Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
Baada ya kufika Kigoma nikakaa siku kama ya 3 hivi nikasema niende mjini , nikaenda barabarani Buzebazeba ( ndo nilipofikia), ilikuwa jioni , nikagundua kumbe
1. Kigoma hakuna foleni barabarani.
2. Hakukuwa na dalalada za mjini kama huku Bali Kuna vibajaji.
Basi nikapanda kibajaji , njiani namwambia dereva
"Vipi hakuna foleni , tutawahi kufika".
Dereva akanishangaa😅, akanambia "huku hakunaga foleni", nikasema "weee, kumbe". Baada ya dakika kadhaa kweli tukawa tumefika Kigoma mjini ( mwisho wa reli).
3. Watoto wa kule ni wakubwa tofauti na umri wao.
Pale kwa wenyeji wetu kulikuwa na Wasichana , ukiwaangalia mimi na wao tulikuwa kimo sawa na wengine walinizidi , kumbe bhana ni vitoto😅 ila miili mikubwa.
Nilijua hayo siku alipokuja mtoto wa mwenyeji wetu kutuona, wakati wa maongezi ndo akataja umri wake , miaka 16 , ukimwangalia sasa huyo msichana wa miaka 16 na mimi wakati huo 21 heee!! Yeye mkubwa mimi mdogo. Nikaulizia na wale wengine eti miaka 15, 16, 17 hakuna 18 , duuh!! Nikasema tembea uone.
4.Samaki fresh kutoka baharini zinanenepesha.
Ndani ya mwezi mmoja wa kukaa hapo nguo nilokuja nazo zikawa ndogo, zinanibana nimefutuka balaa, nikafanya udadisi bhanaa, kumbe ni zile samaki( migebuka) inatoka Moja kwa moja baharini tunaila ikiwa fresh ndo inatunenepesha, kwahiyo vile vitoto vinanenepeshwa na migebuka na marumbu.
5. Mzunguko mdogo wa pesa miaka nenda miaka rudi.
Kumbe ndomna waha wanang'ang'ania dar, kgma mzunguko wa pesa upo taratiibu sanaa, dar unaweza kuishi kwa kuuza barafu na ice cream sio kigoma, unamuzia nani!?.
6. Wanawake ndo watafutaji kwa asilimia kubwa.
Kila utakapokatiza unakutana na wanawake na mashuka Yao, hata wakiwa kwenye mikutano wapo nayo, masokoni ndo usiseme wamejaa, waume zao wapo kwenye vijiwe vya kahawa wanajadili ACT wazalendo, akirudi akute ugali umeiva.
7. Wanaume wa gungu ni wajuaji kuliko sehemu zingine.
Yaani wanaume wa gungu unaweza ukabishana nao mpaka asubuhi bila kuchoka, Kila kitu wanajua wao, hakuna wasichokijua.
Ni mji Mzuri kwa kupumzisha akili ila kimaisha mgumu sana.
Najipanga nirudi tena.