Mara ya mwisho kwenda kijijini kwenu ni lini

Mara ya mwisho kwenda kijijini kwenu ni lini

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
11,261
Reaction score
17,202
Najua wengi wetu tuko mijini kiutafutaji,lakini kiasili tuna maeneo yetu ya asili ambayo tunatokea,wengine husema kwenye asili ya ukoo.binafsi weekend iliyopita nilikua huko.

Haijalishi kama babu na bibi walishafariki au la lakini bado naamini kuna ndugu wapo..je unakumbuka mara ya mwisho kwenda kijijini kwenu ni lini?
 
Najua wengi wetu tuko mijini kiutafutaji,lakini kiasili tuna maeneo yetu ya asili ambayo tunatokea,wengine husema kwenye asili ya ukoo.binafsi weekend iliyopita nilikua huko.Haijalishi kama babu na bibi walishafariki au la lakini bado naamini kuna ndugu wapo..je unakumbuka mara ya mwisho kwenda kijijini kwenu ni lini?

Kabla ya weekend iliyopita, mara ya mwisho ulienda lini?
 
Safi sana...nadhani mnaongoza kwa kuthamini kwenu..kuhesabiwa sio?
Ndio mkuu kuhesabiwa ni fahari..Pia tunaenda kuangalia what's poppin..Mijengo mipya iliyodondosha nini nini..Na kikubwa tunakutana na marafiki wa zamani sababu wengi pia wanarudi kuhesabiwa
 
Ndio mkuu kuhesabiwa ni fahari..Pia tunaenda kuangalia what's poppin..Mijengo mipya iliyodondosha nini nini..Na kikubwa tunakutana na marafiki wa zamani sababu wengi pia wanarudi kuhesabiwa
Nakubali kaka..nadhani hii pia inaongeza hasira ya utafutaji kwa wengi wenu,unakuta jamaa yako mlipiga wote shule unaoneshwa mjengo wake,na kama unavyojua wengi wanamiliki ndinga za maana.,kwahiyo inastimulate utafutaji.
 
Back
Top Bottom