Timu za Africa hazijawahi kuwa na umakini. Hata kipindi kile cha kina Roger Milla, baadae Nigeria ya kina Kanu, Ghana iliyotolewa na Uruguay, nk pamoja na kuwa na timu nzuri sana zinazovutia kuangalia, zilishindwa kwa kukosa umakini. Tena unapojua haupendwi, ingebidi tuwe extra careful hasa katika kucheza rough.
Kina Kanu walionyesha katika Olympics kuwa Africa tunaweza mpira tukiamua.
Toka nishuhudie Cameroon na Nigeria wameenda World Cup wakaamua kufanya mgomo baridi kisa pesa zao za posho zimeliwa na viongozi wao, baadae nikaona Ghana anatolewa ki***ge kwa kukosa ile penalti, sijawahi kuwa na matumaini na timu za Africa. Senegal kidogo aliyemfunga Ufaransa alionekana anajua nini anatakiwa afanye.