Mara ya mwisho kumwambia Mwanao unampenda ni lini?

Mnaiga umagharibi na hizo gender studies zenu halafu mnataka kuyaleta Africa. Magharibi kumeoza chakushangaza eti ndio mifano yetu. Unafikiri mtoto hana inteligensia kichwani, anayo tangu miaka 3.
 
Mtoto muoneshe Kwa Vitendo upendo atauona tu . Kumtamkia unampenda haitoshi
Ni kweli, na ni muhimu pia akajua. Usije kuashum kuwa anajua sababu tu unatimiza wajibu wako kama baba
 
Mi siwaambii ila wanajua nawapenda. Kuna huyu wa kiume ye ndo huwa kila mara lazima aniambie "mama nakupenda".Mdogo wake pia akimaliza ananiuliza "mama na we unanipenda?"
Umejuaje kama wanajua? Kama kila siku anakuuliza hivyo huoni kunashida yoyote?
 
haya mambo mnayatoa wapi hivi?
upendo wa wazazi kwa mtoto au watoto ni kimatendo zaidi
Mbali na matendo akisikia kutoka kwako ni vizuri zaidi.... Si kwa ubaya, ni kumhakikishia upo hapo kwa ajili yao. Inaweza ukawa unaashumu wao wanajua lakini ikawa siyo hivyo. Tujitahidi kuongea na watoto wetu
 
Mnaiga umagharibi na hizo gender studies zenu halafu mnataka kuyaleta Africa. Magharibi kumeoza chakushangaza eti ndio mifano yetu. Unafikiri mtoto hana inteligensia kichwani, anayo tangu miaka 3.
Kumwambia mtoto wako unampenda ni kuiga umagharibi? Halafu mtoto akikua akiwa anampenda mzazi mmoja mnaanza kulaumu. Mbali na kutimiza majukumu yako kuhakikisha anavaa, kula nk, unaongea na mwanao? Mtoto wako anafeel your presence kwao?
 
Kumwambia mtoto wako unampenda ni kuiga umagharibi? Halafu mtoto akikua akiwa anampenda mzazi mmoja mnaanza kulaumu. Mbali na kutimiza majukumu yako kuhakikisha anavaa, kula nk, unaongea na mwanao? Mtoto wako anafeel your presence kwao?

Mkuu moja ya sentensi za kinafiki dunia ni neno nakupenda. Sishauri umwambie mtoto hivi wewe zingatia vitendo watoto wanajifunza Kwa vitendo kuliko maneno na wanaona. Ndo maana wazazi wetu hawakutwambia haya maneno lakini tunawapenda mpaka kesho , mtoto anachapwana na mama yake ndani ya dk 20 keshasahau wanacheka, sasa mchape wewe stranger uone dogo atakuweka akilini milele, unajua hapa ni Kwa nini ? Mtoto anatambua upendo wa kweli wa mama yake kupitia vitendo

Nakupa Mfano mwingine , kuna wale masela unakuta wanapendana Kama ndugu lakini kamwe hutosikia neno nakupenda kati Yao hutosikia kamwe lakini they are there for each other iwe jua iwe mvua, bunafsi Nina marafiki wa hivi wachache sana hawazidi wanne.

Hata mbwa wako hapo nyumbani anajua Nani anampenda bila kumwambia maneno nakupenda

Zingatia vitendo achana na mambo ya nakupenda za asubuhi mchana na jioni . Nakupenda ni neno la kinafki sana
 
Jamani haya watamkieni,wato hata watakushangaa na wata anza kudeka, huyo mke tu kumwambia nakupenda nilimwambia kipindi cha uchumba ....upendo unaonyeshwa kwa matendo tu....hata uyo mke au mtoto umwambie nakupenda then chakula ndani hkn, nguo hawana, etc haisaidii
 
Wazaz wangu najua wananipenda balaa hasahasa mzee wangu. Ila hajawahi tamka hilo neno. Upendo wa mzazi huonekana tu hata ile closeness .
Nje wa mada kidogo .nimedate na wanawake kadhaa lkini neno nakupenda halijawahi kutoka kati yetu mwanzoni lbda baadae sijui ndo mnaitaga "love at first sight"?
 
Kuambia mtoto nakupenda so lazima kwa mtoto kujua anapendwa.
Haijawahi tokea ww kuliliwa either na mtoto wa jirani kila akikuona tu anakukimbilia ni kusema kwa sababu ulisema "nakupenda mtoto"?
No, ila issue ni ile "CLOSENESS".
 
Nimwambie nampenda ili iweje? Ataambiwa na mama yake! Kwangu mimi ni utani kidogo na bakora kwa mbali..
 
Usimwambie mtoto unampenda. Are you a crazy Westerner,or what?
Makid ya now days. kizazi cha pampas. unawezaliambia litoto la kike likaona Mshua kaelewa Mzigo. Kifuatacho sasa!! hutakaa uamini. labda hizi zifanyike huko masaki,capripoint,forest, uhidini na place kaa hizo. lakini mbagala,bugalika,Matola, nyihogo, kanyenye,sombetini,Chogo au buzebazeba? utaishia kuchumishwa tunda na utalila tu kama Mwanangu Adamu wa pande za Eden mapindi yale
 
Unamuonyeshaje mapenzi ya baba Mkuu?
Hakikisha anapata mahitaji muhimu, nguo kali, shule nzuri english medium, chakula kizuri, kumtomkaripia bila sababu ya maana, outing, kumpenda mama yake,kumfundisha kazi, kumjenga kiimani, kumtengenezea vision nk. Sio eti mwanangu Benard nakupenda.....kwanza dogo wangu ataniona nimeanza kudata
 
Unafikiri wanaolalamika watoto wao hawaoni mchango wao na kuona mchango wa mama pekee hawafanyi yote hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…