Mara wamsimika Makonda na kumpa jina la Manyama, aagiza bodaboza ziachiliwe, Mizigo ya magendo itozwe kodi na iachiliwe

Mara wamsimika Makonda na kumpa jina la Manyama, aagiza bodaboza ziachiliwe, Mizigo ya magendo itozwe kodi na iachiliwe

Unaongelea musoma!?....

Bado haujafika mara wewe!...

Huwezi kukubalika mkoani Mara... Kama haujakubalika TARIME...

Huwezi sema amefika Mara... Kama Bado hajakanyaga TARIME!

HAUJAFIKA MARA... KAMA BADO HUJAKANYAGA TARIME(Hasa vijijini)

TARIME HAKUNAGA FALA!!!
Kote kakanyaga huko. Na Tarime ndio kafanya mkutano.
 
Kote kakanyaga huko. Na Tarime ndio kafanya mkutano.
Hao watu waliompa jina ni WA musoma(wajita)... Tarime hakuna jina la kikurya(manyama!)...

Na pengine ni watu wa maigizo... Maana makonda kazoeleka kwa hilo ...

Nasubiri kumuona akipiga mbizi kuelekea zenji!
 
Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.
Umeliona hilo jicho?
 

Attachments

  • FB_IMG_1699989623291.jpg
    FB_IMG_1699989623291.jpg
    17.7 KB · Views: 3
Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.
Hivi Makonda ni mkabila gani...?
 
"Ninafahamu ya kwamba zipo bodaboda zilizotumia fursa ya mpaka kufanya biashara za magendo hilo halipingiki na mimi ni msema ukweli lakini wapo Wananchi ambao wameendelea kufanya shughuli zao katika kusongesha maisha yao na hili sio la kupinga"

"Sasa Maelezo ya CCM na Mkuu wa Mkoa upo hapa Mhe. Mtanda upo hapa, na nimemsikia Mhe. Waitara anasema nimpigie simu Waziri wa Fedha, sasa hili swala wala sio la kupiga simu ni maelekezo tu ya Chama Cha Mapinduzi, kuanzia sasa leo tarehe 14 hadi ifikapo kesho tarehe 15 pikipiki zote zilizokamatwa Silali warudishiwe pikipiki zao na kama kuna mali zilizokamatwa watozwe kodi warudishiwe mali zao na kuanzia hapo utaratibu wa kisheria ufuate mkondo wake, wapeni fursa watu wafanye biashara kama ni bodaboda alipe kodi, ushuru achukue bidhaa auze, CCM Oyeee"

Cde. Paul Makonda
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa Tarime Mkoani Mara , leo tarehe 14 Novemba, 2023.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendaNaMama
 
Ukiona mkoa wa Mara unafanya jambo hili ujuwe wewe ni kidume kwelikweli. Kule hakunaga chawa.

Ngoja tuone mwisho wa Makonda.

Akabidhiwa kifimbo cha Nyerere.
Manyama ni jina la kijita, ulichodhamiria sicho.
 
📌📌 TUOMBEANE KWA MAANA ZIARA HII IMEWAVURUGA KWELIKWELI WALE WOTE WANAOUTAKA URAIS 2025 NA KUIVURUGA CCM - MWENEZI MAKONDA

"Hayati Mwalimu Nyerere alisema CCM kiwe Chama Cha Sauti ya Wanyonge, kisimamie haki kwahiyo lazima nizingatie na nitahakikisha kwamba heshima yake na kazi zake nzuri alizoziifanya zinaendelea kuwa kumbukumbu katika Taifa hili"

"Tuendelee kuombeana sana kwa maana mafisadi kwenye hii nchi wapo wengi bado hawajaisha, mafisadi na wanaotaka Uongozi na wakati sifa hawana bado wapo kwahiyo wakiona nasimamia hivi utekelezaji wa Ilani lazima watataka kutuchonganisha"

"Na najua hii ziara ya kanda ya ziwa tuliyoanza nayo imewavuruga kweli na si kwa watoa taarifa tu hata wale waliopo ndani ya chama ambao wanataka kuvuruga chama na kumvuruga Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili wao watake kuchukua nafasi ya urais , sasa nawaambie nimepewa fimbo hapa na familia ya Mwl. Nyerere nitaitumia kuwachapa kwelikweli"

Cde. Paul Makonda
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo.

15 Novemba, 2023
#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendaNaMama
 
Kuna kutangulizwa mbele pia. Unapewa Kamba ya kutosha, kiti kinachofaa na mazingira conducive ya ‘kujinyonga’ kwa mikono yako mwenyewe.


Kama huu ni mtego kwake watakua wamemuweza vibaya, maana kazi yao anaifanya na ataitimiza kwa asilimia nyingi huku akilichimba kaburi kwa mikono yake! Nani ataliingia kaburi, yeye au wao?





Tuko nyakati muhimu kisiasa, history inaandikwa na itakumbukwa.
 
Back
Top Bottom