Mara: Mzazi ampiga mwalimu na kumjeruhi baada ya kumuadhibu mwanae

Mara: Mzazi ampiga mwalimu na kumjeruhi baada ya kumuadhibu mwanae

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa mwanafunzi ni mtumwa ama mfungwa (na wafungwa pia wana haki zao!). Serikali ilishaweka masharti ya viboko, walimu wengine wanapiga watoto hadi kuwaumiza hata kwa kosa dogo tu! Mtoto anapigwa hadi kutoka alama ya viboko, hadi wengine wamefariki! Acheni kutetea ujinga, kama huna karama ya kufundisha bila kupiga, nenda kalime!
 
Kulikuwa mtoto mmoja wa kiume wa brother wangu mmoja. Alikuwa mtukutu sana. Kesi shuleni(primary) haziishi, kila wakati "uje na mzazi wako"
Akiitwa mzazi, alikuwa ananiomba niende. Baada ya majadiliano, nawaomba radhi sana Walimu wake.
Hitimisho inakuwa viboko sita vya makalioni kutoka kwa mzazi. Nakabidhiwa kiboko. Nilikuwa nacharaza bakora kisawasawa. Toto halitowi hata chozi.
Jioni tukikutana nyumbani, maneno yake:
"Daa! Baba mdogo anachapa fimbo kuliko hata Mwalimuu!!
Uzuri wa yule mtoto, kichwani alikuwa yuko vizuri.
Paaap! akafaulu darasa la saba, akapelekwa shule moja nzuri sana Mkoa wa Pwani. Ile karibia anamaliza form two, akamlamba mwenzie ngumi za uso, akafukuzwa shule.
Brother akawazaa, akaona ngoja amtafutie shule moja private ya watemi watupu, kwao makonzi ya kichwa ni kama kutafuna karanga.
Akaipata Tanga mjini. Dogo likapigana kitemitemi mpaka likamaliza form four.
Baba yake akawa ameishapoteza matumaini kabisa hata maendeleo yake hafatilii.
Siku ambayo sitakuja kuisahau ni siku ambayo Dogo anamkabidhi baba yake matokeo ya mitihani ya form four.
Brother alicheka, alicheka, mpaka akakaa chini!! Kulikoni?
Dogo limepaform, limepiga division one, point 16 yenye misonge miwili, Mathematics na Physics!!
Toka siku hiyo wakawa marafiki kama mtu na mdogo wake!
 
Huyo mzazi akae na mtoto wake nyumbani awe anamfundisha mwenyewe.
Poleni sana walimu matoto majeuri yatafunzwa na walimwengu
 
Unaanzaje kupiga mtoto wa watu kwa kazi ya malipo ya shilling laki 8. We ingia fundisha maliza fanya mambo yako mengine ya kujijenga kipato. Mtoto mtukutu toa nje ya darasa tu ujinga utamfunza mwenyewe.

Sema elimu bado tunaachangamoti nyingi, fikiria hadi leo mabinti hawaruhusiwi kusuka, au wanafunzi lazima kuvaa viatu vyeusi.
 
Kama hutaki mwanao apigwe baki naye nyumbani uwe una mfundisha wewe
Kuwa makini unaposoma mada, wewe unaniambia mimi wakati mimi ninamnukuu mwanasiasa aliyeshindwa kutatua tatizo!
JF should be for GT's.
 
Mambo ya walimu kuchapa viboko watoto wasiowazaa (wanafunzi) ni ya ki primitive.
Hebu tuwaige wazungu waliotuletea elimu.
Siku moja mwanangu p wa chekechea aliniambia kuwa hataki shule mwalimu Jane kamchapa.
Niliwaza mbali sana.
Kuchapana ni ukoloni, sio shule tu hata nyumbani hatupaswi kuwachapa watoto
 
Unaanzaje kupiga mtoto wa watu kwa kazi ya malipo ya shilling laki 8. We ingia fundisha maliza fanya mambo yako mengine ya kujijenga kipato. Mtoto mtukutu toa nje ya darasa tu ujinga utamfunza mwenyewe.

Sema elimu bado tunaachangamoti nyingi, fikiria hadi leo mabinti hawaruhusiwi kusuka, au wanafunzi lazima kuvaa viatu vyeusi.
Mwl wa primary gani analipwa laki 8 mkuu.?!
 
Mpaka anatoa kwenye ATM ana 380k - 400k

Wa sekondari hawa diploma science wanakula 530k, hamna mwl wa primary wala secondary serikalini anaelipwa laki 8

Sasa kwa nini wanapiga watoto wa watu kwa ujira mdogo hovyo
 
Kuna watu wanaamini kabisa kuwa mwanafunzi ni mtumwa ama mfungwa (na wafungwa pia wana haki zao!). Serikali ilishaweka masharti ya viboko, walimu wengine wanapiga watoto hadi kuwaumiza hata kwa kosa dogo tu! Mtoto anapigwa hadi kutoka alama ya viboko, hadi wengine wamefariki! Acheni kutetea ujinga, kama huna karama ya kufundisha bila kupiga, nenda kalime!
Hakika "Kama huna karama ya kufundisha nenda kalime"
 
Mpaka anatoa kwenye ATM ana 380k - 400k

Wa sekondari hawa diploma science wanakula 530k, hamna mwl wa primary wala secondary serikalini anaelipwa laki 8
Wapo wanalamba hadi M na usher upo wapi wewe Mkuu
 
Huyo mzazi akae na mtoto wake nyumbani awe anamfundisha mwenyewe.
Kama huna karama ya kufundisha nenda kalime! KUPIGA SIO KUFUNZA MNAWAUMIZIA WENZENU WATOTO TU.!!!
Nani alikufunza kuwa MIFIMBO HUFUNDISHA???? AU KUMFANYA MTOTO AELEWE???!
 
Katika kitu kilikua kinanikera shuleni ni fimbo, mwalimu anaingia anacharaza viboko darasa Zima.

Fimbo zilikua zinanifanya nione shule ni kitu kibaya mpaka nilipohamia shule ambayo hawachapi viboko na wanafunzi wanafaulu vizuri sana.

Ninayo Mifano ya wanafunzi walioacha shule Kwa kuogopa viboko tu.
Kama kuna watu fimbo ziliwasaidia mimi hazikunisaidia kabisa.
 
Sasa kwa nini wanapiga watoto wa watu kwa ujira mdogo hovyo
Kazi ya ualimu ni ngumu mno mkuu, bahati nzuri kipindi nikogo chuo miaka kadhaa mewahi ifanyia field so na experience na challenges zake. Watoto wenyewe wakorofi ila pia walimu wengine wanachapa sana kupitiliza idadi ya viboko 6 kikawaida.
 
Back
Top Bottom