UFAFANUZI WA ADHABU YA FIMBO.
Kwanza niwapongeze walimu wenzangu kwa shughuli tunayofanya ya ujenzi na uandaaji wa kada mbali mbali za kujenga taifa letu. Pia poleni kwa misuko suko ya mazingira yetu ya kazi pamoja na changamoto nyinginezo.
Nikiwa kama Mwalimu naelewa uchungu mnaopata mnapokumbana na hali ngumu mathalani mada yetu hapa.
Wazazi/walezi na watanzania kwa ujumla, kwanini Walimu tunatumia fimbo kama adhabu?
Kwanza muelewe, si shule zote Walimu wana chapa wanafunzi, kuna shule adhabu ya fimbo ni mwiko, na ufaulu wa wanafunzi upo imara tu, niwaambie tu Walimu hao ni matokeo ya mfumo wa walimu wale wale wanaotumia fimbo. Suala linalofanya approach kuwa tofauti ni mazingira ya ufanyaji kazi, huwezi kukuta shule yenye mazingira mazuri ya ufundishaji (well-established learning environment) walimu wakawa wanachapa, kuna shule zina wanafunzi wachache sana, pia matumizi ya fimbo ni madogo, kwanini? Kwa sababu adhabu yoyote inahitaji usimamizi, na ifike wakati muelewe kwamba adhabu lazima iwe na maumivu, ili mkosaji ajutie makosa yake, kama adhabu haimuumizi mkosaji hiyo siyo adhabu. Kama una kundi kubwa la wanafunzi wa kuhudumia, hutathubutu kutoa adhabu na kupoteza muda wa kusimamia wakati ambao una mikondo minne ya kufundisha, fimbo ni time saving punishment, mnamalizana yanaisha.
Pia, hakuna kitu waalimu tunaogopa kama adhabu za kisaikolojia, kumbuka neno ama adhabu ya UTENGWAJI inauma na inakaa kichwani kuliko maumivu ya fimbo, na hukaa miaka yote ya maisha ya mwanafunzi, unakumbuka mpaka leo maneno walimu waliokutamkia ila sio fimbo zao, mpka leo unaishia tu kusema ‘yule ticha anachapaa’ ila hujawahi kumfikiria kama mwalimu mbaya, hakuna mwalimu anayetaka ku impart adhabu ya kisaikolojia kwa mwanafunzi, ili anendelee kukaa akilini mwake mpaka atakapokuwa mkubwa.
Elimu ya Ualimu, inafundisha adhabu nyingi, ila walimu wengi wanatumia fimbo kama adhabu tulioona kuwa reliable, waalimu sio wanakada waliopewa mafunzo (trained) sisi ni wanakada tulioelimishwa (educated) hatungoji muongozo kutoka serikalini ni namna gani tuadhibu. Adhabu zifuatazo hazipendelewi na walimu, kwa sababu hukaa akilini kwa mwanafunzi au usimamizi wake unahitaji muda wa ziada zaidi.
1. Detention; kumfungia mwanafunzi kwenye darasa maalumu mithili ya jela ili kumtenga na wenzie na shughuli zote za shule (imagine)
2. Rejection; mfano, imagine wanafunzi wanakusanya madaftari halafu la mwanafunzi mkosaji husahihishi, au wakati wa kujibu maswali hata akinyoosha kidole peke yake humchagui.
3. Suspension; kumuondoa mwanafunzi shule ka kipindi fulani , wengi mnaifahamu
4. Time-out; kumfukuza mwanafunzi kwenye kipindi.
Kumbuka; adhabu zote hizi zinafanywa kwa kipindi fulani.
Kuna adhabu kama kazi za shule, jamani hizi ni mpaka shule ikihitaji [emoji2] huwezi kumpa adhabu mtoto achimbe shimo wakati shimo halihitajiki shuleni, apande maua wakati yapo, afagie wakati pasafi, huo ni uwendawazimu. Kumpa mtoto adhabu constructive kama kuandika essay, [emoji23] sas nyie hii adhabu inamkuta mtoto kipanga, unadhani ataumia? Na kwa taarifa yenu ni kwamba, kama huna cha kuandika, ni huna tuu kwa sababu mental ability has procrastinating peak.
Naomba mjue kama Walimu tuna kazi ngumu, msituchukie ati kwa sababu tumeadhibu watoto wenu, japo kisingizio chenu ni tunazidisha.
Mungu awabariki walimu wenzangu, kuufuta ujinga ni kazi ngumu kwa sababu ujinga wa watu wengi ndio utajiri wa wanye ufahamu kwa namna yoyote lazima tupigwe mawe.
Nawasilisha. [emoji966]