magawa rushwa na hii ni rushwa (jinai) inayoratibiwa na majitu yanayojiita kuwa ni wazalendo kumbe ni mahujumu uchumi tu.Ndugu SS, usimuunge mkono wala usimtie manani.
Lakini una maswali ya kujiuliza NA kukiuliza chama chako.
1. Kwa nini wabunge wenu wote wanao jiuzulu, mnawatilia mashaka kuwa wamenunuliwa , lakini hamjiulizi jee haya wanayoyasema yana ukweli wowote?
2. Chadema mlikuwa mkijigamba kuwa mnaa idara kubwa NA imara ya kuchunguza mambo, NA hata mlikuwa mkipata mikakati, ya serekali kabla haijatikizwa. Leo mnashtukizwa na kimbia kimbia NA bila habari wala kuona ishara. JEE ile idara yenu imekufa au Slaa kaondoka nayo?
Na kunangwa kote kule na mzee Magu ukisikia kujipeleka kwenye mdomo wa mamba ndio hivi
Thibitisha rushwa inaingiaje hapo. Lowassa aliondoka CCM na kugombea urais. Je hakukuwa na rushwa hapo. Masha, Makongoro Mahanga, Nyarandu nakadhalika. Iweje wanaelekea CCM muiite rushwa? Acheni ujingaa jamaani. Tafuten sababu ya kukimbiwa.Sisiem ni magawa rushwa na hii ni rushwa (jinai) inayoratibiwa na majitu yanayojiita kuwa ni wazalendo kumbe ni mahujumu uchumi tu.
Mkuu ni kweli njaa ni kitu kingine ila hii biashara inayofanywa kwa sasa na hawa kijani inathibitisha ni kwa nini mwafrika alipelekwa/alifanywa mtumwa na mtu mweupe....mtu mweusi haaminiki anaweza kukana hata ndugu zake wa damu sembuse chama cha siasa? laana tupu Africa na waafrika tazama bara zima la Africa ni vituko tu..Dark continentsana
Kwa hiyo wewe ni mwerevu na una hekima na busara umehamia ccm kwa sababu ya kuhakikishiwa ushindi na vyeo iko siku mtatamani milima iwaangukieKwa mtu makini na mwenye busara hawezi kubakia CHADEMA .
Watu wa kanda maalumu hawataki unafiki ndio maana wanahama. Huwezi kuwaswaga kama ng'ombe eti waipinge serikali wakati wanaona kero walizokuwa wanazipigia kelele zinarekebishwa.Watu wa kanda maalum mmekuaje, binafsi naona kitu cha fedheha
Sijui hata cha kukujibu kwani usemayo ni yale yale ya siku zote kama wenzako! Hakuna hoja mpya so no comments on this flap.Sijazaliwa nanjilinji mjomba kama hicho kivuko cha tazara au sijui Bombardier ndio vinakuchanganya ni wewe unalipia bombardier au sijui uwanja wa ndege Chato ,wakati kuna kivuko cha miaka ya Nyerere kinaua watu 200 mnashindwa kuwaokoa kisa giza ? Elimu yetu ni uchafu tu ,kilimo ni uchafu vilevile ,vitu ambavyo vinagusa maisha ya mtanzania wa kawaida kabisa ,halafu ndio unashangazwa na usanii wa wanasiasa huyo anapiga mark time tu amalize muda wake asepe
1.5 Trilioni alizosema CAG hazijulikani matumizi yake ,ingefanya mangapi ?
Unataka niungane na wewe kusherekea upuuzi huku maradhi ,umaskini na ujinga ndio Diet ya Watanziania ?
utawala chama kimoja umepanda moto, kumuunga mkono mpaka uhame? NEC hiyo gharama tuzijinge shule zetu jamani yale mapango kwenye shule za kata yawe madarasa. Kumuunga mkono muislamu kwa matendo yake, mpaka uhamie ukristoni.
Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.
Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Akitangaza kujivua uanachama amesema,
Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.
Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.
VIDEO:
🙂🙃Alifika Bei Huyu Sasa Anahaha[emoji854]