Mara ya kwanza kuingia Gerezani 2017, sikulala hakika Sitosahau

Na usikute unaona na ukawa unaona umeonewa si ndyo?..

Vijana wengi hamjuwi kujenga hoja wala kupinga kwa hoja zaid ya matusi bila kujari unaye mtusi ni mtu mzima na kiongozi mkubwa, na kuna wapumbavu wanaweza kukuunga mkono kwa upuuzi uliofanya.

Hayo mambo ya haki za kijinga jinga za kuzalilisha viongozi, zipo huko magharib ambako wanajiona wana Uhuru uliopitiliza, kiafrika na kitamaduni ni kosa kumtusi kiongozi wako hatakama anakosea, mrekebishe kistaharabu.

Mkome na wengine jifunzeni
 
Tangazo tangazo limefika
 
Hapo watu wataanza kukufuata PM kukutaka uwaoneshe mganga uliyetumia kupangua msala huo, na kuna wengine watakuja hapa hapa kukuuliza kama uliliwa kiboga na wakati kiboga kinatafunwa ulikuwa unajisikiaje
 
Yani hii stori nayo ni ya kufupisha Hadi useme itaendelea Kama vile ulikaa gerezani miaka 30? We Nesi wa jela nini?
 
SEHEMU YA PILI

Wakati kesi ikiendelea Katika Mahakama ya wilaya mkoani x nilianza kushauliwa na ndugu na Jamaa wangu wakaribu kuwa niende kwa Mganga kumaliza hii kesi

Baada ya kupewa ushauri , Mimi nilikataa kutumia Ndumba zozote Bali nilisema ikitokea nimefungwa itabidi nitumikie tu kifungo .

Wakati kesi ikiendelea nilimuomba sana Mungu anivushe maana sikukusudia mtukana Rais bali ni yeye Raisi ndo alituletea Maneno ya kuhudhi kipindi kile amekuja Bukoba na kudai kuwa Hatowapatia Wahanga wa Tetemeko hela zao tulizowachangia. Na Mimi ndipo Nilimtukana Live kwa kumuita katili asiyekuwa na Huruma dhidi ya Binadamu wenzio .

Jambo hilo lilizua Gumzo kwani niliongea hayo Maneno Mbele yake na nilikuwa na umri Mdogo 19 years tu.

Zipi sababu za kufariki wapelelezi was kesi yangu wote .

Ukweli hawa wapelelezi waliniomba sana pesa ili kunisaidia na niliwaambia hakuna pesa ya Bure. Jambo ili liliwakera hadi kuanza kunikandamiza Mahakamani ili tu nifungwe.

Nilichofanya Ni kuwaombea Dua tu kuwa washindwe wao na nia zao hasi juu yangu.

Maaajabu hii kesi watu 90% walikuwa upande wangu kuanzia hakimu , wanasheria wa serikali hadi Wananchi.

Hivyo Basi Hakimu na mwanasheria was serikali na DPP wote walisema dogo yupo kwenye haki na anabidi kuachiwa huru maana huyu Rais amezidi kuendekeza kunyanyasa watu.

Jambo hili lilinifanya nimshukuru sana Mungu kwani ukiwa upande wake hakuna linaloshindikana.

Maisha ya Gerezani , ukweli Gerezani hasa Tanzania sio sehemu salama maana watu wengi wananyimwa haki zao muhimu Kama kula , kuabudu , kusoma n.k

Kuhusu ushoga Mimi Jambo hili sijaliona Wala kulisikia maana Mimi nilitengwa nikawa tunakaa sero yenye watu 04 tu VIP maana Mimi nilikuwa moja ya watu waliokuwa wanaogopwa wakidhani eti Mimi natumiwa na Tiss hakika maaskari wetu kitaaluma Bado sana.

Hali za watu Gerezani
Kiukweli niliwaona watu wamekonda na wamechoka sana na wamekaa Gerezani Muda mrefu wakiwa mahabusu , Aisee hapa panaumiza watu haki. Zao zinavunjwa sana

MSAADA WANGU NIKIWA GEREZANI WAFUNGWA

Nilifanikiwa kuwaandikia watu 05 rufaa zao waliokuwa na kesi mbalimbali na sasa wapo huru 03 na wawili wamepunguziwa Adhabu kutoka life sentences hadi miaka kadhaaa.

Ni hayo tu ndugu zangu.

NYONGEZA

Ukweli ni kwamba wapelelezi walifariki baada kesi yangu kufutwa mahakamani pia hata Mwanasheria wa serikali aliyepewa Ujaji alipewa baada ya kuwa amefuta kesi yangu

Japo haya Matukio yalifatana sana. Ilikuwa ni ndani ya Mwezi mmoja .
 
Natumaini sio tangazo la uganga maana mwanzo tu wa stori umeshaua wapelelezi woote waliohusika na kesi yako
 
Yaan askari wakuogope wewe waache kuwaogopa akina mbowe jela hakunaga umaarufu kwanza
 
Ukiweza ishi jela za bongo kuzimu cha mtoto utoshindwa kuishi
 
Jela zingekuwa kwa ajili ya matajiri na wanasiasa zingekuwa chuo cha mafunzo, pia zingeboreshwa. Jela ni jehanamu ndogo duniani
 
Hapo watu wataanza kukufuata PM kukutaka uwaoneshe mganga uliyetumia kupangua msala huo, na kuna wengine watakuja hapa hapa kukuuliza kama uliliwa kiboga na wakati kiboga kinatafunwa ulikuwa unajisikiaje
Kashasema hakuliwa hapo kwenye Part II; sijui ni kweli hakuliwa au anatudanganya?
 
hii chai imepoa kabisa eti uliwaandikia mahabusu wenzako 05 rufaa zao kwanza hapo ulikuwa na elimu gani na uzoefu upi hadi ukaandikia rufaa mahabusu wenzako kwanza tangu lini mahabusu akawa na rufaa kabla ya kuhukumiwa maana umesema mwenyewe kipindi hiko ulikuwa na miaka 19 tu..acha kutufanya sisi mazuzu
 
Hii ni zaidi ya chai,
Hii ni alkasusu.

Unasema wanainchi pamoja na mahakimu wote walikuwa upande wako.

Sababu rais alikuwa ananyanyasa watu.

Umesahau kwamba ulikiri kutoa lugha ya matusi kwa rais.
 
Hii ni zaidi ya chai,
Hii ni alkasusu.

Unasema wanainchi pamoja na mahakimu wote walikuwa upande wako.

Sababu rais alikuwa ananyanyasa watu.

Umesahau kwamba ulikiri kutoa lugha ya matusi kwa rais.
Nisha shuhudia Mtuhumiwa wa Jambazi, karani na Hakimu wanapiga stories kabla ya kesi kwa tabasamu kuuuuubwa.

Hapakua na ushahidi wa kutosha...imefika muda jamaa anahojiwa anajibu kwa kwa kujiamini na tabasamu paaaana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…