Mara ya kwanza kuingia Gerezani 2017, sikulala hakika Sitosahau

Mara ya kwanza kuingia Gerezani 2017, sikulala hakika Sitosahau

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Ilikuwa 2017 nilipoingia Gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa la kutoa lugha ya kuudhi dhidi ya Rais wa Tanzania kipindi hicho John Pombe Magufuli.

Kweli wakuu Nilimtukana Rais wa JMT tena kwa lugha Kali hii ni baada ya Kupata hasira za hapa na pale.

Ilikuaje nikamtukana Rais maneno makali, hapa ni baada kusikia kuwa hela za Tetemeko tulizowachangia wahanga hazitowafikia hata senti 100.

Hakika jambo hili lilinifanya kumtukana Rais matusi ya kutosha.

Baada ya kumtukana Rais nilikamatwa na Makachero na kuniweka kizuizini siku 08 ndipo nilipewa dhamana.

Baada ya dhamana niliendelea kuripoti kituo Cha police kila siku.

Na baada ya hapo nilipelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka 03 yote yanahusu kumtukana Rais na kumdhalilisha.

Baada ya kufika mahakamani nilikana kosa na kupelekwa Gerezani moja kwa moja maana nilikosa wadhamini.

Nilikaa Gerezani siku 23 ndipo nilipatiwa dhamana.

Kesi yangu ilichukua Mwaka 1 tu na niliachiwa huru na wale wote wapepelezi kutoka upande wa Jamhuri walifariki wote na Mwanasheria aliyeniachia huru kupitia Nole sahivi Ni jaji wa Mahakama kuu Maana aliteuliwa na Magufuli 2019.

Maisha ya jela
Ukweli Ni kwamba Gerezani Kuna watu wanaishi vizuri sana kama vile wapo nje pia kuna watu wanaishi motoni

ITAENDELEA
JE ILIKUAJE NIKAACHIWA HURU KWA KESI NZITO KAMA HIYO LICHA YA KUTOKUWA NA PESA.
 
Ilikuwa 2017 nilipoingia Gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa la kutoa lugha ya kuhudhi dhidi ya Rais wa Tanzania kipindi hicho John Pombe Magufuli.

Kweli wakuu Nilimtukana Rais wa JMT tena kwa lugha Kali hii ni baada ya Kupata hasira za hapa na pale.

Ilikuaje nikamtukana Rais maneno makali , hapa ni baada kusikia kuwa hell za Tetemeko tulizowachangia wahanga hazitowafikia hata senti 100
Hakika jambo
Acha ujinga kijana. Sisi mbona tulikichangia chama chetu pale Mbagala (uchaguzi mkuu), na matokeo yake mwenyekiti wetu michango yetu akaenda kuzipigia bapa zote usiku ule. Sisi wala hatukumtukana.

images (39).jpeg
 
Alisema mtanikumbuka [emoji849]. Ni muda ss umepita lkn bd watu wanazd kumkumbuka. Kwa mazuri na mapungufu yake....
 
Pole sana, lakini inafikirisha kwa nini wale wote wapepelezi kutoka upande wa Jamuhuri walifariki?. Anyway dunia ina mengi.
 
Ilikuwa 2017 nilipoingia Gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa la kutoa lugha ya kuhudhi dhidi ya Rais wa Tanzania kipindi hicho John Pombe Magufuli.

Kweli wakuu Nilimtukana Rais wa JMT tena kwa lugha Kali hii ni baada ya Kupata hasira za hapa na pale.

Ilikuaje nikamtukana Rais maneno makali , hapa ni baada kusikia kuwa hela za Tetemeko tulizowachangia wahanga hazitowafikia hata senti 100
Hakika jambo hili lilinifanya kumtukana Rais matusi ya kutosha

Baada ya kumtukana Raisi nilikamatwa na Makachero na kuniweka kizuizini siku 08 ndipo nilipewa dhamana.

Baada ya dhamana niliendelea kuripoti kituo Cha police kila siku.

Na baada ya hapo nilipelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka 03 yote yanahusu kumtukana Rais na kumzalilisha.

Baada ya kufika mahakamani nilikana kosa na kupelekwa Gerezani moja kwa moja maana nilikosa wadhamini.

Nilikaa Gerezani siku 23 ndipo nilipatiwa dhamana .

Kesi yangu ilichukua Mwaka 1 tu na niliachiwa huru na wale wote wapepelezi kutoka upande wa Jamuhuri walifariki wote na Mwanasheria aliyeniachia huru kupitia Nole sahivi Ni jaji wa Mahakama kuu Maana aliteuliwa na Magufuli 2019

Maisha ya jela
Ukweli Ni kwamba Gerezani Kuna watu wanaishi vizuri sana Kama vile wapo nje pia Kuna watu wanaishi motoni

ITAENDELEA
JE ILIKUAJE NIKAACHIWA HURU KWA KESI NZITO KAMA HIYO LICHA YAKUTOKUWA NA PESA .
Saizi tukana mpaka uchoke, keshakufa
 
Gereza ni sawa na kuzimu, nyampara kijana mdogo anampiga mzee mtu mzima bila heshima kwa kosa dogo, ila kuna ambao wanaona gereza ni paradiso, wanakula chakula cream na wana afya kuliko maisha yao ya nje. Nyampara ndio huishi vizuri gerezani
 
Hebu Ngoja kwanza. Ni wewe au Unatuletea Hadithi za Kutunga.? Mambo ya. ITAENDELEA yanatoka wapi
 
Kesi yangu ilichukua Mwaka 1 tu na niliachiwa huru na wale wote wapepelezi kutoka upande wa Jamuhuri walifariki wote na Mwanasheria aliyeniachia huru kupitia Nole sahivi Ni jaji wa Mahakama kuu Maana aliteuliwa na Magufuli 2019
Dah!... Nini sababu ?
 
Back
Top Bottom