SEHEMU YA PILI
Wakati kesi ikiendelea Katika Mahakama ya wilaya mkoani x nilianza kushauliwa na ndugu na Jamaa wangu wakaribu kuwa niende kwa Mganga kumaliza hii kesi
Baada ya kupewa ushauri , Mimi nilikataa kutumia Ndumba zozote Bali nilisema ikitokea nimefungwa itabidi nitumikie tu kifungo .
Wakati kesi ikiendelea nilimuomba sana Mungu anivushe maana sikukusudia mtukana Rais bali ni yeye Raisi ndo alituletea Maneno ya kuhudhi kipindi kile amekuja Bukoba na kudai kuwa Hatowapatia Wahanga wa Tetemeko hela zao tulizowachangia. Na Mimi ndipo Nilimtukana Live kwa kumuita katili asiyekuwa na Huruma dhidi ya Binadamu wenzio .
Jambo hilo lilizua Gumzo kwani niliongea hayo Maneno Mbele yake na nilikuwa na umri Mdogo 19 years tu.
Zipi sababu za kufariki wapelelezi was kesi yangu wote .
Ukweli hawa wapelelezi waliniomba sana pesa ili kunisaidia na niliwaambia hakuna pesa ya Bure. Jambo ili liliwakera hadi kuanza kunikandamiza Mahakamani ili tu nifungwe.
Nilichofanya Ni kuwaombea Dua tu kuwa washindwe wao na nia zao hasi juu yangu.
Maaajabu hii kesi watu 90% walikuwa upande wangu kuanzia hakimu , wanasheria wa serikali hadi Wananchi.
Hivyo Basi Hakimu na mwanasheria was serikali na DPP wote walisema dogo yupo kwenye haki na anabidi kuachiwa huru maana huyu Rais amezidi kuendekeza kunyanyasa watu.
Jambo hili lilinifanya nimshukuru sana Mungu kwani ukiwa upande wake hakuna linaloshindikana.
Maisha ya Gerezani , ukweli Gerezani hasa Tanzania sio sehemu salama maana watu wengi wananyimwa haki zao muhimu Kama kula , kuabudu , kusoma n.k
Kuhusu ushoga Mimi Jambo hili sijaliona Wala kulisikia maana Mimi nilitengwa nikawa tunakaa sero yenye watu 04 tu VIP maana Mimi nilikuwa moja ya watu waliokuwa wanaogopwa wakidhani eti Mimi natumiwa na Tiss hakika maaskari wetu kitaaluma Bado sana.
Hali za watu Gerezani
Kiukweli niliwaona watu wamekonda na wamechoka sana na wamekaa Gerezani Muda mrefu wakiwa mahabusu , Aisee hapa panaumiza watu haki. Zao zinavunjwa sana
MSAADA WANGU NIKIWA GEREZANI WAFUNGWA
Nilifanikiwa kuwaandikia watu 05 rufaa zao waliokuwa na kesi mbalimbali na sasa wapo huru 03 na wawili wamepunguziwa Adhabu kutoka life sentences hadi miaka kadhaaa.
Ni hayo tu ndugu zangu.
NYONGEZA
Ukweli ni kwamba wapelelezi walifariki baada kesi yangu kufutwa mahakamani pia hata Mwanasheria wa serikali aliyepewa Ujaji alipewa baada ya kuwa amefuta kesi yangu
Japo haya Matukio yalifatana sana. Ilikuwa ni ndani ya Mwezi mmoja .